Saturday, 7 August 2021

CNN YAWAFUKUZA KAZI WAFANYAKAZI WAKE WALIOKWENDA OFISINI BILA KUPEWA CHANJO YA CORONA

...

Shirika la habari nchini Marekani CNN limewafuta kazi wafanyakazi watatu kwa kwenda ofisini bila kupewa chanjo dhidi ya Covid - 19 vyombo vya habari vya Marekani vinasema.

Ni moja wapo ya mifano ya kwanza ya wafanyikazi wa kampuni ya Marekani kuwafuta kazi wafanyikazi wake kwa kukiuka mwongozo wa chanjo wa kampuni.

Ni halali nchini Marekani kwa makampuni kutaka wafanyikazi wapewe chanjo.

Kampuni nyingi kubwa - pamoja na Facebook na Google - zinasema zitahitaji wafanyikazi kupewa chanjo wakati ofisi zitafunguliwa kikamilifu katika miezi ijayo.

Mkuu wa CNN Jeff Zucker alitaja kufutwa kazi katika katika arifa ya ndani ya kampuni iliyotumwa Alhamisi na kutazamwa na vyombo kadhaa vya habari vya Marekani .

Chanjo ni lazima kwa mtu yeyote anayeripoti nje , anayefanya kazi na wafanyakazi wengine wowote au akiingia ofisini, ananukuliwa akisema katika arifa hiyo.

"Wacha niwe wazi - tuna sera ya kutolegeza kamba kuhusu suala hili," Bwana Zucker, mwenyekiti wa habari na michezo kwa WarnerMedia, amenukuliwa akisema.

Mnamo Mei serikali ya Marekani ilisema ilikuwa halali kwa waajiri kuhitaji wafanyikazi wanaokwenda ofisini wapewe chanjo dhidi ya Covid-19.

Mashirika makubwa ya ndege Delta na Shirika la ndege la United yanahitaji wafanyikazi wapya kuonyesha uthibitisho wa chanjo, wakati benki ya uwekezaji Goldman Sachs inataka wafanyikazi wake wafichua hali yao ya chanjo, ingawa haiitaji wafanyikazi kupewa chanjo, AP inaripoti.

Rais Biden ameamuru wafanyikazi milioni mbili wa serikali kuu kuonyesha uthibitisho wa chanjo au wafanyiwe vipimo vya lazima na kuvaa barakoa.

CHANZO - BBC SWAHILI
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger