Mlinzi wa Kampuni ya Bonite, aliyetambulika kwa jina la Shamba baada ya kupigwa risasi na majambazi mjini Moshi.
Dereva wa Kampuni ya Bonite aliyetambulika kwa jina moja la Mselemu mara baada ya kushambuliwa kwa risasi na majambazi.
...wakiwa kwenye gari baada ya kushambuliwa kwa risasi na majambazi.
Mlinzi baada ya kuuawa na majambazi.
MAJAMBAZI
yaliyokuwa na silaha yamevamia gari mali ya Kampuni ya Bonite na
kuwamiminia risasi dereva wa gari hilo aliyetambulika kwa jina moja la
Mselemu na mlinzi wa Kampuni hiyo aliyetambulika kwa jina la Shamba
kisha kupora fedha na kutokomea kusikojulikana.
Tukio hilo limetokea jana mjini Moshi ambapo majambazi wanne
waliokuwa kwenye pikipiki walivamia gari la Bonite lililokuwa likitoka
kuchukua pesa za mauzo ya kampuni hiyo.
Taarifa zinadai kuwa dereva na mlinzi wa gari lililoshambuliwa
walifariki palepale kutokana na kupigwa risasi nyingi sehemu mbalimbali
za miili yao.
Hujulikana sana kwa maringo yake,lakini kwa kweli Kanye West asingekufuru na kujitambulisha kama mungu katika biblia hiyo.
Kitabu
hicho kitukufu kimebadilishwa na kuwa Biblia ya sasa kwa jina
''Yeezus'' na amini usiamini kila neno la Mungu katika kitabu hicho
limeondolewa na badala yake msanii huyo wa muziki wa kufoka foka ameweka
jina lake.
Kulingana na gazeti la The Independence nchini Uingereza,kitabu hicho kinasema kuwa katika kizazi hiki ,Kanye West ndio mkubwa na vile vile kiongozi wa kidini
Kitabu hicho kinaongezea kwamba ''katika utangulizi wetu tunamsherehekea Kanye West na vile alivyotufanyia katika maisha yetu''
Japokuwa Kanye hajatoa tamko lolote kuhusu wadhfa huo aliojipatia,amekuwa akijifananisha na Mungu hapo mbeleni.
''Mungu alinichagua mie,alinitengezea njia.Mimi ni chombo cha mungu'',alisema mwaka 2009.
''Lakini kinachoniudhi maishani mwangu ni kwamba sitawahi kujiona nikicheza muziki moja kwa moja''.,aliongezea.
Wasanii wengine waliofananishwa na Yeezy ni Marilyn Monroe na Michael Jackson.