Wednesday, 19 August 2020

MAISHA MAPYA ACHUKUA FOMU KUGOMBEA URAIS TANZANIA KUPITIA NLD

...


Mgombea urais kwa Tiketi ya Chama NLD Bw. Maisha Mapya Mchunguzi baada ya kuchukua fomu NEC

Ikiwa zimesalia siku Saba kufikia ukomo wa kurejesha fomu wagombea kwa nafasi ya Urais leo mgombea wa nafasi hiyo kwa Tiketi ya Chama NLD bwana Maisha Mapya Mchunguzi amejitokeza ofisi za Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC na kukabidhiwa fomu hiyo.

Akikabidhi fomu hizo kwa Mgombea huyo wa Urais wa Jamhuri ya Muungano Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji mstaafu Semistocles Kaijage amemtaka mgombea huyo kupitia na kuzisoma fomu hizo na kuzijaza ipasavyo kabla ya kuzirejesha kwa ajili ya uteuzi.

"Ndani ya mkoba huo tumekukabidhi fomu pamoja na kitabu Cha maadili kisome kitakupa mwongozo wa ukizingatia matakwa ya Kisheria kabla ya zoezi la Uteuzi."

Awali mgombea huyo amepatiwa maelekezo ya awali kuhusu kuzunguka katika mikoa kumi ili kutafuta wadhamini Mia mbili ambao watakamilisha hesabu ya wadhamini takribani 2000 wanaotakiwa huku mgombea huyo kutoka Chama Cha NLD akielezea vipaumbele vyake kama Chama Hicho kitashika hatamu.

"Nina Imani kubwa na watanzania watakipatia nafasi Chama changu Cha NLD na sisi vipaumbele vyeti Kama Chama ni kuhusu uchumi shirikishi utakaogusa kila sekta."

Hadi kufikia Sasa kwa mujibu wa Taarifa za Time ya Taifa ya Uchaguzi Mgombea huyu kutoka NLD anakamilisha hesabu ya jumla ya vyama 17 vilivyojitokeza kugombea kwa ngazi ya Urais.
 Chanzo - EATV
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger