Friday, 9 April 2021

Mpango wa nyuklia wa Iran: Nchi zenye nguvu zakutana na Marekani na Iran

...


Wanadiplomasia kutoka nchi zenye nguvu wamekutana na kila upande, Marekani na Iran, kujadili jinsi ya kufufua mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 ambao Washington ilijiondoa miaka mitatu iliyopita.

Marekani na Iran hawatarajii maendeleo ya haraka katika mazungumzo yaliyoanza katika mji mkuu wa Austria, Vienna, Jumanne wiki hii, na wanadiplomasia kutoka Umoja wa Ulaya na nchi zingine wakijaribu kupatanisha pande hizo mbili, kwaniTehran inakataa kwa sasa mazungumzo ya moja kwa moja na Washington.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alijiondoa katika makubaliano hayo, ambayo yaliondoa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran kwa kupunguza mpango wake wa nyuklia, na kuiwekea tena vikwazo vya Marekani, na kusababisha Iran kukiuka mipaka ya makubaliano ya mpango huo wa nyuklia.

Pande zilizobaki kwenye makubaliano hayo - Iran, Uingereza, China, Ufaransa, Ujerumani na Urusi - zilikubaliana Jumanne kuunda makundi mawili ya wataalam kwa lengo la kuanzisha, kwa upande mmoja, orodha ya vikwazo vya Marekani vinavyoweza kuondolewa na  upande mwingine orodha ya mambo muhimu ambayo iran itatakiwa kuheshimu na kufuata.
 
-RFI


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger