KIMENUKA! RB namba
KT/RB/1178/2014-KUTISHIA KUUA KWA NJIA YA MTANDAO inamsaka staa wa Ngoma
ya Nakula Ujana, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwa tuhuma ya
kutishia kumuua mdogo wake aliyetajwa kwa jina la Amani Shija, Ijumaa
Wikienda limeinyaka.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Nay alikuwa akiishi na Shija kwa zaidi ya miaka mitano nyumbani kwake, Manzese jijini Dar.
Habari zilitonya kuwa ugomvi wa Nay na
Shija ulianza zaidi ya miezi mitatu iliyopita ambapo hivi karibuni
walikuwa maeneo ya Kijitonyama, Dar, wakipata chakula cha usiku na
marafiki zao wengine ndipo ghafla dogo akajichanganya na kujikuta
akiropoka neno lililomuudhi Nay, akapaniki.
Ilisemekana kwamba baada ya kupaniki,
Nay alianza kumfokea Shija na kutishia kumuua, ambaye alishindwa
kujizuia na kujikuta akimwaga chozi.
Alikwenda mbele zaidi na kudai kuwa Nay amekuwa akiendelea kumtishia kumuua jambo linalomfanya aishi kwa shaka mjini.
Gazeti hili lilimtafuta Nay bila
mafanikio lakini kwa mujibu wa mtu wake wa karibu, baada ya kujua msala
huo ametorokea nchini China.
-GPL
0 comments:
Post a Comment