Mkurugenzi wa uwezaji na utawala wa kampuni ya michezo ya kubahatisha nchini Sports Pesa ndugu Abbas Tarimba amewashauri Yanga Sc kujifunza kwa Simba Sc kutokana na ubora walionao kuanzia kwenye uwekezaji mpaka Uwanjani.
Tarimba amesema kuwa amekuwa msema ukweli siku zote pale Klabu ya Simba inapopeperusha vyema bendera ya Tanzania na anaamini kwamba itafika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba imetinga hatua ya robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa kinara katika Kundi A, ikiwa na alama 13 baada ya kucheza jumla ya mechi 6 inafuatiwa na Al Ahly yenye pointi 11.
Tarimba amesema kuwa ikiwa itatinga hatua ya fainali itakuwa ni heshima kwa Tanzania hivyo ni fursa kwa timu nyingine ikiwa ni pamoja na Yanga kujifunza.
"Siku zote mimi nakuwa mkweli nimesema hata bungeni wakati wote Simba wakifanya vizuri mimi nawapongeza na walipofika si mzaha na wameinyanyua Tanzania na ninaiona Simba fainali itakuwa ni heshima kwa Tanzania na waliowekeza pale.
"Hakika Simba wanaweka mipango kuna jambo la kujifunza kwa Yanga kwa mambo ambayo yanafanyika Simba kuanzia kwa wachezaji na uwekezaji.
"Klabu zingine ziige mfano wa Simba na nimekuwa nikimpongeza pia Mwekezaji Mohamed Dewji kwa uwekezaji wake ambao umelipa na pia najua akina Mo Dewji wapo wengi Tanzania ni wakati sasa kutumia watu kama hawa kwa faida ya nchi.
Kuhusu kauli ya Mo Dewji kusema kwamba hivi karibuni kuwa hawapati asilimia moja kutoka kwa kampuni hiyo alisema:"Hayo ni maoni yake na ana Uhuru wa kuongea, sisi tulivyofundishwa maswala ya ulinganishi vitu ambavyo vinafanana sijui alikuwa amelenga nini," .
Aidha Tarimba akazungumzia kuhusia na chapisho la Mwenyekiti wa bodi ya Simba Sc juu ya udhamini wa Sport Pesa kutofika hata Asilimia Moja ya fedha inayoipata Manchester United kutoka katika udhamini wao wa (Team Viewers )kwa kusema kuwa hakuelewa Mohamed Dewji alikua akimaanisha kitu Gani.
''Ni maoni yake kwakuwa kila mtu ana uhuru huo, lakini tulipokuwa tunakwenda chuoni kufundishwa masuala ya ulinganishi, ni lazima uweze kulinganisha vitu vinavyofanana''.
0 comments:
Post a Comment