Yanayojiri Bungeni Dodoma: Leo Jumatano, Tarehe 26 Novemba, 2014
Habari wakuu,
Moja kwa moja kutoka bungeni Dodoma, leo tunaanza safari yetu yetu ya hitimisho kuhusu Escrow, japo kuna zuio la mahakama jana spika alisema bunge lina kinga na hakuna atakaezuia bunge lisijadili ripoti. Zitto pia amesema kamati ya PAC itawasilisha ripoti yake kama ratiba ilivyosema. Baada ya pilikapilika za usiku Dodoma tusubiri kitachojiri bungeni leo.
Hakikisha kifaa unachotumia kutembelea JamiiForums kina chaji ya kutosha kutokana na hofu ya TANESCO pia kifurushi chako kiwe kinatosha kuperuzi hii kurasa mara nyingi iwezekanavyo.
============================== ===========================
Kamati ya Uongozi imekutana sasa hivi
Bunge limeanza na aliekalia kiti leo ni mwenyekiti wa bunge, mheshimiwa Zungu kuna maelezo juu ya malalamiko ya walimu, maelezo yanatolewa na upande wa serikali
Swali: Wapo watumishi kama wauguzi wanadai zaidi ya milioni 100, japo kulikuwa na ahadi swala hili litashuhulikiwa, lakini hadi leo, nini kauli ya serikali?
Jibu: Hospitali ya Tumbi ilipandishwa hadhi lakini bado haimudu. Mpaka sasa serikali imeshatoa bilioni tano kwa ajili ya jengo la upasuaji na baadhi ilinunua dawa. Serikali katika bajeti ya sasa imetenga pesa zaidi ili kufanikisha jengo la upasuaji
Swali(Zainabu): Ni lini serikali itatoa pesa ili hospitali ya Tumbi ikamilishe ujenzi? Lini hospitali za wilaya zitaweza kujitegemea kulingana na jiographia mkoa wa Pwani ngumu kwenda Tumbi
Jibu: Jambo linafatiliwa na namuhahakishia Mbunge tunafatilia fedha. Ni jambo la msingi tu tunazingatia kuzipa uwezo hospitali za wilaya
Swali (Mariam): Serikali ina mpango gani kuhahakisha Tumbi inapata madaktari bingwa kutukana na ajali
Jibu: Wizara ya afya ina mpango na madaktari washapatikana MOI na watasambazwa ikiwemo hospitali ya Tumbi
Swali(Mwanjelwa): Walimu wa Mbeya baada ya kujiendeleza bado wanalipwa mishahara kiduchu
Jibu: Kulingana na taratibu watumishi hupandishwa vyeo kulingana na sifa, baada ya kujiendeleza wanatakiwa kupandishwa daraja. Ni kweli wapo baadhi ya walimu walipandishwa lakini bila kufata taratibu lakini tumeshatoa agizo lirekebishwe na tutaendelea kufatilia
Swali(Nyongeza-Mwanjelwa): Kwa kua lishakua kero, serikali inawaambia nini halmashauri?
Jibu: Mpango wa serikali kuunda tume ya kusimamia mishahara ya walimu itamaliza tatizo, na suala la madai kama pensheni na mengineyo linahitaji kufatiliwa na mheshiwa alete malalamiko sisi tutafatilia.
Swali: Kuna walimu wameenda kusoma lakini walivyorudi wameendelea kufundisha shule za msingi wakati kuna uhaba shule za kata, serikali wanasemaje kuhusu hilo?
Jibu: Muundo wa utumishi umerekebishwa, kwa walimu waliojiendeleza kada isiyo ualimu inategemea na nafasi zilizopo serikalini na kama nafasi hamna anaendelea na ajira yake ya mwanzo.
Swali: Kuna maksudi inafanyika kutopandisha daraja walimu waliosomea kada tofauti kujiendeleza
Jibu: Kuanzia mwaka huu, serikali kwa watumishi wote wanaopanda vyeo imeagiza maafisa utumishi wawapandishe kwa wakati.
Swali(Murtadha): Je! Serikali ina mpango gani wa kutoa gawiwo kwa jamii inayozunguka kwenye uvuvi
Jibu: Serikali imeweka utaratibu wa mgawanyo wa mapato kwa serikali kuu na serikali za mitaa kwa mapato yanayokuswanywa kulingana na kanuni za uvuvi.
Nyongeza(Murtadha): Sikumaanisha uvuvi mdogo unaofanyika halmashauri, ni jinsi gani mapato yanayopatikana bahari kuu yanarudi kuwaendeleza wavuvi wadogo? Kwa jinsi serikali iko tayari kuboresha
Jibu: Kuna utaratibu wa kuweka asilimia mbalimbali kurejesha mapato kwa wavuvi wadogo wadogo, tutwasaidi kujenga mabwawa na kutafuta chakula cha samaki
Swali: Wavuvi pesa zinachukuliwa wakaliwa wakati mrejesho hakuna na halmashauri wanakula pesa zote
Jibu: Swala la uvuvi kama kulikuwa na makosa, hiyo trend tunaibadilisha kwa sababu tumeingia watu wapya.
Swali: Sekta ya uvuvi haijachangia pato stahiki kama inavyotarajiwa, serkali ina mpango gani kuwapatia wavuvi wadogo zana za kisasa
Jibu: Nakubaliana na mbunge lakini sekta kwa sasa inakua kwa kasi sana na kuna mpango wa kuwasaidia kupata vifaa na tumeshatenga fedha na hii habari sasa tunaiangalia na lazima tuwajali hawa watu
Swali: Hawatozi mrahaba zaidi ya leseni, kwa nini serikali ina kigugumizi kuwatoza mrahaba wavuvi wakubwa?
Jibu: Ni kweli hatujafanya vya kutosha katika mrahaba lakini tunaomba muheshimiwa atupe muda kwa sababu tunarejea kanuni kipindi hiki
Swali: Serikali itasimamia vipi miondombinu ya maji taka
Jibu: Wananchi wanajiunganishia mambomba ya maji taka kiholela, serikali ina mpango wa kuboresha mfumo wa maji taka na mitambo mitato itawekwa, tupo katika mchakato wa kumpata mhandisi mshauri
Swali: Nyongeza: Majibu hafifu, kwa serikali imekiri, Je serikali haioni halmashauri ya DSM imeshindwa haini inatakiwa kuwajibishwa? Na mashimo katika ya jiji yanasubiri mshauri
Jibu: Tumetenga bilioni kumi hivyo tunashughulikia na tuwaombe DAWASCO tulishughulike hili swala
Swali: Watu wanaongezeka DSM, Je! hamna umuhimu kuongeza special bajeti kukarabati miundominu
Jibu: Ushauri tumepokea na pesa ambazo tumeshatenga litaanza kushughulikia tatizo.
Swali: Maji taka yanatiririka na hakuna jitihada za DWASCO, nini mpango wa serikali kuondoa kero hii
Jibu: Tuendelee kushirikiana na wizara ya maji, tushughulikie tatizo hili kwa haraka.
Swali: Maji taka husafishwa hadi mara tatu kabla ya kumwaga, Je! DSM yanasafishwa mara ngapi?
Jibu: Nachoelewa husafishwa ila kitaalamu husafishwa mara ngapi sina hilo jibu
Swali(Shekifu): Serikali inachungua hatua gani kufikisha maji katika vijiji vya Rombo, Itasaidiaje wilaya ya Lushoto kuzuia kuharibu mazingira?
Jibu: Tutayafanya haya kadri pesa zinatavyokua, tunapokea changamoto. Swala la mazingira kila mwananchi ana jukumu la kutunza mazingira na tutaendelea kutoa semina.
Swali: Mradi wa maji ya ziwa Victoria haitatosheleza vijiji vyote vya Kishapu, Je! Muheshimiwa waziri atapokuja aje na wataalamu maji yawafikie wananchi
Jibu: Nakubali na nafahamu na ushauri alioutoa tutauzingatia
Swali: Lipo tatizo la serikali kupeleka pesa zinazoonekana katika mtandao lakini Kasulu hazifiki
Jibu: Nakubali tumeshaonana na tuna mpango wa kufika kwake, wizara ya nmaji pesa zikishatengwa ni suala za utaratibu tu lakini zitafika.
Swali (Ngonyani): Serikali itakua tayari kufungua mradi wa maji Mombo?
Jibu: Nimeshanya ziara kata ya Vuga na nimeshaagiza wapete maji kwenda Mombo kilichobaki ni utekelezaji tu.
Swali (Chilolo): Mji hauna umeme japo ni makao makuu ya wilaya, serikali itakua tayari kutenga pesa kwa ajili ya kupeleka umeme
Jibu: Serikali kupitia REA ilipeleka umeme Nduguti, umeanza kutekelezwa tangu 2013/14 na unakamiliki June 2015
Swali nyongeza Chilololo: Mitaa iliopata umeme Nduguti ni michache, mitaa iliyobaki itamaliziwa na REA kwa bei poa au TANESCO
Jibu: Utekelezaji ya mradi wilaya ya Mkalama unaendelea, mpaka kufikia June mwakani ndo utakamilika hivyo wananchi wanaohitaji umeme wajiandikishe.
Swali: Wilaya ya Kasulu kuna chuo cha ualimu Kabanda, ni lini umeme utapelekwa Kabanga?
Jibu: Kuweka umeme maeneo mbalimbaili ni wajibu wetu serikali, huwa tunaweka vipaumbele kwenye huduma za jamii hivyo tutaangalia jinsi gani tunaweka
Swali: Bado kuna tatizo gani za gharama za nguzo, nguzo hizi ziwe bura auz ipunguzwe sana?
Jibu: Ushauri tumeuchukua na kuangalia TANESCO wanawezaje kupata umeme wa namna hio
Swali(Hussein): Umeme umeshashushwa Nyang'alwe lakini nguzo hamna
Jibu: Mahitaji ya nguzo nchi nzima ni makubwa sana lakini kuna mpango tunaufanya
Swali: Mradi REA unasaidia, ni vijiji vingapi Tabora vitapatiwa umeme
Jibu: Serikali kupitia REA ina peleka umeme katika vijiji(anavitaja) ni vijiji 16 na utekelezaji umefikia 19%. Unatarajia kukamilika 2015
Swali: Waziri anathibitishia kuwa wakandarasi watafika na watakamilisha kabla ya mwezi wa sita mwakani? Mkandarasi hana nguzo, je serikali inatuhakikishiaje kama kazi itakamilika kama ilivyopangwa
Jibu: Mkandarasi ashafanya survey na ni kweli hakua na nguzo lakini ameshaagiza nguzo kutoka SA, Kenya na Njombe. Tumemtaka awe na sub contractors.
MUDA WA MASWALI NA MAJIBU UMEISHA HAPA LAKINI HAYANA DALILI YA KUISHA
Swali: Lini mkandarasi ataanza kufanya survey
Jibu: Itategemea na upatikanaji wa pesa lakini tumeshawaagiza TANESCO wafanye survey
Swali: Unyapaa juu ya wagonjwa wa HIV, Kwanini kuwe na milango na madirisha ya dawa tofauti kwa wagonjwa wa ukimwi na wagonjwa tofauti, Je! sio unyanyapaa?
Jibu: Serikali kupitia wizara ya afya inatoa tiba bila malipo kwa hospitali zote nchini, Natoa wito kwa wanaoishi na VVU kujiandikisha ili kupata huduma. Milango ni tofauti ili kuimarisha huduma.
Swali: Vijana na vikundi vya uporaji, serikali inaelewa tatizo
Jibu: Serikali inajitahidi kudhibiti makundi yanayoibuka, nawaomba kuwashawishi wananchi kujiepusha na watu waovu na watoe taarifa polisi.
Swali: Jeshi la polisi halina vitendea kazi
Jibu: Ni kweli Polisi wanafanya kazi katika hali ngumu kutokana na ufinyu wa bajeti, tunaiomba serikali iongeze bajeti.
Swali: Ongezeko la ujambazi wa silaha Zanzibar baada ya kuondolewa hati ya kusafiria
Jibu: Kuondosha hati ya kusafiria Zanzibar kulifanywa kisheria, tafiti za karibuni matukio hayo yamepungua
MUDA WA MASWALI NA MAJIBU UMEISHA NA WANATAMBULISHWA WAGENI HAPA
Kuna wageni nane wa Zitto Kabwe, Fulikujombe, wageni wa Wenje, mgeni wa Suzan Lymo, wageni saba wa Mashishanga, wageni kutoka Songea, wageni wa Mbumba, wageni wa Machali, Wageni wa Abood, wageni wawili wa Nchambi, Kuna wageni waliokuja kwa ajili ya mafunzo. Kuna mgeni mahsusi ambae ni mke wa David Kafulila ambae pia ni kiongozi wa CHADEMA kanda ya kati.
Yanafata matangazo ya kazi kutoka kwa Magreth Sitta kuhusu semina, Serukamba kamati ya miondominu itakua na kikao, Ardhi Lembeli anatangaza kikao, kamati ya UKIMWI kutakua na kikao Msekwa.
============================== =========
MIONGOZO
Nchambi: Kuna taarifa mahakama imepinga kujadili Escrow (anazomewa sana na mwenyekiti anaomba order kwa tabu sana na anasema kila atakaeomba muongozo leo atapewa nafasi na anatoa tishio la kusitisha bunge kama makelele yanaendelea) swala liloenda mahakani pia linamuhusisha pia mjumbe, kwa kua mjumbe huyu kamati kuu CHADEMA ameenda kuomba swala hili lisijadiliwe bungeni, CHADEMA wameonyesha wanapinga swala hili, tumjadili pia na mjumbe.
Lissu: Huyu mtu ni mwanaCCM(Wakili wa PAN Afrika), mimi nimesoma nae na ndie alieua mke wake na kesi ikafutwafutwa na mimi nimesoma nae, ni kweli anafanya kazi na Mabere Marando lakini Marando hajausika. Hoja yangu ni mara ya kwanza mahakama kuu kutoa zuio bungeni, tangia mahakama kuu ianzishwe mwaka 1922, ibara ya nne ya katiba kuhusu mgawanyo wa madaraka kwa mihimili imekiukwa(Makelele mengi na miongozo). Bunge lina uhuru wa majadiliano hivyo bunge liendelee na mjadala
Sendeka: Kutakua na uhuru wa mawazo kwenye bunge kwa mujibu wa katiba na hakutakua na chombo chochote kitachoweza kukabili ikiwemo mahakama. Nchi nzima inasubiri bunge kujadili ripoti bila ushabiki wa vyama vya siasa.
Khalifa: Tuna hofu ya nini, spika alichosema jana ilikua ruling ya bunge, tunachosubiri hapa ni ripoti tujadili
Deo: Spika alisema jana taarifa ya mahakama haipo, nadhani tuendelee kujadili bila kupoteza kwenye miongozo
Wabunge wanahitaji haki ya kujiandikisha kupiga kura
Bulaya: Niliwaambia mahakama zinatumika vibaya, waliofungua kesi ndio watuhumiwa. Mimi mbunge wa CCM siwezi kumlinda waziri, ilitwe ripoti ijadiliwe kila mtu abebe mzigo wake.
Msigwa: Tuliomba muongozo kuhusu briefing, ofisi ya spika inaendeshwa vipi
Nassari: Tunahitaji ripoti tuanze mjadala, na habari ya vyama vya siasa ikome
Lekule: Jana spika alitoa rulling bunge linaendelea, tunasubiri taarifa ya PAC wala mjadala huu haupiswi kuwepo, tunataka kujadili tufate order paper
Mwenyekiti: Miongozo yote tumeipokea, Kwenye order paper Escrow ipo na hati zimewasilishwa mezani, taarifa ya kiti bado bunge halijapokea barua yoyote kwa mjadala wa Escrow kukatazwa kujadiliwa bungeni, Miongozo nitaijibu jioni yote na kanuni inaniruhusu kutojibu papo hapo, nasitisha shughuli za bunge mpaka saa kumi na moja jioni
0 comments:
Post a Comment