MSICHANA Atu Gabriel mwenye umri wa
miaka 20, mwanafunzi wa Chuo cha Eden Hill kilichopo Kwamfipa wilayani
Kibaha mkoani Pwani, amekutwa amekufa chumbani kwa mtu anayetajwa kuwa
ni hawara yake, Hafidh Mohammed.
Mwili wa Atu ukiwa chumbani kwa mtu anayesadikika kuwa ni mpenzi wake, Hafidh Mohammed.
Tukio hilo lilitokea April 26, mwaka huu
na kukusanya umati huku mwanaume aliyelala na binti huyo akitokomea
kusikojulikana.Marehemu anadaiwa kuwa mwenyeji wa Makambako mkoani
Njombe.
Akizungumza na waandishi wetu juzi
Kibaha, mama wa Hafidh ambaye pia ni mjumbe wa eneo hilo, Zainabu Saidi
alisema mwanaye alimweleza kutokea kwa tukio hilo asubuhi kulipokucha na
kabla ya hapo, hakuwa akifahamu kama alikuwa na uhusiano wa kimapenzi
na msichana huyo kwa vile aliyekuwa akimfahamu ni mwanamke mwingine
ambaye alizaa naye.
“Mimi kwa kweli sikuwa na taarifa yoyote
juu ya uhusiano wao na huyu mwanafunzi, nimeletewa taarifa asubuhi na
kijana wangu huku akionekana kuchanganyikiwa, nimejaribu kumsihi
asikimbie lakini imeshindikana,” alisema mama huyo.
ALIVYOAGA CHUONI
Wanafunzi wa chuo hicho kinachofundisha masomo ya biashara na habari ambao walikataa kutaja majina yao waliliambia gazeti hili kuwa, marehemu Atu aliwaaga anakwenda jijini Dar es Salaam kumuuguza wifi yake aliyelazwa katika Hospitali ya Amana, Aprili 23, mwaka huu.

Hata hivyo, walisema uondokaji wake
uliwapa maswali mengi kwani tofauti na walivyotegemea kuwa angebeba
mfuko mkubwa wenye nguo za kubadili, yeye aliondoka akiwa na mkoba wake
wa mkononi pekee hali iliyoonesha hakuwa akienda mbali.
Walisema siku tatu baadaye walipatwa na
mshtuko mkubwa baada ya mlinzi wa hosteli yao kuwaletea taarifa za kifo
cha mwenzao kilichotokea katika chumba cha mvulana huyo anayeishi
jirani.
MAJIRANI NAO WANENA
Majirani waliozungumza na gazeti hili walisema kwao haikuwa mara ya kwanza kumuona msichana huyo, kwani mara kwa mara alikuwa akifika pale ingawa akishaingia ndani hakuwa akitoka nje.
Majirani waliozungumza na gazeti hili walisema kwao haikuwa mara ya kwanza kumuona msichana huyo, kwani mara kwa mara alikuwa akifika pale ingawa akishaingia ndani hakuwa akitoka nje.
Walisema mara zote hizo, mwanaume huyo mwenyeji ndiye alikuwa akitoka nje na kwenda kumnunulia chakula.
POLISI WAUPELEKA MWILI HOSPITALI YA TUMBI
Jeshi la polisi liliwasili eneo la tukio na kuukuta mwili huo ukiwa umelala kitandani ukiwa hauna jeraha, lakini pembeni yake kulikutwa vidonge ambavyo havikufahamika ni vya aina gani ambavyo pia vilichukuliwa pamoja na mkoba wake hadi kituonis.

Minong’ono kutoka kwa majirani kuhusiana
na vidonge hivyo ilitofautiana, baadhi yao walisema huenda vilitumika
katika jaribio la kutoa mimba, wengine walisema inawezekana msichana
huyo alipata ugonjwa wa ghafla usiku na mwanaume huyo alikwenda
kumchukulia vidonge hivyo ambavyo havikuweza kumsaidia marehemu kupata
nafuu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, SACP
Ulrrich Matei alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema juhudi za
kumtafuta mwanaume huyo zinaendelea huku madaktari nao wakiendelea na
uchunguzi wao ili kubaini chanzo cha kifo hicho.
0 comments:
Post a Comment