Tuesday, 6 May 2014
AJARI MBAYA YASABABISHA KIFO CHA MTOTO MCHANGA
AJARI MBAYA YASABABISHA KIFO CHA MTOTO MCHANGA
TANKI LA MAFUTA LALIPUKA NA KUSABABISHA ADHA KUBWA KWA WASAFIRI SHELUI, SINGIDA
Msururu wa magari ukiwa mkubwa katika eneo hilo baada ya kushindwa kupita kutokana na moto mkubwa uliokuwa ukiwaka.
Baadhi
ya wananchi wakipiga picha wakati tanki la mafuta la kampuni ya B.
Clarke Haulege Construction, Tanki hilo ni mali ya Bw. Bundala Kapela wa
Igunga ni namba T634 BCZ lenye vyumba vinne na uwezo wa kubeba lita
40.000 za mafuta ya Petroli lililipuka majira ya Saa 11:00 katika
barabara kuu ya Dodoma Mwanza eneo la Shelui mkoani Singida wakati breki
za tanki hilo upande wa kushoto zilipojam na kusababisha moto, Jambo
lililomfanya dereva wa roli lenye namba za usajiri T 164 CGF aina ya
Scania lililokuwa likivuta tanki hilo kusimamisha na kukata haraka tanki
hilo huku akiondoa haraka injini ili kuepusha madhara zaidi ambayo
yangeweza kutokea, Katika tukio hilo lililosababisha usumbufu mkubwa kwa
abiria na msururu wa magari kushindwa kupita katika eneo hilo kutokana
na moto mkubwa uliochanganyika na moshi kutishia usalama wa watumiaji
wengine, hata hivyo baada ya moto kupungua kiasi askari wa usalama
barabarani waliamuru magari yaanze kupitia pembeni mwa barabara hiyo ili
kuendelea na safari hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa
katika tukio hilo.
Wananchi na wasafiri mbalimbali wakitoka kuangalia tukio hilo.
Askari wa usalama barabarani akihakikisha mambo yanakwenda sawana usalama unaimarishwa katika eneo hilo.
FID Q SINA BIFU LOLOTE NA WEUSI
Hii
inahusisha show iliyofanyika Maisha Club Dar May 4 2014 usiku ambayo
Adam Mchomvu ndio alikua mwenye show pamoja na kuzindua video yake mpya
ya ‘au sio’ kisha Fid Q ndio akawa MC.
Miongoni mwa watu waliokuwa wanapanda
kwenye stage kutoa burudani ni kundi la Weusi lakini ilipofika zamu yao
kupanda, MC Fid Q hakuwataja kwamba ndio wanapanda kwenye stage bali
walipanda kimyakimya.
Gossip cop Soudy Brown alizipata stori
kwamba WEUSI walikataa kuitwa kwenye stage na Fid Q, yani hawakutaka Fid
awataje kwamba ndio wanapanda.
Fid Q alipoulizwa
ilikuaje akajibu ‘Zile ni style za show tu mtu anakuja anasema sisi
tufanye kama suprise lakini sio kwamba walikua hawataki, mimi na WEUSI
tuko poa’
Soudy Brown: Mbona watu wanasema tuzo ulizoshinda ndio zimeleta matatizo?
Fid Q:
Hapana na sidhani kama zinaweza kuleta matatizo kwa sababu nina uhakika
hata WEUSI wanajua tuzo niliyopewa ninastahili labda kama wao sio
hiphop.. hatuna matatizo, hata jana baada ya kuchukua tuzo nilikua
kwenye viwanja tofautitofauti na Joh Makini.
Fid Q: Hakujawahi kuwa na tatizo isipokua mashabiki ndio waliwahi kuhisi kuna matatizo, wakati mwingine inabidi uache fans wawe fans.
Baada ya hayo maneno ya Fid Q Soudy
Brown alimpata msemaji wa WEUSI ambae ni rapper Nikki wa II aliesema
‘hakuna ukweli kwamba tumekataa kutambulishwa na Fid Q, kama umefatilia
show zetu nyingi huwa hatuna utaratibu wa kutambulishwa kwa sababu huwa
imezoeleka kila mtu akiingia anatambulishwa, ni kitu ambacho kimezoeleka
sana, hata Fiesta yenyewe huwa tunatokea tu bila kutambulishwa’
Kwa kumalizia Nikki wa II amesema labda tofauti iliyopo kati yake na Fid Q ni rasta au majina ila wako sawa na mtu yeyote.
Soudy Brown: Mlipatana lini?
Nikki wa II: ‘Kwani tuliwahi kugombana?’
MASWAYETU: MENINAH-MWANAMKE MREMBO KATIKA TASNIA YA BONGO FLA...
MENINAH-MWANAMKE MREMBO KATIKA TASNIA YA BONGO FLA...: Hakika ni Mrembo wa Haja Anayewakilisha Vyema Wanawake katika Tasnia ya Music wa Bongo Flava....Nani mwingine anakutia uzuri wake kati...........
BILIONEA HOME SHOPPING CENTRE AHAMA NCHI,NI YULE A...
TUANGAZE BONGO: BILIONEA HOME SHOPPING CENTRE AHAMA NCHI,NI YULE A...: KUNA madai mazito kwamba, yule bilionea kijana anayemiliki kampuni ya uuzaji na usambazaji wa vifaa vya nyumbani ya Home Shopping Centre ...
MGANGA WA DIAMOND AIBUKA NA MAPYA BAADA YA TUZO SABA
Yule mganga maarufu wa mastaa nchini ambae
aliwahi kutangaza kuwa amekuwa na ukaribu na
mwanamuziki Diamond ameibuka na kusema
kuwa tuzo hizo saba alizozipata zinamaana
kubwa sana kwenye kazi zake anazozifanya.
alisema" Niliongea na Diamond wiki moja kabla
ya shoo nikamueleza kuwa atapokea tuzo nyingi
sana mwaka huu na hizo tuzo ni ishara tosha ya
kudumu kwenye game kwa miaka kama hiyo ya
tuzo zake kwa maana ya miaka saba mbele yote
nyota yake itaendelea kung'ara" Alisema Dokta
Kamdege
Aidha Mganga huyo aliendelea kusema" Unajuwa
haya mambo ya maagano yapo muziki na miti
shamba zinaendana kwani kwenye dunia hii ya
leo maadui ni wengi kuliko marafiki kwani wapo
watakaokuchukia bila sababu za msingi hivyo ni
vyema ukalijua mapema hilo na kujikinga kama
ilivyo kwa Diamond" Alisema mganga huyo
mwenyeji wHa Mkoa wa Tabora
Hata hivyo mganga huyo aliendelea kuto uwito
kwa watanzania popote walipo duniani
waendelee kupata huduma zake kwani hii ni
kama baraka kwa taifa la Tanzania.
Dokta Kamdege amekuwa akitumiwa sana na
vigogo wa Serikali, wasanii na watu mbalimbali
duniani kufanikisha mambo yao kwa kuwapatia
baraka kupitia miti shamba.
Monday, 5 May 2014
Kigwangala Atafakari Urais 2015
Na John Dotto
Mbunge
wa jimbo la Nzega Mkoani Tabora kupitia CCM, Hamis Kigwangala,
ametanabaisha kuwa anatafakari kama anaweza kugombea Urais kwenye
uchaguzi mkuu ujao kupitia chama cha mapinduzi CCM.
Akijibu
maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua fununu zilizo enea kwenye
baadhi ya mitandao ya kijamii ambayo imekuwa ikiibua mijadala mara kwa
mara inayomshawishi kugombea Urais mwaka 2015, Dk. Kigwangala amesema
anatafakari jambo hilo zito na kuongeza kuwa muda utakapofika
atayazingatia maoni ya wananchi.
Akizungumzia
maelezo kwamba haoni kama ni hatari kwake kutangazwa mapema kwamba
anataka kuwa kugombea Urais ni kujipunguzia sifa katika chama chake, Dk.
Kigwangala alisema yeye hajatangaza kama anataka Urais na wala
hajamtuma mtu kuanza kumfanyia kampeni, kwani watanzania wanaongozwa na
katiba yenye Uhuru wa kujieleza na kutoa maoni, hivyo hayo ni mawazo yao
na wana haki ya kufanya hivyo na yeye binafsi hawezi kuwapinga.
Hivi
karibuni kumeibuka mijadala mizito kwenye mitandao ya kijamii na baadhi
ya wanaharakati kutengeneza vuguvugu la kumshawishi Dk. Kigwangala
kuchukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
ifikapo mwaka 2015.
Mijadala
hiyo mizito imeanzishwa katika mitandao ya Internet na simu za mkononi
walio ipachika jina "Citizens for Kigwangala" ambapo katika mijadala
hiyo wamekuwa wakishawishiana na kumwagia sifa Dk Kigwangala kwamba
ndiye kiongozi pekee anayefaa kuwakilisha chama cha Mapinduzi katika
uchaguzi mkuu ujao.
Baadhi ya
vijana wamekuwa wakijadili kuwa Dk Kigwangala ndiye anayeweza kuleta
upinzani wa kweli kwa vyama vya upinzani, wakijenga hoja kuwa amekuwa na
misimamo na uwezo wa kujieleza kwa ufasaha ndani ya vikao vya bunge.
Dk
Kigwangala ni mbunge wa jimbo la Nzega mkoani Tabora, mwenye taaluma ya
udaktari wa tiba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge
ya tawala za mikoa na serikali za mitaa.
MVUA YAMUWEKA KINANA DAKIKA 20 ANGANI
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kutoka kwenye ndege ya
kampuni ya Flightlink kwenye uwanja wa Ndege wa Zanzibar baada ya kukaa
angani kwa dakika 20 zaidi ya muda uliopangwa kutokana na hali ya hewa
kuwa mbaya na mvua kubwa kunyesha.Katibu Mkuu amewasili Zanzibar kwa
ajili ya mkutano wa hadhara utakaofanika kwenye viwanja vya mikutano vya
Kibanda Maiti.
Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye akishuka kutoka kwenye ndege ya
kampuni ya Flightlink kwenye uwanja wa Ndege wa Zanzibar baada ya kukaa
angani kwa dakika 20 zaidi ya muda uliopangwa kutokana na hali ya hewa
kuwa mbaya na mvua kubwa kunyesha. Katibu Wa NEC ameongozana na Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mvua kubwa ikinyesha Zanzibar ambapo CCM inatazamiwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara.