Wanafunzi saba wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya jengo la darasa la Shule ya Precious Talent kuanguka eneo la Ngado Nairobi nchini Kenya saa 1 asubuhi leo Jumatatu Septemba 23, 2019.
Shule hiyo ipo mkabala na Barabara ya Ngong'; shughuli za uokozi zinaendelea kwa sasa huku ikiarifiwa tayari wanafunzi zaidi ya 50 wametolewa kwenye vifusi na kupelekwa Hospitali Kuu ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH).
Kwa Mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya shughuli ya uokoaji inaendelea na wanafunzi wanne wamepelekwa Hospitali ya Taifa ya Kenyatta.
0 comments:
Post a Comment