Tuesday, 8 September 2020

Picha : SALOME MAKAMBA AZINDUA KAMPENI KWA KISHINDO SHINYANGA MJINI…AZUA GUMZO AKIFANYIWA TAMBIKO LIVE JUKWAANI…TAZAMA HAPA

...
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Maelfu ya wakazi wa Shinyanga Mjini wamejitokeza katika Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi za Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Uzinduzi huo wa aina yake ulioambatana tukio la Mgombea huyo wa Ubunge Salome Makamba ‘Ng’wana O – Shimba’ kufanyiwa tambiko na kupewa silaha za jadi na wazee wa kimila umefanyika leo Jumanne Septemba 8,2020 katika eneo la Ngokolo Mitumbani Mjini Shinyanga.

Shangwe zilisika zaidi mara baada ya Mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Salome Makamba kumaliza mkutano wake wa hadhara ambapo viongozi wa CHADEMA waliwakaribisha Jukwaani wazee wawili wa Kisukuma wakiwa na vifaa vya kimila ambapo mmoja wa wazee hao alizua gumzo akimfanyia tambiko Mgombea Ubunge Salome Makamba Mubashara Jukwaani. 

Akinadi sera zake, Salome Makamba ambaye ni Mwanasheria amewaomba wakazi wa Shinyanga kutofanya makosa katika uchaguzi Mkuu 2020 hivyo wamchague yeye kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kwani amedhamiria kuwaletea maendeleo.

Salome Makamba pamoja na mambo mengine ya kuwaletea maendeleo wananchi, asema miongoni mwa vipaumbele vyake ni masuala ya elimu,uchumi na kupigania haki za wanawake na watoto.

Naye Meneja Kampeni  wa Salome Makamba, Juma Protas alisema uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 siyo wa kufanya masihara na kuwasihi wananchi kuacha ushabiki wa siasa hivyo wafanye maamuzi sahihi kwa kuchagua wagombea wa CHADEMA akiwemo Tundu Lissu kuwa Rais wa Tanzania,wabunge na madiwani wa CHADEMA ili kuwaletea maendeleo wananchi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwasalimia wananchi wa Shinyanga wakati wa uzinduzi wa Kampeni  katika eneo la Ngokolo leo Jumanne Septemba 8,2020. Kulia ni Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi ambaye ni Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini leo

Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini leo
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiomba kura kwa wananchi wa Shinyanga wakati wa uzinduzi wa Kampeni  katika eneo la Ngokolo leo Jumanne Septemba 8,2020

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni  katika eneo la Ngokolo leo Jumanne Septemba 8,2020

Meneja Kampeni  wa Salome Makamba, Juma Protas (kushoto) Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi na Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini wakiwa jukwani.
Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini leo

Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini leo
Vijana wa Sarakasi wakionesha vipaji vyao
Vijana wa Sarakasi wakionesha vipaji vyao
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA 
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA 
Mzee wa kimila akimvalisha vifaa/mavazi kimila Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakati akimfanyia tambiko maalumu kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini
Mzee wa kimila akimvalisha vifaa/mavazi kimila Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akifanyiwa tambiko maalumu kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini
Wazee wa kimila wakiendelea kumfanyia tambiko Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Wazee wa kimila wakiendelea kumfanyia tambiko Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini
 Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiendelea kufanyiwa tambiko maalumu kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini

Wananchi wakifuatilia tukio la kufanyiwa tambiko
Wazee wa kimila wakiendelea kufanya tambiko
 Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwa amesimama wakati  akifanyiwa tambiko maalumu kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini
 Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiondoka eneo la mkutano wa kampeni baada ya kufanyiwa tambiko kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini

Wananchi wakichangia kampeni za CHADEMA wakati wa uzinduzi wa kampeni za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini

Wananchi wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Kampeni za CHADEMA
Viongozi wa CHADEMA wakiwa wamekaa jukwaa kuu

Wananchi wakimsindikiza Salome Makamba baada ya uzinduzi wa kampeni za CHADEMA

Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger