Friday, 14 February 2020

Picha : WANAFUNZI 700 WA SHULE YA SEKONDARI SHINYANGA 'SHY BUSH' WAANDAMANA ZAIDI YA MASAA MANNE KWENDA KWA MKUU WA MKOA

...
Na Mwandishi wa Malunde 1 blog
Wanafunzi zaidi ya 700 wa shule ya Sekondari Shinyanga maarufu 'ShyBush'  wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wameandamana hadi ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, umbali wa zaidi ya kilomita 30 kufikisha kilio chao wakidai kunyanyaswa na mkuu wao wa shule na mwalimu wa nidhamu.

Wanafunzi hao wameanza kuandamana leo Ijumaa Februari 14,2020 kuanzia majira ya 11 alfajiri hadi saa nne tatu asubuhi ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack huku wakiamini kuwa yeye ndiye anayeweza kutatua tatizo lao kutokana na kuvumilia kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi wa kusikilizwa.

Kaka mkuu wa shule hiyo Mwendesha Manyangu akizungumza kwa niaba ya wanafunzi amesema malalamiko mengi ya wanafunzi ya kudai kutotendewa haki na mkuu wao wa shule Malambi Malelemba pamoja na baadhi ya walimu akiwemo wa nidhamu yameshindwa kupatiwa ufumbuzi ndiyo maana wameamuwa kwenda kwa mkuu wa mkoa ili kupata ufumbuzi.

Kiongozi huyo wa wanafunzi alisema wanafunzi wanashindwa kujua simu wanazokamatwa nazo zinakwenda wapi kwani hawazioni zikichomwa moto licha ya kujua kuwa hairuhusiwi kuwa na simu pamoja na kupewa adhabu kwa makosa ambayo wangeweza kuonywa na baada ya kubaini hayo walikubaliana kwenda kwa mkuu wa mkoa kufikisha kilio chao.

“ Tunaamini mkuu wa mkoa atatusikiliza  na kutatua matatizo yaliyopo na hapa tatizo ni mkuu wetu wa shule tunapomueleza matatizo yaliyopo hayapatii ufumbuzi hata idara ya nidhamu nao hawachukui hatua sasa mwanafunzi anaambiwa anyowe kipara wakati haitakiwi anapewa adhabu”,alisema Manyangu.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amewasihi wanafunzi hao kuacha kujiingiza kwenye migomo isiyo ya maana ambayo inawapotezea muda wa masomo yao,huku akiwataka kuzingatia maadili na kujiepusha na vitendo ambavyo vitarudisha nyuma maendeleo ya taaluma yao na kushindwa kufikia ndoto zao.

Aliwataka wanafunzi kuwa watulivu kwani suala lao analifanyia kazi ili kuhakikisha changamoto zilizopo zinatatuliwa,huku akiiagiza idara ya elimu halmashauri ya Kishapu kuhakikisha wanafika shuleni hapo na kutatua changamoto za wanafunzi ikiwa ni pamoja kufuatilia maendeleo yao .


Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Joseph Paul aliwataka wanafunzi kuachana na makundi ambayo hayawajengi kuanzisha migomo isiyo na maana na kuwaeleza kuwa anawashukuru kwa kuwa hawakufanya fujo na kuharibu mali za shule.
Maandamano ya Wanafunzi wakiingia kwenye geti la kuingia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo



Wanafunzi wakiwa wamekaa chini wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack
Wanafunzi wakipanda kwenye gari la polisi kwa ajili ya kurudishwa shuleni kwao.
Wanafunzi wakipanda kwenye gari la polisi kwa ajili ya kurudishwa shuleni kwao.
Wanafunzi wakiwa katika eneo la Ibadakuli barabara ya Shinyanga - Mwanza wakiandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Wanafunzi wakiwa katika eneo la Ibadakuli barabara ya Shinyanga - Mwanza wakiandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Wanafunzi wakiwa katika  barabara ya Shinyanga - Mwanza wakiandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga


Wanafunzi wakiwa katika  barabara ya Shinyanga - Mwanza wakiandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger