Sunday, 16 August 2020

TAKUKURU Yamshikilia Mfanyabiashara kwa tuhuma za ukwepaji kodi, udanganyifu na utakatishaji fedha haramu

...
TAKUKURU inamshikilia kwa mahojiano Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya White Star Investment Taalib Karim Mbowe, inayofanya biashara ya usafirishaji ndani na nje ya nchi kwa makosa ya ukwepaji wa kodi, udanganyifu na utakatishaji wa fedha haramu.

Taarifa hiyo imetolewa leo Agosti 16, 2020, na Afisa Uhusiano wa TAKUKURU Doreen Kapwani, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo, ambapo licha ya uchunguzi huo Taasisi hiyo pia inachunguza vichwa vya malori 100 vinavyomilikiwa na mfanyabiashara huyo.

Aidha TAKUKURU pia inachunguza mikopo ya mfanyabiashara huyo ya zaidi ya Dola za Marekani 3,000,000, sawa na Bilioni 6.3 za Kitanzania kutoka Benki ya Barclays, pamoja na Dola 540,000 sawa na Bilion i 1.1 kutoka Benki ya Equity.

Uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo ukikamilika, mfanyabiashara huyo atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger