Friday, 13 June 2014
SOMA:BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2014/2015
HOTUBA YA MHESHIMIWA WAZIRI WA FEDHA, SAADA MKUYA SALUM (MB) AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA FEDHA KWA MWAKA 2014/15
UTANGULIZI:
1. Mheshimiwa Spika, kufuatia
taarifa iliyowasilishwa hapaBungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, naomba kutoa hoja kwamba Bunge
lako Tukufu likubali kupokea, kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato
na Matumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2014/15.
2. Mheshimiwa Spika, awali
ya yote napenda kumshukuruMwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa
kuniwezesha kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara ya mwaka 2014/15.
Aidha, natoa shukrani zangu za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuniteua kuwa Waziri wa
Fedha. Ninaahidi kwamba nitatekeleza jukumu hili kwa weledi na uadilifu.
Vile vile, nawapongeza Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mhe. Adam
Kighoma Ali Malima (Mb) kwa kuteuliwa kuwa Naibu Mawaziri wa Wizara ya
Fedha. Kadhalika, namshukuru pia aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha Mhe.
Janeth Zebedayo Mbene (Mb) kwa utendaji kazi wake mahiri na tunamuombea Mwenyezi
Mungu ampe nguvu na afya njema katika kazi zake mpya Wizara ya Viwanda
na Biashara. Nichukue pia fursa hii kumpongeza Bw. Rished M. Bade kwa
kuteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
MAHUSIANO:TAMU WA KUNYONYWA, UMPATE MNYONYAJI ANAYEJUA KUNYONYA...!
Thursday, 12 June 2014
MATOKEO KOMBE LA DUNIA DK YA 75 :BRAZIL 2 CROTIA 1
HATIMAE,
Fainali za Kombe la Dunia zinaanza Leo hii huko Sao Paulo, Brazil
wakati Wenyeji Brazil wataivaa Croatia katika Mechi ya Kwanza ya Kundi A
itakayochezwa Arena Corinthians, au kwa Jina jingine Arena de Sao
Paulo.
SIKILIZA MAJIBU YA MBUNGE SALVATORY MACHEMLI WA CHADEMA KUHUSU PICHA ZA UTUPU ZILIZOSAMBAZWA MITANDAONI ZENYE SURA YAKE
Siku chache zilizopita kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii
zilisambazwa picha mbalimbali za Wabunge wa Bunge la Tanzania
zikionyesha wakiwa kwenye sehemu za faragha sehemu ambazo hutumiwa zaidi
na wapenzi na zaidi ni namna picha hizo zilivyotoka maana zingine zilikua ni
zaidi ya nusu utupu.
Salvatory Naluyaga Machemli mbunge wa Ukerewe kupitia Chadema ni
miongoni mwa wabunge waliotajwa kuwepo kwenye orodha hiyo na ni baada ya
kusambaa kwa picha zinazomuonyesha akiwa na binti wakiwa zaidi ya nusu
utupu,Soudy brown akaongea naye.Majibu na kila kitu kilichozungumzwa kipo hapo chini. ANGALIA VIDEO HAPA
WAZIRI ANUSURIKA KUFA AKIWA NA GARI LAKE
Gari la Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka likiwa katika kituo cha polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga baada ya kugonga punda |
DENTI YATIMA AKATWA MGUU
KUELEKEA KOMBE LA DUNIA HII NDIO MISHAHARA YA MAKOCHA WA KOMBE LA DUNIA
Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza,
Fabio Capello ndiye anaongoza kwa kulipwa vizuri miongoni mwa makocha
wote wa timu za taifa zinazoshiriki Kombe la Dunia mwaka huu nchini
Brazil.