Sunday, 1 August 2021

BOSI WA CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA KOLANDOTO AELEZA KUFAIDI MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA

...
Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kinachomilikiwa na Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga, Dkt. Paschal Shiluka amesema Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yamekuwa na manufaa makubwa kwani zaidi ya watu 450 wametembelea banda lao  na kujionea kuonesha shughuli wanazofanya kwenye chuo chao, kupata elimu ya afya ,kupima afya ikiwemo upimaji wa Sukari, Shinikizo la damu na malaria.

Dkt. Shiluka amesema Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yaliyoanza Julai 23,2021 na kufungwa leo Agosti 1, 2021 na Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga yamewasaidia pia kutangaza chuo chao. 

"Banda letu limekuwa Busy muda wote, wananchi wamejitokeza kupima afya zao,mpaka tunafunga walikuwa bado wanahitaji kupata huduma ya kupima shinikizo la damu, malaria, urefu na uzito na wote waliojitokeza kupima afya zao tumewapa ushauri na kuwashauri hatua za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuwapa Rufaa kwenda kutibiwa wale waliobainika kuwa na magonjwa tuliyokuwa tunapima",amesema Dkt. Shiluka

"Kupitia maonesho haya tumejitangaza na kutangaza huduma tunazozitoa. Zaidi ya watu 450 wametembelea banda letu na kusaini kitabu chetu. Pia zaidi ya watu 150 wamechukua fomu za kujiunga na mafunzo ya Sayansi za Afya katika kada za Nursing, Maabara, Utabibu, Famasia na Mafunzo ya Maabara Viwandani yanayotarajia kuanza Mwezi Septemba 2021. Milango ya maombi bado iko wazi naomba wananchi watumie Mwezi huu Agosti kutuma maombi yao kwa kufika chuoni au kupitia website yetu ya https://kchs.ac.tz",amesema Dkt. Shiluka.

Soma pia

WANANCHI WAMIMINIKA BANDA LA CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA KOLANDOTO KUPIMA AFYA MAONESHO SHINYANGA

Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto , Dkt. Paschal Shiluka akizungumza baada ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga kufungwa leo Jumapili Agosti 1,2021 na Waziri wa Madini Doto Biteko
Wanafunzi na Wafanyakazi wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto , Dkt. Paschal Shiluka wakipiga picha ya kumbukumbu nje ya banda lao baada ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga kufungwa leo Jumapili Agosti 1,2021 na Waziri wa Madini Doto Biteko
Wanafunzi na Wafanyakazi wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto , Dkt. Paschal Shiluka wakipiga picha ya kumbukumbu nje ya banda lao baada ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga kufungwa leo Jumapili Agosti 1,2021 na Waziri wa Madini Doto Biteko.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger