Friday, 9 May 2014

UFUSKA BONGO MOVIE WAMKOSESHA DILI NORA


MWANADADA wa ‘long time’ kwenye sanaa ya uigizaji amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukosa dili za kazi za maana kutokana na tabia za kifuska kwa baadhi ya wasanii wa kike wa Bongo Movie.
Msanii Nora.
Akipiga stori na paparazi wetu, Nora alisema amekuwa akitembelea katika ofi si mbalimbali
na kila anapojitambulisha kwamba ni msanii wa fi lamu watu wanashtuka na sehemu nyingine anakosa dili za maana kutokana na uchafu wa baadhi ya wasanii hasa wasagaji na wanaojiuza.
“Yaani naona aibu sana kujitambulisha kwenye ofi si za watu kwani kila ninakoenda na kujitambulisha watu wanaanza kunong’ona huku wakidai kwamba wasanii wa kike wa fi lamu wana tabia chafu wakati tunachafuliwana watu wachache tu wasiojiheshimu,” alisema Nora.
Share:

Thursday, 8 May 2014

RAIS KIKWETE ATEUA KAMISHNA MPYA TRA


Rais Jakaya Kikwete amemteua Rished Bade kuwa Kamishna mpya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Harry Kitilya aliyestaafu kazi akiwa katika nafasi hiyo, mwaka jana, Ikulu imesema leo
Share:

MWANAFUNZI AMUA KUWEKA PICHA YAKE MTANDAONI AKIWA UCHI

Huyu ndio dent ambaye ameamua kuweka wazi sehemu zake nyeti ....
Shariti lazima uwe mtu mzima umri kuanzia +18,ndipo uangalie hii picha,TUANGAZE BONGO atupo hapa kumzalilisha mtu ila tupo kwa ajili ya kukomesha vitendo vichafu vya kujiuza kupitia mitandao ya kijamii
Share:

MAHABUSU WA GEREZA KUU LA MKOA WA ARUSHA WAVUA NGUO KUPINGA WENZAO KUACHIWA...SOMA HABARI KAMILI HAPA


 
Mahabusu wa Gereza Kuu la Mkoa wa Arusha, jana walizua tafrani katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini hapa, baada ya kuvua nguo na kugoma kushuka kwenye basi wakipinga kitendo cha watuhumiwa wawili wa dawa za kulevya kuachiwa kinyemela.  
 
Watuhumiwa wanaolalamikiwa ambao mashtaka yao yalibadilishwa mara mbili ili wapewe dhamana ni Dharam Patel (26) na Nivan Patel (20) wanaodaiwa kukamatwa na kete 173 za heroini na misokoto 300 ya bangi, Aprili mwaka huu.
 
Mahabusu hao walikuwa wakipaza sauti kupinga madaraja kati ya wenye nacho na wasio nacho kwa wengine kuachiwa na wengine kubaki ndani kwa kisingizo cha ‘upelelezi haujakamilika’.
 
Huku wakipaza sauti zao kwa nguvu, mahabusu hao wa kesi za mihadarati ikiwamo mirungi na bangi, wizi wa kutumia silaha na mauaji, walisema wamekaa mahabusu kwa zaidi ya miaka miwili, lakini hawajawahi hata kusomewa maelezo ya awali na kuendelea kuteseka gerezani.
 
Sauti ilisikika kutoka ndani ya basi: “Wenzetu hata mwezi haujaisha wanafutiwa kesi, jamani sisi tumekosa nini? Tunataka haki itendeke kwa wote.”
 
Mahabusu hao walionekana wakiwa wamesimama ndani ya basi hilo bila nguo, huku umati wa watu waliofika mahakamani hapo ukitazama.
 
Baada ya kuona umati wa watu unazidi kuongezeka kuwashangaa mahabusu hao, askari wa magereza waliondoa basi hilo eneo la Mahakama.
 
Kuachiwa watuhumiwa
Taarifa za kuachiwa kwa watuhumiwa hao wa dawa za kulevya waliokuwa na kesi mbele ya Hakimu Mkazi Arusha, Mwakuga Gwanta zilidaiwa kuwa zilitokana na Ofisi ya DPP Arusha, kubadilisha hati ya mashtaka.
 
Ilidaiwa kuwa badala ya kudaiwa kuwa walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya, iliandikwa kuwa walikutwa na dawa hizo mashtaka ambayo yana dhamana.
 
Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa alisema jana kuwa ofisi yake haina taarifa za watuhumiwa hao kupewa dhamana lakini alisema kulikuwa na jaribio hilo.
 

“Ninachojua kesi hii ilipangwa kutajwa Aprili 29, mwaka huu, lakini ikasogezwa mbele hadi Mei 2 na kilichofanyika hati ya mashtaka ilibadilishwa na kuandikwa wamepatikana na dawa za kulevya."

Alisema kwa mujibu wa sheria, mtu ambaye anakamatwa na dawa za kulevya zenye thamani chini ya Sh10 milioni anaweza kupewa dhamana, lakini kiwango kikiwa zaidi ya hapo, hapati dhamana.
 
“Baada ya kubainika kuna njama za mashtaka kubadilishwa, tulipinga kwa kuwa kosa lipo wazi kwamba walikuwa wakisafirisha dawa hizo, sidhani kama wamepewa dhamana... sidhani kama inawezekana ila tunafuatilia kwa karibu tukio hili,” alisema Nzowa.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema kazi ya polisi ilikuwa ni kukamata watuhumiwa na kuwafikisha mahakamani tu.
 
Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Wilibard Mashauri alisema hahusiki katika malalamiko hayo kwa kuwa si mpelelezi wa kesi.
 
“Lakini hawa mahabusu wanalalamikia kuachiwa kwa wale watuhumiwa wenye kesi ya dawa za kulevya, kesi ambayo haipo kwangu wala sijui wameachiwa kwa kifungu gani na inategemea na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DP) amewaachia kwa kifungu gani,” alisema.
Share:

NI ZAIDI YA UNYAMA!!..AZALIA KWENYE NDOO, APIGWA PINGU!


MWANAMKE aliyejulikana kwa jina la Hadija Mohammed, mkazi wa Mchikichini, Ilala jijini Dar es Salaam amekumbana na mkono wa sheria baada ya kufanya kitendo cha kinyama kufuatia kujifungulia kwenye ndoo kisha kichanga kukitupa chooni.
Hadija Mohammed, anayetuhumia kukitupa kichanga baada ya kuzaliwa.
Kwa mujibu wa chanzo, mwanamke huyo alikuwa na ujauzito uliotimiza miezi tisa na kila mtu alikuwa akiuona, lakini ghafla siku ya tukio baadhi ya ndugu waligundua kuwa hakuwa na ujauzito tena!
NDUGU WAMBANA
Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kuwa baadhi ya ndugu na majirani walipomuona bila ujauzito walimbana kwa kumuuliza iliko mimba hiyo.
Hadija Mohammed akiwa chini ya ulinzi.
“Ndugu zake na majirani walipomuona hana tumbo kama mwanzo walishangaa, wakaamua kumbana tena kwa vitisho kwamba watampeleka polisi.
“Ndipo alipoamua kueleza ukweli kwamba, alijifungulia kwenye ndoo lakini mtoto alikwenda kumtupa chooni,” kilisema chanzo hicho.
POLISI WAAMBIWA, WAKOMAA NAYE
Habari zilizidi kudai kuwa baada ya majirani na ndugu kuambiwa hivyo walikwenda kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Pangani kilichopo Ilala, Dar ambapo walifika na kukiokoa kichanga hicho lakini walikuta kimeshakata roho.
MAMA APELEKWA POLISI
Mpashaji wetu alizidi kudai kuwa, baada ya polisi kuuchukua mwili wa mtoto huyo hawakumwacha mama mtu aendelee kuponda maisha uraiani, walimbeba mpaka kituoni hapo na kumfungulia jalada lenye namba ILA/RB/1715/2014 kisha kumpeleka  kwenye Mahabusu ya Polisi Msimbazi huku mwili wa mtoto huyo ukipelekwa Hospitali  ya Amana na baadaye Hospitali ya Taifa Muhimbili.
NI FUNDISHO
Afande mmoja ambaye aliomba jina lake lisiandikwe, alisema ni lazima Hadija apambane na mkono wa sheria ili iwe fundisho kwa wanawake wengine wenye mchezo huo.
“Hii tabia imekua sana. Wanawake wengi wanajifungua kisha wanawatupa watoto chooni au kokote kusikojulikana ili wao waendelee kula raha mjini. Huyu lazima sheria ishike makali yake ili iwe fundisho,” alisema afande huyo. 
Share:

MWANAJESHI APEWA KICHAPO KIKALI NA ASKARI WA USALAMA!



Askari wa Usalama barabarani eneo la Makumbusho, Dar wakimpiga Dereva wa gari ambaye amejitambulisha kama mwanajeshi! Tukio hili limetokea mida ya saa 9 mchana huu. Bado haieleweki chanzo ni nini.

Je, unadhani hivi ndivyo askari wetu wanatakiwa kutekeleza majukumu yao?
Share:

SNURA MAMA WA MAJANGA AINGILIA KATI BIFU LA WEMA, KAJALA

MSANII wa filamu na muziki, Snura Mushi ameingilia kati ugomvi wa wasanii wenzake, Wema Sepetu na Kajala Masanja na kuwaagiza wamalize tofauti zao.
Msanii wa filamu na muziki, Snura Mushi a.k.a mama majanga.
Wasanii hao ambao wameingia kwenye bifu la kufa mtu kufikia hatua ya kuanikana kwenye vyombo vya habari huku chanzo kikubwa kikitajwa ni shilingi milioni 13 ambazo Wema alimlipia Kajala kama faini ya kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa rehani kisheria iliyokuwa ikimkabili mahakamani.
Nyumba hiyo iliwekwa rehani kutokana na mume wa Kajala, Faraja Agustino kushitakiwa kwa kosa la kutakatisha fedha haramu.
Wema na Kajala.
Snura amewataka Wema na Kajala kutoangalia nani ana makosa, wamalize tofauti zao.
“Nawashauri wenzangu wasigombane na kuwekeana vinyongo hiyo ni kama wanawapa watu faida,
nawaomba wamalize kwani haipendezi kabisa kwa jinsi walivyokuwa wameshibana. Kama mmoja anaona amemkosea mwenzake ajishushe na kuomba msamaha,” alisema Snura.
Share:

WANAFUNIKA NYWELE LAKINI WANAFUNUA MATITI!


Afrika kama tunavyoifahamu, ilikuwa ni sehemu ya Mila na Tamaduni bora kabisa, sehemu ambayo heshima adabu vilikuwa ni msingi wa jamii yake, hasa kwenye jamii.

Ni sehemu ambayo masikini waliishi kwa mlo mmoja lakini bado waliheshimiana, kuvumiliana na kupendana. Ni sehemu ambayo binti angekutwa akifanya mambo ya aibu basi wazazi wake wangenyooshewa vidole kwa malezi mabaya kwa binti yao. Vivyo hivyo kwa vijana wa kiume. Mambo haya yalipatikana zaidi kwenye nchi nyingi za kiafrika na Tanzania ni mojawapo.

Ila kwa sasa, Waafrika wengi, hasa vijana wamezua mijadala mingi inayotokana na mienendo ya tabia zao zinazopelekea kuvunjika kwa Mila na Tamaduni bara hili…. Kitu kinachozua maswali juu ya nani wakulaumiwa kwa kuvunjika na kuharibika kwa Mila na Tamaduni za Afrika…? Mfano mdogo uko kwenye hiyo picha hapo juu, huyu binti anafunika nywele kwa imani lakini anafunua matiti. Dini, shule, wazazi, walezi na walimu wameshindwa kukisaidia hiki kizazi. Ni nani wa kulaumiwa? Kwangu mimi hiki bado ni kichekesho tu!
Share:

KOLETA AWALIPUA WAKE ZA WATU BONGO MOVIES


STAA wa filamu Bongo, Coletha Raymond ‘Koleta’ amewashukia waigizaji wenzake ambao ni wake za watu na kudai kuwa wanaichafua sanaa hiyo kwa kujirahisisha kwenye ngono na wanaume wengine.
Staa wa filamu Bongo, Coletha Raymond ‘Koleta’.
Akizungumza kwa sharti la kutowataja majina, Koleta alisema anawatambua wasanii wengi ambao ni wake za watu na hufanya mchezo huo wakiwa eneo la kutengenezea muvi (lokesheni).
“Wananikera, wamezidi kujirahisisha na kufanya uchafu. Kuna baadhi ya wake za watu hawajitambui wakiwa lokesheni nakuishia kufanya umalaya,” alisema.
Share:

