








Mgeni rasmi ,Waziri Kairuki akikabidhi Kombe kwa nahodha wa timu ya Kisiwani united mara baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya soka ya Ujamaa fc bao 2 kwa 1.
Waziri Kairuki akikabidhi fedha taslimu ,kiasi cha Sh Milioni 1.5 kwa nahodha wa timu ya Kisiwani United mara baada ya kuibuka Mabingwa wapya wa mashindano hayo.

Na Dixon Busagaga ,Moshi.
Mabingwa wapya wa mshindano ya Angela Kairuki Cup
2019 timu ya Kisiwani united wamekabidhiwa zawadi zao ambapo wamefanikiwa kijinyakulia zawadi ya Ng'ombe pesa
taslimu kiasi cha sh Mil 1.5,Pikipiki moja, na Medali 25 kwa Wachezaji.
Zawadi kwa mabingwa hao wapya zimekabidhi na Waziri wa Nchi ,ofisi ya Waziri Mkuu,Uwekezaji ,Angela Kairuki mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali kati ya timu ya Kisiwani United kutoka kata ya Kisiwani dhidi ya timu ya Ujamaa fc ,ambapo Kisiwani walifanikiwa kushinda kwa mabao mawili kwa moja.
Mshindi wa pili katika mashindanohayo,timu ya Ujamaa fc wamejinyakulia kitita Cha sh Mil moja,Medali na pikipiki
huku mshindi wa tatu,timu ya Kiwanja fc akiambulia kiasi Cha sh laki tano pamoja na medali.
Katika mchezo huo mabao ya washindi yalipachikwa na Wachezaji Ally Rajab kunako dakika 35 ya kipindi cha kwanza huku mchezaji Juma Makumbi akipigilia msumari wa pili uliowapatia ubingwa timu ya kisiwani fc.
Bao kwa upande wa timu ya soka ya Ujamaa fc iliyokuwa imesheheni wakongwe limefungwa na mchezaji Ezekiel Ombeni kunako dakika ya 40.
Katika mchezo huo ilishuhudiwa mchezaji Ally Mbaga akitolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kichwa mwamuzi wa pembeni wakati akilalamikia maamuzi yake dhidi ya bao lililofungwa n timu ya Ujamaa fc.
Mashindano ya Angela Kairuki Cup yamekuwa yakifanyika kila
mwaka katika wilaya ya Same na kushirikisha timu kutoka kata 32 za wilaya hiyohuku mdhamini Mkuu wa mashindano hayo ,Wazxiri wan chi,ofisi ya Waziri Mkuu,uwekezaji ,Angela Kairuki akiahidi kuendelea kuyadhamini kwa miaka mitano.
0 comments:
Post a Comment