Mnamo tarehe 19.08.2020 majira ya saa 03:00 usiku huko Mtaa wa Kagwina, Kata ya Sinde, Tarafa ya Sisimba Jijini Mbeya. Mtu / watu wasiofahamika walichoma moto nyaraka mbalimbali zilizokuwa ndani ya ofisi ya CHADEMA Wilaya ya Mbeya Mjini iliyopo eneo hilo. Ofisi hiyo ni ya chumba kimoja ambacho Chama cha Demokrasia na Maendeleo wamepanga kwenye nyumba ya ANNA ABEL @ MWANSASU.
Mbinu iliyotumika ni kuvunja kufuri la mlango wa ofisi, kuingia ndani kisha kutoa baadhi ya nyara kazi ilizokuwa kabatini, kuziweka sakafu na kisha kuzichoma moto. Nyaraka hizo ni pamoja na fomu za matokeo ya kura za maoni kwa wagombea nafasi ya Udiwani, viti maalum wanawake jimbo la Mbeya mjini ambazo zilitakiwa kusafirishwa leo tarehe 19.08.2020 kwenda Makao Makuu – Dar es Salaam .
Aidha vitu vingine vilivyochomwa moto ni pamoja na vitivi nne vya plasti kina mlango mmoja wakabati lililokuwa limehifadhi nyara kahizo.
Ofisi hiyo haina ulinzi Thamani ya mali iliyoteketea bado kufahamika. Kiini cha tukio kinachunguzwa japo uchunguzi wa awali umebaini kuwa kulikuwa na hali ya kutoridhika kwabaadhi ya wajumbe/wagombea kuhusiana na matokeo ya kura za maoni za Viti Maalum naUdiwani.
Ufuatiliaji unaendelea ikiwa ni pamoja na msako wa kuwakamata wa husika kwa hatua zaidi za kisheria.
Imetolewana:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
0 comments:
Post a Comment