Wednesday 7 December 2022

MAHAFALI YA KWANZA SHULE YA AWALI NA MSINGI SHADE YAFANYIKA SHINYANGA

Maandamano ya wahitimu wa darasa la awali yakiendelea kuelekea ukumbini.

Mahafali ya kwanza  katika shule ya Awali na Msingi SHADE ‘Shade English Medium Pre and Primary School’ yamefanyika ambapo jumla ya wanafunzi 17 wavulana wakiwa 8 na wasichana 9 wamehitimu shule ya awali ‘Nursery’ tayari kabisa kwa kujiandaa na masomo ya darasa la kwanza mwaka 2023 katika Shule hiyo.

Mahafali hayo yamefanyika leo jumatano Decemba 7,2022 katika shule ya Msingi Shade (Shade English Medium Pre and Primary School) iliyopo katika mtaa wa Magobeko kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Akisoma Risala, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi SHADE, Lazaro Agustino Sibale amesema shule hiyo imeanzishwa mwaka 2021 ikiwa na jumla ya wanafunzi 21 wa kike 9 na wa kiume 12 na walimu 2 katika eneo la Ushirika Mjini Shinyanga na mpaka sasa shule ina wanafunzi wengi kutokana na wazazi na walezi kuiamini shule hiyo na kuleta wanafunzi ambapo kwa sasa shule ina darasa la awali hadi darasa la pili.

Hata hivyo amesema shule ya Msingi SHADE inakabiliwa na ukosefu wa umeme ,maji pamoja na barabara mbovu ya kutoka Bugweto hadi Magobeko hasa nyakati za masika kwa kuwa na utelezi na matope mengi hivyo kukwamisha maendeleo ya shule kutokana na changamoto hizo.

“Ubovu huu wa barabara unasababisha magari kukwama na kuharibika na mbaya zaidi hali hiyo inahatarisha maisha ya wanafunzi na walimu wao kwa kuwa wakati mwingine imekuwa ikijaa maji kwenye maeneo korofi kama mvua ikinyesha kubwa kiasi cha magari kushindwa kupita”, amesema Sibale.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shade English Medium Pre and Primary School, Bw. John Isack Migila amesema lengo la kuanzishwa kwa Shule hiyo ni kutaka kutoa elimu bora na yenye kukaribia viwango vya kimataifa ikiwemo kuhakikisha mtoto anapata maarifa stahiki awapo katika mchakato wa ujifunzaji .

Amesema pia shule hiyo inatoa elimu bure kwa watoto wamakundi maalumu kama vile watoto wenye ualubino ,yatima nak.huku watoto wengine ambao wazazi wao wana uwezo wakilipa ada rafiki kwa ajili ya kuwezesha nakuendeleza kituo hicho.

Aidha amesema, katika kuhakikisha Shule inatoaelimubora wanafunzi wanalelewa kiroho bila kubagua dini maana watoto wadini zote wanapokelewa katikashule hiyo bila kujali dini zao.

Kwa upande wake afsa elimu taalumu Manispaa ya Shinyanga Wingwira Kitila ambaye alikuwa Mgeni rasmi wakati wa mahafali hayo amesema changamoto zilizo wasilishwa katika risala ya shule ataziwakilisha kwa mkurugenzi mtendaji wa Manispaa hiyo Jomary Satura ili awezekuzipatia 

Kitila ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi na walezi kulinda watoto na kufatilia maendeleo ya watotowao pindi wawapo shuleni na akiwasii kujenga utamaduni wa kuripoti matukio ya vitendo vya ukatili wanavyo fanyiwa watoto kwenye maeneo yao ili serikali iweze kuchukua hatua.
Mgeni rasmi Wingwila Kitila akizungumza na wazazi na walezi.
Mgeni rasmi Wingwila Kitila akizungumza na wazazi na walezi.
Mgeni rasmi Wingwila Kitila akizungumza na wazazi na walezi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shade English Medium Pre and Primary School,Bw. John Isack Migila akizungumza
Mkurugenzi Mtendaji wa Shade English Medium Pre and Primary School,Bw. John Isack Migila akizungumza
Maandamano ya wahitimu wa darasa la awali yakiendelea kuelekea ukumbini.
Maandamano ya wahitimu wa darasa la awali yakiendelea kuelekea ukumbini.
Maandamano ya wahitimu wa darasa la awali yakiendelea kuelekea ukumbini.
Wahitimu wakicheza pamoja na mwalimu wao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shade English Medium Pre and Primary School,Bw. John Isack Migila akijiandaa kukata utepe akiwa na wahitimu.

Mwalimu mkuu wa Shade ,mkurugenzi ,meneja wa shule pamoja na wageni waalikwa wakiwa kwenye picha ya pamoja wakiendelea na sherehe.
Baadhi ya viongozi wakifuatilia mahafali.
Share:

SAMIA, KINANA, MWINYI WACHAGULIWA KWA KISHINDO CCM, MAWAZIRI WATIKISA UJUMBE NEC

Msimamizi wa uchaguzi wa CCM, Dk Ali Mohamed Shein ambaye ni Rais mstaafu wa Zanzibar amemtangaza, Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi kwa mara nyingine baada ya kupigiwa kura za ndio 1914 kati 1915, Abdulrahman Kinana kuwa Makamu mwenyekiti wa CCM Bara baada ya kutetea nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura za ndio 1913 kati ya 1915 huku Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar,baada ya kupigiwa kura za ndio 1912.

Wakati huo huo idadi kubwa ya nafasi za wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) zimechukuliwa na mawaziri ambapowalioshinda ni pamoja na Angelah Kairuki ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Dk Ashatu Kijaji (Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezekezaji), Angelina Mabula (Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi).

Share:

YANGA SC YAJICHIMBIA KILELENI, YAIFUMUA NAMUNGO FC 2-0

NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Yanga imefanikiwa kuichapa Namungo Fc kwa mabao 2-0, mechi ambayo imepigwa katika dimba la Majaliwa mkoani Lindi.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Yannick Bangala dakika 40 na bao la pili likifungwa na Tuisila Kisinda dakika ya 83 ya mchezo.

Ushindi huo wa Yanga sc umewafanya kuwaweka nafasi nzuri ya juu wakiwa na pointi 38 akifuatiwa na Simba mwenye pointi 34.
Share:

Video Mpya : RISANDI LAIZER - MUNGU YUPO KAZINI

Mwimbaji Maarufu wa nyimbo za Injili kutoka Jijini Arusha Risandi Laizer ameachia video mpya wimbo unaitwa Mungu Yupo Kazini! 

Risandi Laizer kupitia 0766200459 au Email : rlaizer.tz108@gmail.com

TAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI

Share:

Picha : TCRA YAKUTANA NA WATOA HUDUMA ZA MAWASILIANO KANDA YA ZIWA

Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumatano Desemba 7,2022. 

Akizungumza katika Mkutano huo, Mhandisi Mihayo amesema TCRA imekuwa ikifanya mapitio ya kanuni zinazosimamia sekta ya mawasiliano mara kwa mara na hivi sasa mapitio ya Kanuni yanaendelea ambapo ada za leseni zimeshuka kwa kiasi kikubwa na kwamba TCRA inaendelea kuelekeza wamiliki wa vyombo vya habari wazingatie sheria, kanuni na miongozo iliyopo
huku akisisitiza kuwa suala la Taaluma kwa waandishi wa habari ni la kisera.

Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumatano Desemba 7,2022 katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Jijini Mwanza. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumatano Desemba 7,2022 katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Jijini Mwanza

Mtaalamu wa TEHAMA kutoka TCRA, Ibrahim Ibrahim akitoa elimu kuhusu Mfumo wa Tanzanite kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumatano Desemba 7,2022 katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Jijini Mwanza

Mhandisi mwandamizi wa TCRA Kadaya Baluhye  akizungumza kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger