Ajali
mbaya imeyohusisha mabasi mawili ya kampuni ya City Boy imetokea katika
kijiji cha Maweni wilaya ya Manyoni, Singida na kusababisha watu 29
kupoteza maisha papo hapo huku chanzo cha ajali kikitajwa kuwa ni mwendo
kasi.
Mabasi hayo yenye namba za usajili T531 DCE na T247 DCD, moja lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Kahama na lingine likitokea Kahama kuelekea Dar es Salaam.
Moja
ya mashuhuda wa ajali hiyo amesema kuwa madereva wa mabasi yote
walikuwa katika mwendo kasi na wakati ajali inatokea walikuwa
wakisalimiana kwa kunyosheana mikono kisha basi moja kupoteza mwelekeo
na kuingia upande wa basi lingine na ndipo yakakutana uso kwa uso na
kusababisha ajali hiyo.
Kamanda wa Polisi Singida, Thobias Sedoyeka tayari amethibittisha kutokea ajali hiyo na uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika.
Katika
hatua nyingine Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi na kueleza
kuwa amepokea taarifa hiyo kwa mshtuko na amesikitishwa na ajali hiyo
ambayo imechukua maisha ya watanzania.
0 comments:
Post a Comment