Saturday, 1 November 2014

MASWAYETU BLOG TEAM INAKUTAKIENI MITIHANI MEMA KIDATO CHA NNE 2014/2015

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Jumatatu ijayo tarehe 03/11/2014 wanafunzi wa kidato cha nne wanakwenda kuanza mitihani yao ya kuhitimu kidato cha nne. Hii ni hatua muhimu sana kwenye maisha yao kwani ndio itapelekea ndoto zao nyingine kuwa kweli. Kama mwananfunzi ana ndoto ya kuwa injinia, rubani, daktari au mwalimu, mitihani hii ni muhimu kwake kufaulu ili kuweza kuendelea na masomo yako.
Hapa napenda kushauri mambo kumi kwa wnafunzi wa kidato cha nne wanaokwenda kuanza mitihani yao. Kwa yeyote anayesoma hapa fikisha ushauri huu kwa mwanafunzi unayemjua, anaweza kuwa kuwa mtoto wako, mdogo wako, ndugu au hata jirani.
1. Kwanza kabisa nitoe hongera kwa wanafunzi wote waliovumilia miaka yote minne na hatimaye sasa mnakaribia kabisa mitihani yenu ya mwisho. Sio kazi ndogo hivyo unastahili pongezi.


2. Kubuka yale uliyosoma na kufundishwa katika miaka yote minne uliyokuwa shuleni. Maswali ya mtihani yanatoka katika mambo hayo.
3. Jiamini unapokuwa kwenye chumba cha mtihani, usiwe na hofu au wasiwasi kwamba mtihani ni mgumu au utafeli. Jitahidi kadiri ya uwezo wako.
4. Wahi kufika kwenye chumba cha mtihani, jitahidi ufike nusu saa kabla ya mtihani kuanza hii itakufanya upate muda wa kutuliza akili. Ukichelewa nakukuta mtihani umeshaanza una nafasi kubwa ya kutofanya vizuri.
5. Unapopewa mtihani wako soma maswali yote kisha chagua maswali unayoweza kuanza nayo na ukayafanya vizuri. Kumbuka huwezi kufanya maswali yote kabisa kwenye mtihani, hivyo anza na yale ambayo unaweza kuyafanya vizuri. Kabla ya kujibu swali hakikisha umelielewa.
6. Ukisikia kuna habari za mtihani umevuja usijihangaishe nazo, zitakupotezea muda na kujiamini na mara nyingi ni habari za uongo. Jiamini kwa yale ambayo umefundishwa na kujisomea, yanakutosha kufaulu mtihani wako.
7. Usipanick, hata unapoona umekosea swali kata na ufanye kwa usahihi. Kukosea swali kwenye mtihani ni swala la kawaida, ila utakapopanick ndio utaharibu kila kitu. Kama umekosea swali, kata na uanze kulifanya kwa usahihi.
8. Ukitoka kwenye chumba cha mtihani msijadili maswali ya mtihani uliopita, unaweza kukata tamaa na kujiona umeshafeli. Mara nyingi baada ya mtihani utapenda kujua wenzako walijibu vipi swali fulani, bahati mbaya sana hakuna hata mmoja wenu ambaye ana jibu sahihi hivyo usisikilize maongezi ya aina hiyo.
9. Siku za mtihani hakikisha unapata usingizi wa kutosha, usikeshe kusoma, akili itashindwa kufikiria vizuri. Hakikisha unapata angalau masaa nane ya kulala na pia hakikisha unapata kifungua kinywa asubuhi kabla ya kwenda kwenye mtihani. Itafanya akili yako iweze kufikiri zaidi.
10. Mwisho kabisa nikuambie kwamba wewe ni hazina kubwa kwa nchi hii, tunakutegemea wewe kama mzalishaji na hata kiongozi wa nchi hii. Jiamini unaweza na fanya maamuzi sahihi kwenye kila hatua utakayokuwa unapitia.
Nakutakia kila la kheri katika mafanikio na ufaulu kwenye mitihani yako.
TUPO PAMOJA. 
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger