Mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya Msingi Kalangalala iliyopo mjini Geita ameuawa kwa kupigwa mateke na ngumi akituhumiwa kuiba Sh 15,000 kwenye duka lililopo jirani na nyumba yao.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe amesema tukio hilo limetokea Aprili 7,2021 wakati mtoto huyo akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Geita.
Kamanda amesema mtoto huyo alishambuliwa na mwenye duka Hamad Juma aliyetoroka baada ya tukio hilo na jeshi la polisi linamsaka.
“Mtoto huyu inadaiwa alikuwa anaiba dukani na mtuhumiwa alimkamata na kumuadhibu sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha kifo chake”amesema Mwaibambe.
Chanzo - Mwananchi
0 comments:
Post a Comment