Monday, 17 August 2020

Majina ya Wagombea Ubunge Watakaoteuliwa na CCM Kujulikana Wiki Hii

...
Majina ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) watakaoteuliwa kugombes ubunge kwenye Bunge la Tanzania na uwakilishi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar yanatarajiwa kufahamika wiki.

CCM imetoa ratiba ya vikao vya uteuzi wa wabunge na wawakilishi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, vikao hivyo vya kuchekecha majina vinaanza leo. Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu kitaketi kesho na pia kitafanyika kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa.

Agosti 20 hadi 21 kitafanyika kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Agosti 22 Jumamosi kitafanyika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger