Tuesday, 16 March 2021

AVULIWA UCHUNGAJI TUHUMA ZA KUMPA MIMBA MUUMINI WA KANISA.. 'ASKOFU AELEZA WALIVYOKWENDA GESTI'

...
Askofu Heryyabwana Majebele
***
Mchungaji msaidizi wa Kanisa la Ufunuo Ushirombo lililopo wilayani Bukombe mkoani Geita, Maliko Elikana amevuliwa wadhifa wa uchungaji na kuwa mumini wa kawaida kwa tuhuma za kumpa mimba muumini wa kanisa hilo.

Akitangaza kumvua uchungaji huo kanisani, Askofu wa Jimbo la Geita la kanisa hilo, Heryyabwana Majebele amesema ana ushahidi wa kutosha na amefuatilia mienendo ya mchungaji huyo na kubaini walikuwa wanakwenda katika nyumba ya kulala wageni na muumini huyo.

Hata hivyo, Mchungaji Elikana amekana tuhuma za kulala nyumba ya wageni na kufanya tendo la ndoa na muumini huyo.

Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger