SIKU chache baada ya kukamatwa kwa
askari wa Jeshi la Polisi aliyefahamika kwa jina la Prisca Kilwai mwenye
namba WP 5367 na picha yake kudaiwa ‘kuminyiwa’ na askari wenzake ili
isionekane, hatimaye Ijumaa Wikienda limeinasa.
Mwanamama
ambaye ni askari wa Jeshi la Polisi aliyefahamika kwa jina la Prisca
Kilwai mwenye namba WP 5367 anayedaiwa kuiba mtoto wa jinsia ya kiume
aliyefahamika kwa jina la Goodluck Salehe (siku 7).
Askari huyo ambaye kituo chake ni Ilala
jijini Dar, alikamatwa kwa tuhuma za wizi wa mtoto jinsi ya kiume
aliyefahamika kwa jina la Goodluck Salehe (siku 7) aliyeibwa April 6,
mwaka huu huko Kasumulu Kata ya Itope Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya.
Ilielezwa kuwa, mtuhumiwa alishirikiana
na baba mzazi aliyefahamika kwa jina la Salehe Issah Mwangosi(31) mkazi
wa Matankini Kyela aliyemtambulisha kwa mama mzazi (Mboka Mwakikagile
umri miaka 20) kuwa Prisca ni shangazi yake hivyo amekwenda kumwona
mtoto aliyezaliwa ndipo akatoroka naye.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa Aprili 17,
mwaka huu huko eneo la Meta Jijini Mbeya majira ya saa nne asubuhi akiwa
na mtoto huyo mkononi ambapo alitiwa nguvuni na kufikishwa Makao Makuu
ya Polisi Mkoa Forest ya Zamani kwa mahojiano zaidi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, siku hiyo
mama huyo alikuwa katika harakati za kutokomea kusikojulikana lakini
bahati nzuri polisi waliimarisha ulinzi.
“Alikuwa ndiyo yupo katika mikakati ya
kutoroka na haikujulikana alikuwa anataka kwenda wapi maana tayari
alishajua kuwa anatafutwa hivyo kutapatapa na kuingia kirahisi katika
mkono wa sheria,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuhojiwa na polisi kujiridhisha
na tuhuma hizo za wizi, mstakiwa huyo alipandishwa katika mahakama
ya…na kusomewa mashtaka yanayomkabili.
Baada ya kusomewa mashtaka siku hiyo,
kesi iliahirishwa hadi Mei 6, mwaka huu ambapo mshtakiwa aliruhusiwa
kupata dhamana lakini akashindwa kutimiza masharti (wadhamini wawili na
hati) hivyo kurudishwa sero hadi kesi hiyo itakapotajwa tena.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kabla ya
kunaswa katika tukio hilo, askari huyo anayedaiwa kuwa ni mama wa
watoto, aliolewa na kuachika miaka kadhaa iliyopita.
0 comments:
Post a Comment