Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifungia kipindi cha Jahazi Cha Clouds FM kwa kosa la kurusha maudhui yenye kuchochea kujichua sehemu za siri na ngono. Clouds FM imetakiwa kutokujaza muda huo kwa kipindi kingine chenye maudhui sawa na Jahazi.
Aidha Wasafi Media Online TV imetuhumiwa kurusha maudhui yanayochochea vitendo vya ngono kupitia kipindi cha Women Matters. Kosa la ngono kamati imetoa onyo na faini ya milioni 5 itakayolipwa TCRA.
Wakati huohuo, TCRA imetoa onyo kali na kuziweka chini ya uangalizi wa miezi mitatu Radio Free Africa na Radio One Stereo kwa kukiuka kanuni za utangazaji viliporusha kipindi cha Amka na BBC ambapo Tundu Lissu aliituhumu serikali kuwazuia viongozi wa Chadema kumuaga Hayati Rais Benjamin Mkapa.
0 comments:
Post a Comment