Monday 19 April 2021

MASHUA YA KWANZA DUNIANI KUTENGENEZWA KWA TAKA ZA PLASTIKI FLIPFLOPI ILIVYOTUA DAR

...
Mnamo mwaka 2016, Ali A. Skanda kutoka Lamu nchini Kenya, pamoja na wenzake wawili kwa waliungana na kutengeneza mashua waliyoiita Flipflopi kwa kutumia taka taka za plastiki zilizokuwa takribani tani kumi (10) na kuifunika kwa ndala elfu thelasini (30,000), ambapo mpaka kukamilika kwake 2018, mashua hiyo ilikuwa na uzito wa tani 8, na ndicho chombo cha kwanza cha majini duniani kutengenezwa kwa takataka za plastiki.

Tarehe 15.04.2021 mashua hiyo ilitua Dar es Salaam ikiwa imebeba ujumbe wa kuhimiza usafi wa mazingira ya Fukwe za Bahari, Maziwa pamoja na mito kwa kwa ajili ya usalama wa viumbe wanaoishi humo na afya kwa wanadamu.

Jumamosi tarehe 17.04.2021 ujumbe huo wa Flipflopi pamoja na wenyeji wao wa Nipe Fagio waliungana kufanya usafi katika ufukwe wa Minazi Mikinda Kigamboni, na kuweza kukusanya zaidi ya mifuko 90 ya takataka.

Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Nipe Fagio kutoka Tanzania kwa kushirikiana na projecti ya Flipflopi pamoja na wakazi mbalimbali wa Dar es Salaam wakiwa katika usafi wa kusafisha ufukwe wa Bahari eneo la Minazi Mikinde Kigamboni wakati ujumbe wa projecti ya FlipFlopi ulipotua Dar es Salaam, Tanzania kwa ajili ya kuhamasisha usafi wa Mazingira ya Bahari hasa kupambana na taka za plastiki pamoja na taka taka zengine ambazo ni hatari kwa viumbe hai wa Baharini.
Mashua na Boti ya FlipFlopi zikiwa katika Bahari ya Hindi eneo la Kigamboni Dar es Salaam

Muonekano wa Dampo ambalo sio rasmi, linalosabisha uchafuzi mkubwa wa ufukwe wa Bahari eneo la Minazi Mikinde Kigamboni ambapo walioshiriki wa kufanya usafi walifanikiwa kupunguza taka hizo kwa kiasi kikubwa.
Zoezi la uchambuzi wa taka likiendelea baada ya kuokotwa kutoka ufukweni mwa Bahari, zoezi hilo hufanyika ili kuweza kufahamu idadi ya taka zilizopatikana na kufahamu makampuni ambayo yanazalisha bizaa hizo zinazopelekea uchafuzi wa mazingira ya Bahari, katika zoezi la usafi Zaidi ya viroba 80 vya taka vilikusanywa, taka zilizokusanywa ni Pamoja na plastiki, nepi za Watoto, vifaa vya umeme, nguo, viatu, ndala, nyavu za Samaki, vifungashio vya vyakula na aina zingine mbalimbali.
Muonekano wa Ufukwe wa Bahari eneo la Minazi Mikinde Kigamboni kabla na baada ya kufanyiwa usafi.
Maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazotokana na urejelezaji wa Taka rejeshi

Picha na Fredy Njeje - Mpiga picha wa picha za Mazingira

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger