Katika jitihada za kuhakikisha Sekta ya habari inatoa mchango katika Ushiriki wa Wanawake katika masuala ya uongozi, Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) unatoa Mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa habari 40 kutoka mikoa wa Mara na Shinyanga ili kuwajengea uwezo wa kuandika habari zenye tija na ili kuhamasisha usawa na mgawanyo wa majukumu katika jinsia zote katika jamii.
Hayo yamebainishwa Agosti 13, 2020, Mjini Shinyanga na Mwezeshaji wa Mafunzo hayo kutoka (TGNP) Dkt. Ananilea Nkya,alisema kuwa Waandishi wa habari kupitia vyombo vyao vya habari wanalojukumu la kuwahamasisha wanawake kushiriki kikamilifu katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika jamii hususani katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu.
Alisema kuwa Waandishi wa habari wanapaswa kutumia kalamu zao kuondoa Mila na desturi ambazo ni kandamizi zilizopo katika jamii zisizompa fursa mwanamke kushirikishwa katika uongozi ili kuwawezesha kutambua haki zao.
“Nyinyi Waandishi wa habari kupitia vyombo vyenu vya habari hakikisheni mnawasaidia jamii kuondokana na mila hizi kandamizi zenye mrengo wa mfumo dume ili kutoa fursa kwa wanawake kushirikishwa katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika maeneo yao wanayoisho,”alisema Nkya.
Alifafanua kuwa ni budi waandishi wa habari kupita vyombo vyao vya habari wakaanda vipindi na kuandika habari zinazohusiana na mafanikio mbalimbali yaliyotekelezwa na viongozi wanawake ili kuwaibua wangine ambao walishakata taama kutokana na mila hizo katika jamii.
0 comments:
Post a Comment