Friday, 9 April 2021

NIKE YAAGIZA 'VIATU VYA SHETANI' VYENYE TONE LA DAMU VIONDOLEWE DUKANI

...




Nike imesema kampuni iliyotengeza "Viatu vya Shetani" ambavyo vinadaiwa kuwa na tone la damu kwenye soli zake imekubali kuondoa dukani viatu hivyo kama sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa katika makubaliano ya kisheria.

Viatu hivyo vinavyouzwa kwa dola 1,018 za Marekani sawa na(pain 740) ni vina mundo wa Nike Air Max 97 zilizofanyiwa marekebisho. Ni viatu 666 pekee vilvyotengenezwa lakini vyote vilikuwa vimesafirishwa isipokuwa kimoja.

Kwa jumla MSCHF itawarudishia wateja pesa zao ili kuondoa vita hivyo madukani, Nike ilisema.

Makubaliano hayo yanasuluhisha kesi ya ukiukaji wa nembo ya biashara iliyowasilishwa na Nike.

Viatu hivyo vyenye utata vilitengenezwa na kampuni ya Brooklyn kwa ushirikiano na mwanamuziki Lil Nas X, ambaye alishikilia viatu vya mwisho ili achagua atakayempatia. MSCHF ilisema itasalia na viatu vya mwisho.

Maelezo zaidi kuhusiana na maelewano hayo ambayo pia yanahusisha viatu vya Yesu vilivyotengenezwa na MSCHF mwaka 2019 kwa kutumia soli ya Air Max 97 hayakutolewa.

"MSCHF ilifanyia marekebisho vita hivi bila idhini ya Nike. Nike haikuhusika kwa njia yoyote na Viatu vya Shetani au Viatu vya Yesu," Nike ilisema katika taarifa yake.

Viatu vya kipekee vinauzwa kwa bei ghali miongoni mwa wateja kwa hivyo haijabainika ni vingapi - ikiwa vipo - wateja watarudisha bidhaa hizo.

Wiki iliyopita Nike iliishtaki MSCHF ikidai kuwa "Viatu vya Shetani [huenda] vikaleta mkanganyiko kati ya bidhaa zake na zile za MSCHF kutokana na kuingiliwa kwa chapa au alama ya biashara ya kampuni.

Lakini MSCHF imesema viatu hivyo vina "muundo wa kipekee" na haikuona mkanganyiko wowote.

Akikubaliana na Nike, Jaji alitoa zuio la muda Alhamisi iliyopita.
Viatu vya rangi nyeusi na nyekundu "vilivyotolewa" na kampuni ya MSCHF Jumatatu, kulikwenda sambamba na uzinduzi wa nyimbo mpya ya mwanamuzi Lil Nas X ya Montero ya (Call Me By Your Name), ambayo ilitolewa kwa mara ya kwanza kwenye mtandao wa YouTube siku chache zilizopita.

Katika video ya muziki huo, mwanamuziki huyo wa rapa anateleza kwenye mlingoti kutoka peponi au mbinguni hadi jehanamu au motoni, akiwa amevaa viatu hivyo.

Taswira na hiyo na viatu ambavyo vimeandikwa andiko la Bibilia Luka 10:18 - "Akawaambia, 'Nilimuona shetani akianguka kama radi kutoka mbinguni'."

CHANZO- BBC SWAHILI

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger