ACT-TANZANIA
Mwenyekiti akikabidhiwa cheti.
kilifanikiwa kumaliza zoezi la uhakiki mara baada ya kuruka vihunzi vingi toka kwa wahafidhina na watu wasiopenda siasa za ushindani. Katika zoezi letu tumekumbana na vikwazo vingi ikiwa pamoja na uchomekaji wa wanachama fake waliotumwa kwaajili ya kazi ya kujifanya wako tayari kuhakikiwa lakini kwa lengo la kutojitokeza siku ya kuhakikiwa, jambo ambalo wahafidhina na maadui zetu walikuwa hawajui ni kuwa chama chetu kinapendwa na wananchi hivyo wengi walijitokeza kiasi cha kuziba mapengo ya mamluki ambao kwa makusudi hawajajitokeza siku ya kuhakikiwa. Pamoja na hayo tunatambua wanachama wetu waaminifu waliotaka kujitokeza lakini sababu zilizo nje ya uwezo wao zilipelekea washindwe kujitokeza siku ya kuhakikiwa.
Karibu ACT-TANZANIA, wewe ndio mbadala wa CHADEMA na CCM.
Mungu ibariki Tanzania.
Wednesday, 7 May 2014
LINAH SANGA:'NAFUNGA NDOA MDA SI MREFU'
MSANII mwenye sauti mwanana anayetesa kwenye Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’, amefunguka kuwa, ndoa yake na mpenzi wake Nagari Kombo ‘Kaka wa Bongo’ inanukia.
Linah alisema hayo wikiendi iliyopita
aliponaswa akijiachia na Kaka wa Bongo katika Ukumbi wa Mlimani City,
Dar ambapo mpango mzima wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards
2013 – 2014 ulikuwa ukifanyika.
“Sina haja ya kuendelea kumficha mpenzi
wangu, kwani kwa sasa anatambulika kwa kila mtu na hasa ndugu zangu wa
karibu, kitu cha kusubiriwa kwa sasa ni tarehe ya ndoa yetu tu,” alisema
Linah.
Kaka wa Bongo alijizolea umaarufu siku
za nyuma baada ya kuingia uwanjani na kumkumbatia mchezaji, Ricardo Kaka
wa Timu ya Taifa ya Brazil iliyokuwa ikichuana na Taifa Stars katika
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Tuesday, 6 May 2014
ACT-Tanzania yapata usajili wa kudumu!
Chama kilichovunja rekodi kwa kupata usajili wa kudumu miezi michache mara baada ya usajili wa muda; ACT-TANZANIA leo ndio kimekabidhiwa cheti chake cha usajili wa kudumu rasmi na masajili wa vyama vya siasa mara baada ya kumalizika zoezi la usajili lililofanyika katika mikoa kumi iliyoteuliwa.
PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO,RIDHIWANI KIKWETE NA GODFREY MGIMWA WAAPISHWA
Spika
wa Bunge,Mh. Anne Makinda na watendaji wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania. Wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya shughuli za Bunge kuanza
leo mei 6, 2014.
Mbunge Mpya wa Jimbo la Kalenga,Mh. Godfrey Mgimwa akisindikizwa na wabunge wa CCM kuingia Bungeni mjini Dodoma leo Mei 2014.
Mbunge Mpya wa Jimbo la Kalenga,Mh. Godfrey Mgimwa akila kiapo Bungeni mjini Dodoma leo Mei 6, 2014.
Mbunge
Mpya wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akisindikizwa na
wabunge wa CCM kuingia kwenye Ukumbu wa Bunge Mjini Dodoma, leo Mei 6,
2014
Mbunge Mpya wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akila kiapo Bungeni Mjini Dodoma,leo Mei 6, 2014.
Waziri
Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akimpongeza Mbunge Mpya wa Chalinze,Ridhiwani
Kikwete baada ya kuapishwa, Bungeni Mjini Dodoma leo Mei 6, 2014.
Waziri
wa Nchi,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. William Lukuvi akimpongeza Mbunge
Mpya wa Chalinze,Ridhiwani Kikwete baada ya kuapishwa, Bungeni Mjini
Dodoma leo Mei 6, 2014.
Mke
wa Rais,Mama Salma Kikwete akiwa Bungeni Mjini Dodoma Mei 6,2014
wakati mwanae,Ridhiwani Kikwete alipoapishwa . Kulia kwake ni Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema nchimbi.
Mke
wa Rais,Mama Salma Kikwete na familia wakiwa Bungeni Mjini Dodoma leo
Mei 6,2014 wakati mwanae,Ridhiwani Kikwete alipoapishwa . Kulia kwake
ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Dr. Rehema Nchimbi.(Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
BUNGE LA BAJETI LAANZA LEO
Spika wa Bunge Anna Makinda |
Katika
mkutano wake na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Shughuli za
Bunge, John Joel, alisema muda wa kuchangia Bajeti hiyo, umepunguzwa
kutoka dakika 10 hadi saba na muda wa uwasilishaji wa bajeti za wizara
mbalimbali, pia umepunguzwa.
Alisema
kutokana na mabadiliko hayo, sasa kila wizara itapewa siku moja ya
kuwasilisha bajeti yake na kujadiliwa. “Tumepima muda tukaona unatosha,“
alisema.
Liverpool's dream is almost over & it's time for Suarez to join Real Madrid
Correspondent Column: The Merseysiders' star man has
been in sensational form this season but he should leave Anfield if he
gets the chance to the Liga giants this summer
Luis Suarez faces Crystal Palace tonight needing two more goals in Liverpool’s remaining two fixtures to break the Premier League scoring record over a 38-game season.
It would be the perfect way for the Uruguayan to finish a sensational individual campaign before moving on to bigger and better things.
Suarez has been the outstanding player in the division this season with a stunning record of 30 goals in 31 league matches, a strike rate that propelled Liverpool up the table into an unlikely title race.
The Reds can still win their first league title in 24 years if Manchester City slip up - but whatever happens, Suarez should be seriously considering a summer move to Real Madrid.
Player Ranking — English Barclays Premier League
# | Player | GP | Team | Goals |
---|---|---|---|---|
1 | Luis Suarez | 32 | Liverpool | 31 |
2 | Daniel Sturridge | 28 | Liverpool | 21 |
3 | Yaya Touré | 33 | Manchester City | 19 |
Bale joined Madrid as the best player in England having won the PFA and FWA player of the year awards.
SUAREZ AT THE DOUBLE | ||||
SUAREZ NAMED FWA PLAYER OF THE YEAR |
The 27-year-old will find he has plenty of reasons to stay at Liverpool. He signed a four-and-half-year contract in December worth £200,000 a week as a reward for his outstanding form; he has improved dramatically under the guidance of Brendan Rodgers; Liverpool are one of the most famous clubs on the planet and will be back where they belong in the Champions League next season.
But they are not Real Madrid.
Suarez claims he is "very happy" and "nothing is going to happen" in the summer, but the chance to move to the Spanish capital is one that few players are able to turn down.
Cristiano Ronaldo pushed through the move in 2009, Bale did the same in 2013. It was an opportunity, they were warned, that might not come again.
One win away from that holy grail of a 10th European title, Madrid have built a team in no small part based on targeting the best Premier League talent. Ronaldo, Bale, Luka Modric and Xabi Alonso all arrived from England.
If Suarez wants to truly be considered one of the very best on the planet, perhaps even one of the greatest of all time, he must follow the same path.
He has conquered the Premier League, now it is time for a new challenge.
At Real Madrid, alongside Bale and Ronaldo, he could have a genuine chance of one day winning the Ballon d'Or.
Mnyika: Tutaandamana kudai maji Ikulu
Mnyika alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kusema baada ya kuona hakuna majibu ya ufumbuzi wa tatizo hilo kutoka kwa viongozi husika aliamua kumuandikia barua Rais Jakaya Kikwete yakumtaka aitishe kikao cha kuzungumzia tatizo hilo, lakini hadi sasa hamna majibu yaliyotolewa.
Aidha, alisema atakwenda katika Bunge la Bajeti kupambana na Profesa Maghembe ampe majibu yanayoeleweka na kuhakikisha anachukua hatua bila hivyo ataungana na wananchi kwenda Ikulu kumtaka Rais Kikwete kuingilia kati tatizo hilo kwa sababu linawatesa sana wananchi.
Mnyika alisema katika ziara aliyofanya jimboni kwake tatizo la maji ni kubwa na baadhi ya kata hazijapata maji kwa kipindi cha miezi mitatu sasa pamoja na kwamba wananchi wamelalamika kwa mamlaka husika, lakini hakuna jitihada zozote zinazofanyika kutatua kero hiyo sugu.