Saturday, 28 September 2019

Iran yaikosoa Marekani kwa kumyima ruhusa waziri wake wa mambo ya Nje Javad Zarif kumtembelea hospitalini Balozi wa Iran

...
Iran imeikosoa Marekani kwa uamuzi wa kikatili wa kumzuia waziri wake wa mambo ya kigeni Javad Zarif kumtembelea hospitalini Balozi wa Iran kwenye Umoja wa Mataifa Majid Takht Ravanchi anaetibiwa ugonjwa wa saratani mjini New York. 

Zarif anahudhuria mkutano wa kilele wa hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa mjini humo. 

Shirika la habari la kitaifa nchini humo IRNA limemnukuu naibu waziri wa mambo ya kigeni Abbas Araghchi akisema Marekani imeligeuza suala hilo la kibinaadamu kuwa la kisiasa. 

Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani imesema itamruhusu iwapo Iran itamuachia huru mmoja wa raia wengi wa Marekani wanaodaiwa kushikiliwa kimakosa nchini Iran. 

Mwezi Julai Marekani ilitangaza kumzuia waziri huyo kuingia nchini humo, ikiwa ni miongoni mwa vikwazo vyake dhidi ya taifa hilo.

-DW


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger