Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemzawadia Askari Polisi PC Alphonce Daniel Mwambenga sh. 200,000 kutokana na ujasiri wake wa kumdhibiti kwa kumkanyaga nyoka mkubwa aliyekuwa akieleakea jukwaa kuu wakati Waziri Mkuu akihutubia katika Kilele cha Wiki ya Viziwi Duniani kwenye Uwanja wa Kichangani, Kihesa mjini Iringa, Sepotemba 28, 2019.
Kitendo hicho kilifanyika kimyakimya hivyo hapakuwa na taharuki yoyote . Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akimkabidhi Mwambenga fedha hizo. Wapili kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara y a Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Dkt.Avemaria Semakafu. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na wa nne kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamkahanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
0 comments:
Post a Comment