Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesimamisha hotuba yake kwa zaidi ya dakika moja kupisha wito wa swala (adhana) ya adhuhuri wakati akitoa salamu za pole kwa Watanzania katika shughuli ya kumuaga aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli leo Jumatatu Machi 22,2021 katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Wakati akianza kutoa salamu zake katika uwanja wa Uhuru jijini Dodoma adhana ilisikika kutoka katika msikiti uliopo karibu na uwanja huo na kumfanya kiongozi huyo kusitisha kwa muda kutoa hotuba yake na adhana ilipomalizika aliendelea na maelfu ya watu waliopo uwanjani hapo walimpigia makofi.
Katika hotuba yake Kenyatta amemwomba Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuendeleza falsafa ya Hapa Kazi Tu aliyoiacha Magufuli kwa kuwa inawafanya Watanzania kuwa na moyo wa ushujaa na kusonga mbele.
Amemtaka Rais Samia kujipa moyo wa ushujaa bila kuteteleka na kuwa Kenya itakuwa pamoja naye wakati wote.
Pakua / Download App ya Malunde 1 blog Tuwe tunakutumia taarifa zote moja kwa moja kwenye simu yako bure kabisa
0 comments:
Post a Comment