Watu 10 wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyohusisha lori aina ya Scania lenye tela namba T 394 DHK na Costa ya abiria yenye namba T 147 DHZ, inayofanya safari za Mbezi kwenda Morogoro.
Imeelezwa kuwa kati yao, majeruhi wanne wako mahututi, wamepelekwa hospitali.
Akizungumza katika eneo la ajali hiyo, Kamanda wa Polisi, Willbroad Mutafungwa amesema tela la lori namba T 394 lilikatika katika kiunguo cha kichwa cha lori hilo na kuangukia basi dogo katika maeneo ya Junior Seminary.
Kamanda Mutafungwa amewataka madereva kuwa makini barabarani.
Dereva wa lori hilo amekimbia na anatafutwa na polisi. Pia, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Goodluck Zelothe amesema kuwa baada ya kupata taarifa ya ajali hiyo walifika mara moja wakiwa na vifaa vya uokoaji.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare, amewaonya madereva na wamiliku wa magari kufanya ukaguzi wa magari yao kabla ya kuanza safari barabarani.
0 comments:
Post a Comment