Taarifa Rasmi kwa
Umma kuhusu Programu ya Pre-Entry ya Kutoka IMTU
Itakumbukwa kuwa Tume ya Vyuo Vikuu katika kikao
chake cha 52 cha tarehe 18 Machi 2011 iliamua kuwa kuanzia mwaka wa masomo 2011
/ 2012 hakutakuwa tena na Programu za Pre-Entry na vyuo vyote viliagizwa
kusitisha ufundishaji wa programu hizo. Vyuo vikuu vyote vilijulishwa kuhusu
maamuzi hayo kwenye kikao maalum cha saba cha kamati ya pamoja ya udahili
(Joint Admission Committee) tarehe 9 Februari 2012. Kwa maamuzi hayo vyuo vyote
viliagizwa kuandaa na kuwasilisha programu za aina hiyo kwa kutumia mfumo mpya
wa Tuzo za Vyuo Vikuu (University Qualifications Framework – Level 6).
Hata hivyo hivi karibuni ilibainika kuwa Chuo
Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU) kilikuwa kikiendelea
kufundisha programu hiyo na wanafunzi 111 walihitimu katika programu hiyo. Kwa
kuwa programu hiyo ilikuwa haitambuliwi na Tume, wahitimu hao walikata rufaa
kwa Mheshimiwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa mujibu wa sheria ya
vyuo vikuu Sura ya 346 ya sheria za Tanzania. Baada ya kupitia rufaa yao,
Mheshimiwa Waziri kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 5(2)(b)
aliagiza kwamba wahitimu hao 111 wa programu ya Pre-entry ya IMTU waruhusiwe
kusoma programu ya MBBS ya IMTU kwa
1
kuwa ndivyo ilivyokusudiwa wakati wa kuanzisha
programu hiyo.
Kutokana na maagizo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi, tunapenda kuujulisha umma ya kwamba, kwa kuwa IMTU imesitishwa
kudahili wanafunzi wapya kwa mwaka wa masomo 2014 / 2015 wahitimu hawa wanaweza
kudahiliwa chuo kingine chochote kilicho tayari kuwapokea kufuatana na taratibu
za udahili zilizopo.
Aidha, Tume inasisitiza kuwa programu za
Pre-entry zilishasitishwa na kuwa programu zote za masomo lazima zifanyiwe
tathmini na kupata ithibati ya Tume kabla hazijaanzishwa na kudahili wanafunzi.
Kwa taarifa hii tunawataka vyuo kuwasilisha programu zao ili kupatiwa ithibati
kabla ya kuanza kudahili wanafunzi ili kuepusha usumbufu wa namna hii.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
2
0 comments:
Post a Comment