Friday, 14 August 2020

Rais Magufuli apewa Tuzo ya umahiri kwa kupambana na Corona

...
Baraza kuu la Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), limemkabidhi Tuzo maalum Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutambua mchango wake katika kuliongoza Taifa kumtegemea Mungu katika kipindi cha janga la Virusi vya Corona nchini.

Tuzo hiyo amekabidhiwa leo Agosti 14, 2020, na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dkt Barnabas Mtokambali, katika Mkutano Mkuu wa Baraza kuu la Kanisa la TAG, wakati akifungua mkutano huo, uliofanyika Jijini Dodoma.

Aidha Askofu Mtokambali amesema kuwa jambo lililofanywa na Rais Magufuli katika kipindi kile la kuruhusu shughuli za kimaendeleo ziendelee kama kawaida, lilikuwa la tofauti kwani ni katika kipindi hiko ambapo Mataifa mengine yaliweka nguvu yakuzuia watu wasitoke majumbani.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger