Thursday, 8 April 2021

ALIYEVUNJA REKODI KWA KUWA NA KUCHA NDEFU ZAIDI DUNIANI AAMUA KUZIKATA

...

Picha ya Ayanna Williams aliyekuwa na kucha ndefu zaidi duniani
***
Ayanna Williams ni mwanamke anayeishi Jijini Texas nchini Marekani, anashikilia rekodi ya kuwa binadamu mwenye kucha ndefu zaidi duniani kwa sasa na taarifa mpya zinasema amekata kucha hizo baada ya kuwa nazo kwa takribani kipindi cha miaka 30.

Ayanna Williams amesema ameamua kukata kucha hizo kwa sababu amezichoka na anataka kuwa na maisha mapya na sasa ndio muda muafaka wa kukata kucha hizo japo anajua kabisa atazikumbuka sana.

"Nipo tayari kwa maisha mapya najua nitazikumbuka sana ila ni muda wa kwenda sasa na nilikuwa nimezichoka, niwe na kucha au nisiwe nazo nitabaki kuwa Malkia kwa sababu kucha hazinitengenezi mimi japo mimi ndio nazitengeneza, nimefurahi kuzikata na ninatarajia mwanzo mpya", ameeleza Ayanna Williams

Kulingana na rekodi ya 'Guinness World Record' inasema Ayanna Willims alivunja rekodi ya kuwa binadamu mwenye kucha ndefu zaidi mwaka 2017, ambapo kucha zake zina futi 19 na inamchukua saa 20 kuzisafisha pamoja na chupa mbili za dawa.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger