Sunday, 11 April 2021

TMA YATOA ANGALIZO LA MVUA KUBWA SIKU TATU MFULULIZO MIKOA 12 KUANZIA APRILI 12

...

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Aprili 11,2021, imetoa angalizo la uwepo wa mvua kubwa kwa siku tatu mfululizo kuanzia kesho Aprili 12 hadi Aprili 14  mwaka huu katika mikoa 15.

Katika taarifa iliyotolewa na TMA imeonyesha mvua hiyo yenye uwezekano wa wastani, itanyesha kesho Aprili 12, kwenye baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani inayojumuisha Visiwa vya Pwani,  Tanga, Lindi na Mtwara.

Pia mvua hiyo inatarajiwa kunyesh kesho kutwa, Aprili 13, katika mikoa hiyo n mikoa mingine kiwemo pia Iringa, Njombe, Ruvuma, Morogoro.


Aidha mvua hiyo inatarajiwa kunyesha Aprili 14  kwenye baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, shinyanga, Kigoma, Katavi, Rukwa, Njombe, Ruvuma pamoja na kusini mwa mkoa wa Morogoro

"Athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji jambo linaloweza kuathiri shughuli za kiuchumi na ucheleweshwaji wa usafiri. Hata hivyo, TMA imewataka wananchi kuzingatia angalizo hilo,.

Taarifa hiyo inayoelezea hali ya hewa kwa siku nne kuanzia Aprili 12 imeonesha kuwepo kwa hali ya kawaida ya hewa kwa siku ya Aprili 15, 2021
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger