Saturday, 10 April 2021

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE KWA MALKIA ELIZABETH II KUFUATIA KIFO CHA PRINCE PHILIP

...


Prince Philip

Rais wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu ametuma salamu za rambirambi na pole kufuatia kifo ch Mume wa Malkia Elizabeth wa Uingereza, Prince Philip, (Duke of Edinburgh) ambaye amefariki dunia asubuhi ya leo akiwa katika Jumba la kifalme (Windsor Castle) na umri wa miaka 99.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anasema ni "kwa huzuni kubwa" kupokea habari za kifo cha Mwanamfalme Philip kutoka Kasri la Buckingham.

Akitoa salamu zake za rambirambi alisema Mwanamfalme Philip alipata mapenzi ya vizazi nchini Uingereza, katika Jumuiya ya Madola na ulimwenguni kote

"Alikuwa mshirika wa kifalme aliyehudumu kwa muda mrefu katika historia, mmoja wa watu wa mwisho nchi hii kuwahi kutumika katika Vita vya pili vya na alitajwa katika barua za ushujaa."


Malkia Elizabeth wa Uingereza akiwa na mume wake Prince Philip enzi za uhai wake

Katika rambirambi zake, Boris Johnson alisema, "alisaidia kuongoza familia ya kifalme na ufalme ili iweze kuwa taasisi muhimu bila shaka kwa usawa na furaha ya maisha yetu ya kitaifa."

Boris Johnson anamaliza rambi rambi zake kwa kusema kwamba Familia ya Kifalme wamepoteza "sio tu mtu anayependwa sana na anayeheshimiwa sana na umma, lakini mume aliyejitolea, baba mwenye fahari na mwenye upendo, babu, na katika miaka ya hivi karibuni, babu-mkubwa".

Waziri mkuu anamnukuu Malkia wakati mmoja akisema nchi hiyo inadaiwa na mumewe deni kubwa kuliko "tunavyopaswa kujua", na kuongeza kuwa alikuwa na hakika kuwa makadirio hayo yalikuwa sahihi.

'Tunaomboleza leo na Malkia, tunampa pole zetu, na familia yake yote na tunashukuru, kama taifa, na ufalme, kwa maisha ya kipekee na kazi ya Mwamfalme Philip, Mtawala wa Edinburgh," alisema.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger