Mama mmoja kutoka Tana River nchini Kenya aliyejulikana kwa jina la Ann Maweni, amewashangaza mashemeji wake baada ya kutoroka na KSh170,000 za mahari ya binti yake.
Ann Maweni alikuwa amewaalika wazee kutoka kwa familia ya marehemu mume wake katika sherehe ya mahari ya binti yake kulipwa.
Kwa mujibu wa ripoti ya Daily Nation, Maweni aliwaandalia wageni pamoja na wazee chakula wakati wa karamu hiyo lakini alitoweka na pesa hizo kabla ya karamu hiyo kuisha akihofia kuwa mashemeji wake watamgeuka.
Kulingana na dada yake Veronica Meilu, Maweni alimtumia ujumbe mfupi akimuagiza afunge sherehe hiyo kwa kutoa shukrani.
Ni katika hali hii ndipo wazee walitambua kuwa mama huyo alikuwa amehepa na pesa lakini walisubiri hadi wageni walipoondoka kuzingatia suala hilo.
"Sikuwa nafahamu mipango ya dada yangu lakini nilipewa kibarua cha kuelezea namna tuliiba mahari na mahali dada yangu alikuwa," Meilu.
Wazee hao wenye hamaki waliamua kuwa watapiga ripoti kwa polisi kuhusu suala hilo na hapo ndipo Meilu alimpigia Maweni simu akitaka azungumze na wazee.
Maweni alielezea kuwa alitoroka na pesa hizo kwa sababu wazee hao hawakutakiwa kuzifurahia zote.
"Baada ya mume wangu kufariki, mlinifurusha bila chochote bali binti yangu. Mlininyanganya mwanangu wa kiume ambaye alifariki mikononi mwenyu.Na kisha mkasema mtoto wa kike hana faida katika jamii," mama huyo aliwaambia wazee kwenye simu.
Mama huyo alisema alimlea binti yake bila kusaidiwa na yeyote wakati wazee hao walimtupa na hivyo hawatakani kufurahia pesa hizo za mahari.
Maweni alifichua kwamba alikuwa amepanga njama hiyo pamoja na mkwe wake, ambapo wakkati wa kukabidhi mahari walibadilshana mabegi iliyokuwa na pesa na nyingine iliyokuwa imejaa leso.
"Nimewachia leso ya wanawake mjifunge kwa sababu hamkusimama na mjane wakati wa shida," alisema
0 comments:
Post a Comment