BABY MADAHA AUMBUKA


STAA wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ambaye aliwahi kutangaza kuacha fani ya maigizo na muziki amejikuta akiumbuka kwa mashabiki wake kutokana na kuendelea kukomaa katika gemu kwa kuachia kazi mpya na kuandaa matamasha mbali mbali.
Staa wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha akiwa kwenye pozi.
Msanii huyo alitoa uamuzi huo kwa madai kuwa alichoshwa na skendo za kila kukicha ambazo wakati mwingine zimekuwa zikimshushia hadhi katika jamii, ikiwemo skendo ya kunaswa kwenye mtego wa kujiuza ilioandliwa na Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Baby Madaha alisema hawezi kupinga kama alizungumza hayo isipokuwa tangu atoe kauli hiyo amejikuta akizidi kupata mafanikio makubwa katika muziki.
“Naweza kusema nimeumbuka kwa kile nilichoongea, maana nimejikuta nashindwa kutekeleza nilichowaambia mashabiki wangu sababu dili zinakuja, siwezi kuziacha,” alisema Baby.
Share:

JOKATE AANIKA SIFA ZA MUME MTARAJIWA


MTOTO mzuri kunako anga la watangazaji Bongo, Jokate Mwegelo ameibuka na kuanika sifa za mwanaume ambaye anafaa kuwa mume wake.
Mtoto mzuri kunako anga la watangazaji Bongo, Jokate Mwegelo.
Akipia stori na paparazi wetu juzi jijini Dar, Jokate alisema anapenda mwanaume ambaye atajua kutafuta fedha kwa nguvu zote, awe anajua kubembeleza na awe na nidhamu kwa wazazi wake.
“Sifa ya mume ninayemtaka, anapaswa kuwa mtafutaji wa fedha, sipendi mwanaume asiyependa kutafuta, awe anajituma kwa kazi zake na kwa mpenzi au familia yake na pia ajue kunibembeleza,’’ alisema Jokate.
Share:

DIAMOND KATIKA POZI

Mshindi wa tuzo saba za KTMA Nasibu Abdul ‘Diamond’ katika pozi.
Share:

Lulu Aomba Basata Waruhusu Kufanya Movie Nusu Utupu Waendane na Soko la Kimataifa

 DIVA wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameziomba mamlaka zinazosimamia maadili ya filamu nchini ziwaruhusu wasanii waigize nusu utupu ili kuendana na soko la kimataifa.

Akitetea hoja yake mbele ya paparazi wetu, staa huyo aliyeitendea haki filamu ya Foolish Age alitolea mfano Tamthiliya ya Shuga iliyomtoa Lupita Nyong’o ambayo alicheza akiwa nusu utupu.

“Wanasema hatufuati maadili wakati kuna muvi ambazo zipo theatre na watu wanaangalia hazina maadili, wao wanataka tufanye vitu kwa kudanganya wakati sasa hivi tuko dunia ambayo tuna takiwa tuweke vitu wazi, wasibane sana,” alisema Lulu.


Share:

OLE MEDEYE AMCHANA LEMA, ADAI AMEKULIA GHETO


Mbunge wa Arumeru Magharibi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ole Joseph Medeye.
MBUNGE wa Arumeru Magharibi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ole Joseph Medeye, amemchana Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema hivi punde bungeni kuwa amekulia gheto na kupata huruma ya wanannchi wa Arusha waliomchagua kuwa mbunge. 
Medeye ameongea hayo wakati wa Majadiliano ya Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Tamisemi.
Medeye ameahidi kugombea Jimbo la Arusha Mjini Uchaguzi Mkuu ujao wa 2015 ili achukue nafasi ya Lema!
Share:

Wednesday, 7 May 2014

MAGAZETI YA JUMATANO

Share:

Uchaguzi Serikali za Mitaa watengewa Sh5 bilioni


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana aliwasilisha bungeni, bajeti ya ofisi yake na mfuko wa Bunge inayofikia Sh5.21 trilioni. Kati ya hizo, Sh5 bilioni zimetengwa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Hayo yalielezwa bungeni jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia wakati wa maelezo kuhusu kazi zilizotekelezwa mwaka 2013/2014 na mwelekeo wa kazi zitakazotekelezwa 2014/2015.
Ghasia alisema shughuli zitakazogharimiwa na fedha hizo ni pamoja na maandalizi ya masanduku ya kupigia kura, kupitia kanuni za uchaguzi na kuandaa fomu na nyaraka mbalimbali za uchaguzi.
Shughuli nyingine ni uhakiki wa majimbo ya uchaguzi huo ambayo ni vijiji, mitaa na vitongoji.
Malipo ya wabunge
Katika bajeti hiyo ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sh132.6 bilioni zimetengwa kwa ajili ya Mfuko wa Bunge la Muungano, kati yake posho na mishahara kwa ajili ya Bunge (wabunge na watumishi wa Bunge) ikiwa ni Sh123.94 bilioni.(P.T)
Kwa mujibu wa nyaraka za bajeti hiyo, wabunge peke yao wametengewa Sh102.317 bilioni kwa ajili ya mishahara, posho za vikao na kujikimu na posho za safari ndani na nje ya nchi.
Kwa mwaka wa fedha unaomalizika Juni 30 mwaka huu, mishahara na posho za wabunge zilitengwa Sh93.37 bilioni, kati ya hizo posho zilikuwa Sh48.74 bilioni ikilinganishwa na Sh49.526 bilioni zilizotengwa katika bajeti 2014/2015, sawa na ongezeko la Sh800 milioni.
Usimamizi wa rasilimali watu na utawala ambayo ndiyo inayohusika na mishahara na posho kwa watumishi wa Bunge kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015, umetengewa Sh21.6 bilioni.
Takwimu hizo zinaonyesha kuwa mishahara ya wabunge imetengewa Sh12.769 bilioni.
Safari za ndani
Posho za safari ndani ya nchi zimetengewa Sh11.192 bilioni wakati zile za safari za nje kwa wabunge zimetengewa Sh9.08 bilioni.
Posho hizo ambazo hazikatwi kodi ni karibu mara nne ya kiwango kilichotengwa kwa ajili ya mishahara yao ambayo ndiyo pekee hukatwa kodi.
Fedha za Maendeleo
Kati ya Sh8.7 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo, Sh2.9 bilioni ni kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya Ofisi za Bunge, Sh5.9 bilioni ni kwa ajili ya programu ya kujenga miundombinu ya Bunge na programu ya kuimarisha Bunge imetengewa Sh755 milioni.
Chanzo:Mwananchi
Share:

MBOWE kutangaza Baraza Kivuli kesho


Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kesho atatangaza Baraza Kivuli la Mawaziri.
Kwa mara ya kwanza tangu Uchaguzi Mkuu uliopita wa 2010 na baadaye kuzinduliwa kwa Bunge la 10, baraza hilo litawajumuisha wabunge kutoka vyama vingine nje ya Chadema. Vyama vitakavyojumuishwa ni CUF na NCCR – Mageuzi.
"Nitalitangaza baraza langu jipya la mawaziri Alhamisi (kesho) baada tu ya kukamilisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu," alisema Mbowe jana mjini Dodoma.
Alisema mawaziri hao wataanza kutekeleza majukumu yao katika Bajeti ya mwaka 2014/2015 kwa kusoma hotuba zao za bajeti.
Kujumuishwa kwa wabunge wa vyama vya CUF na Chadema ni matunda ya kuundwa kwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakati wa Bunge la Katiba.
Hivi karibuni, Mbowe alikaririwa na gazeti hili akisema hatua hiyo imefikiwa baada ya "kila upande kukubali kuwa unamhitaji mwenzake katika harakati za kuikomboa nchi hii."
Ukawa ndiyo iliyowaongoza baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu kutoka nje kususia mchakato wa Katiba Mpya kutokana na kile ilichodai kuwa ni kutokuridhishwa na jinsi mambo yanavyokwenda.
Wakati huohuo; wabunge wamekubaliana kuwa shughuli za Bunge zitakuwa zikianza saa 3:00 asubuhi na kusitishwa saa 7:00 mchana na kurejea tena saa 10:00 alasiri hadi saa 2:00 usiku.
Ratiba hiyo itahusisha pia Ijumaa na Jumamosi.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah alisema utaratibu huo utaongeza nafasi za wabunge kuchangia katika Bunge la Bajeti.
Imeandikwa na Sharon Sauwa, Daniel Mjema na Edwin Mjwahuzi
Chanzo: Mwananchi
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger