Monday, 8 February 2016
Sunday, 7 February 2016
Ajali ya gari la mafuta Kibaigwa Dodoma
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Ripoti
kutoka Dodoma leo ni hii ya ajali ya gari la mafuta
lililodondoka na kulipuka katika eneo la Kibaigwa, hadi sasa hakuna
taarifa kamili ya ajali hii.
Wanafunzi Shule ya Kivukoni Wanasomea Kwenye Vibanda vya nyasi na Manailoni Ruvuma.
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Wanafunzi katika shule ya msingi Kivukoni iliyoko mpakani mwa Tanzania na Msumbiji wilayani Songea mkoani Ruvuma wanasomea katika vibanda vilivyoezekwa kwa makaratasi ya nailoni na nyasi baada ya majengo ya shule yao zikiwemo ofisi za walimu kuharibiwa na ufa na hivyo walimu wameomba watalaamu wa miamba kuchunguza tukio hilo.
Kufuatia tukio hilo la shule hiyo yenye miaka kumi na nane kuharibiwa kwa ufa uliopasua sakafu na kuta zote za shule hadi nje ya shule walimu wa shule hiyo wameiomba serikali kutuma watalaamu wa miamba kuchunguza tukio hilo.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Kivukoni Bw. Hakim Kais amesema shule hiyo kuharibiwa na ufa ni maafa na kuomba serikali ya wilaya kuwasaidia kupitia mfuko wa maafa badala ya kuagiza wachangishane shilingi elfu ishirini kila mwananchi huku mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw. Erick Ndunguru akiiomba serikali kusaidia ujenzi wa shule hiyo kwani wanafunzi wamekuwa watoro kutokana na mazingira magumu ya kusomea.
Wanafunzi wa shule hiyo wanaelezea mazingira magumu wanayosomea na kuiomba saerikali kuharakisha ujenzi wa shule hiyo ambapo toka shule imefungua wanafunzi kumi na tano hawajaripoti kutokana na mazingira magumu ya kusomea.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Songea Bw. Sigsbert Valentine amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza jitihada zilizofanyika.

Saturday, 6 February 2016
MPYA:HAYA HAPA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2015
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Tunakuletea matokeo hayo mda si mrefu endelea kutembelea maswayetu blog

RAIS MAGUFULI AKIWA SINGIDA KWENYE SHEREHE ZA KUZALIWA CHAMA CHA CCM
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na wanachama wote wa CCM
katika sherehe za maadhimisho ya miaka 39 ya Chama hicho zilizofanyika
leo tarehe 06 Januari, 2016 katika uwanja wa Namfua, Mjini Singida.
Viongozi wengi waliohudhuria sherehe hizo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mheshimiwa Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana pamoja na Wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, pamoja na kuwashukuru wananchi wa Singida kwa kumchagua kwa kura nyingi kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Magufuli amewaahidi kuwa atahakikisha serikali yake inatekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020 kikamilifu ili kila mtanzania anufaike na matunda ya nchi yake.
Amebainisha kuwa serikali yake imedhamiria kufanya kazi kwelikweli chini ya kauli mbiu ya "Hapa Kazi Tu" huku akionya kuwa watendaji wa serikali ambao watashindwa kutekeleza ilani ya CCM wataondoka.
Rais Magufuli ameupongeza mkoa wa Singida kwa kuchangisha fedha zilizofanikisha kutengeneza madawati 1,000 kwa ajili ya wanafunzi wa shule, na ameelekeza kuwa viongozi wa mikoa mingine waige mfano huo, vinginevyo watakuwa wamedhihirisha kuwa hawatoshi kuendelea na nyadhifa hizo.
"Haingii akilini viongozi wanakaa kwenye ofisi nzuri zenye viyoyozi lakini wanafunzi wakaa chini kwa kukosa madawati, na ikiwa hivyo, basi hicho ni kigezo tosha kuwa viongozi wa mkoa ama wilaya hiyo hawafai kuendelea na nyadhifa hizo" alisisitiza Rais Magufuli.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amesema kwa miaka 39 Chama hicho tawala kimefanikiwa kulinda amani, kusimamiwa usawa na uzalendo kwa watanzania na kwamba kinajivunia mafanikio hayo makubwa.
Dkt. Kikwete pia amempongeza Rais Magufuli, Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, kwa kazi nzuri wanayoifanya ambayo licha ya kukiongezea heshima Chama Cha Mapinduzi, imejenga matumaini na imani ya wananchi kwa chama chao na serikali yao.
"Naomba nikuhakikishie kuwa mimi na wana CCM wenzangu tunakuunga mkono na tunawatakia kila heri katika kutekeleza ilani ya CCM" alisema Dkt. Kikwete.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana, amesema CCM inampongeza kwa dhati Rais Magufuli kwa kazi nzuri aliyoanza kuifanya kwa kipindi cha siku 90 za tangu alipoapishwa kuwa Rais.
Ametaja baadhi ya kazi hizo kuwa ni kukabiliana na wizi wa mali ya umma, rushwa, kubana matumizi, matumizi mabaya ya madaraka na kudhibiti nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma.
"Rais Magufuli nakupongeza sana sana, unatekeleza uliyoyaahidi na wananchi wanafurahishwa sana. Endelea hivyo hivyo, mambo mazuri" Alisisitiza Ndugu Kinana
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dododma
06 Januari, 2016
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telegrams : "CABINET"
DAR ES SALAAM
Telephone : 2116898, 2116900/6
E-mail : chief@ikulu.go.tz
E-mail : ikulu@ikulu.go.tz
Fax : 2113425/2116914/2117272
DAR ES SALAAM
Telephone : 2116898, 2116900/6
E-mail : chief@ikulu.go.tz
E-mail : ikulu@ikulu.go.tz
Fax : 2113425/2116914/2117272
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD
11400 DAR ES SALAAM.
THE STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD
11400 DAR ES SALAAM.
Viongozi wengi waliohudhuria sherehe hizo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mheshimiwa Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana pamoja na Wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, pamoja na kuwashukuru wananchi wa Singida kwa kumchagua kwa kura nyingi kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Magufuli amewaahidi kuwa atahakikisha serikali yake inatekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020 kikamilifu ili kila mtanzania anufaike na matunda ya nchi yake.
Amebainisha kuwa serikali yake imedhamiria kufanya kazi kwelikweli chini ya kauli mbiu ya "Hapa Kazi Tu" huku akionya kuwa watendaji wa serikali ambao watashindwa kutekeleza ilani ya CCM wataondoka.
Rais Magufuli ameupongeza mkoa wa Singida kwa kuchangisha fedha zilizofanikisha kutengeneza madawati 1,000 kwa ajili ya wanafunzi wa shule, na ameelekeza kuwa viongozi wa mikoa mingine waige mfano huo, vinginevyo watakuwa wamedhihirisha kuwa hawatoshi kuendelea na nyadhifa hizo.
"Haingii akilini viongozi wanakaa kwenye ofisi nzuri zenye viyoyozi lakini wanafunzi wakaa chini kwa kukosa madawati, na ikiwa hivyo, basi hicho ni kigezo tosha kuwa viongozi wa mkoa ama wilaya hiyo hawafai kuendelea na nyadhifa hizo" alisisitiza Rais Magufuli.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amesema kwa miaka 39 Chama hicho tawala kimefanikiwa kulinda amani, kusimamiwa usawa na uzalendo kwa watanzania na kwamba kinajivunia mafanikio hayo makubwa.
Dkt. Kikwete pia amempongeza Rais Magufuli, Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, kwa kazi nzuri wanayoifanya ambayo licha ya kukiongezea heshima Chama Cha Mapinduzi, imejenga matumaini na imani ya wananchi kwa chama chao na serikali yao.
"Naomba nikuhakikishie kuwa mimi na wana CCM wenzangu tunakuunga mkono na tunawatakia kila heri katika kutekeleza ilani ya CCM" alisema Dkt. Kikwete.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana, amesema CCM inampongeza kwa dhati Rais Magufuli kwa kazi nzuri aliyoanza kuifanya kwa kipindi cha siku 90 za tangu alipoapishwa kuwa Rais.
Ametaja baadhi ya kazi hizo kuwa ni kukabiliana na wizi wa mali ya umma, rushwa, kubana matumizi, matumizi mabaya ya madaraka na kudhibiti nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma.
"Rais Magufuli nakupongeza sana sana, unatekeleza uliyoyaahidi na wananchi wanafurahishwa sana. Endelea hivyo hivyo, mambo mazuri" Alisisitiza Ndugu Kinana
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dododma
06 Januari, 2016
JOSE MOURINHO KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAN UNITED
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Manchester United imefanya mazungumzo na wawakilishi wa kocha wa zamani Chelsea Jose Mourinho, BBC imetambua.
Mreno, 53, ambaye alitupiwa virago na Blues mwezi Desemba, anaendelea kuwa na matumaini ya kumrithi Louis van Gaal Old Trafford.
Hakuna makubaliano yaliyofiki, na klabu haijatamka lolote, lakini makubaliano yameanza.
Mholanzi Van Gaal, 64, anatarajiwa kuondoka United mwishoni mwa msimu – mwaka mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika.
Hiyo itamuwekea njia wazi Mourinho, ambaye anajulikana kuwa atafurahia endapo ataichukua Old Trafford.

NACTE:CHUO CHA ST. DAVID COLLEGE OF HEALTH LOCATED IN KIMARA - SUKA, DAR-ES-SALAAM CHAFUNGWA
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
This release serves to inform the
Public that the Council (NACTE) by powers vested to it under Section
5(1)(a) of the Act (Cap 129) has directed the following:
Both institutions have been given 14 days to stop operating and show cause.
PRESS RELEASE
STOP ORDER AND NOTICE OF CLOSURE
1. Closure
of St. David College of Health located in Kimara - Suka, Dar-es-salaam
after finding it operating without registration and accreditation of the
Council and offering “unrecognized” programmes in Health related
fields; and
2. Cease
operations of Tanzania International University (TIU) of Kimara
Stop-Over related to Certificate and Diploma programs since the TIU had
no such permit from Tanzania Commission for Universities (TCU).
Both institutions have been given 14 days to stop operating and show cause.
Issued by:
EXECUTIVE SECRETARY
5th February 2016
ANGALIA MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA 2015/2016
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Standings Vodacom Premier League 2015/2016
Rnk | Team | MP | W | D | L | GF | GA | +/- | Pts | |||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | Young Africans | 17 | 12 | 4 | 1 | 38 | 9 | 29 | 40 | |||
2 | Simba SC | 17 | 12 | 3 | 2 | 32 | 10 | 22 | 39 | |||
3 | Azam | 15 | 12 | 3 | 0 | 30 | 10 | 20 | 39 | |||
4 | Mtibwa Sugar | 17 | 9 | 5 | 3 | 20 | 11 | 9 | 32 | |||
5 | Mwadui | 17 | 8 | 4 | 5 | 19 | 15 | 4 | 28 | |||
6 | Stand United | 16 | 9 | 1 | 6 | 17 | 13 | 4 | 28 | |||
7 | Tanzania Prisons | 16 | 8 | 4 | 4 | 18 | 17 | 1 | 28 | |||
8 | Toto African | 17 | 4 | 6 | 7 | 15 | 21 | -6 | 18 | |||
9 | Mbeya City | 17 | 4 | 5 | 8 | 15 | 22 | -7 | 17 | |||
9 | Mgambo JKT | 17 | 4 | 5 | 8 | 15 | 22 | -7 | 17 | |||
11 | Ndanda | 17 | 3 | 7 | 7 | 15 | 18 | -3 | 16 | |||
12 | Kagera Sugar | 17 | 4 | 3 | 10 | 9 | 20 | -11 | 15 | |||
13 | Coastal Union | 17 | 2 | 7 | 8 | 10 | 18 | -8 | 13 | |||
14 | JKT Ruvu | 17 | 3 | 4 | 10 | 17 | 29 | -12 | 13 | |||
15 | Majimaji | 17 | 3 | 4 | 10 | 10 | 31 | -21 | 13 | |||
16 | African Sports | 17 | 3 | 3 | 11 | 5 | 19 | -14 | 12 |