Wednesday 18 May 2022

RC SOPHIA MJEMA AZINDUA CHANJO YA UGONJWA WA KUPOOZA 'POLIO' MKOA WA SHINYANGA...WATOTO 450,000 KUPEWA MATONE



Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akimpa mtoto matone ya Chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza (Polio) wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga ambapo takribani watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano  450,000 mkoani Shinyanga wanatarajiwa kufikiwa/kupatiwa chanjo ya Polio kuanzia Mei 18 hadi Mei 21,2022. Chanjo hiyo itatolewa nyumba kwa nyumba na kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watoto likiendeshwa na timu ya wataalamu 855. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akimpa mtoto matone ya Chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza (Polio) wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akimpa mtoto matone ya Chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza (Polio) wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akimpa mtoto matone ya Chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza (Polio) wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akimpa mtoto matone ya Chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza (Polio) wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akimuwekea  mtoto  alama ya kuwa amepata Chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza (Polio) wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akimuwekea  mtoto  alama ya kuwa amepata Chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza (Polio) wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Mtaalamu wa afya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga akiendelea kutoa Chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza (Polio) wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akizindua Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Mwakilishi Wizara ya  Afya, Aziz Sheshe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
 Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Afisa Ufuatiliaji wa Magonjwa ya Milipuko - Shirika la Afya Duniani (WHO) Ofisi ya Tanzania Dkt. George Kauki (kulia), Mwakilishi Wizara ya  Afya, Aziz Sheshe (katikati) na Mwakilishi wa OR- TAMISEMI, Carle Silas Lyimo (kushoto) wakiwa kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Mkazi wa Shinyanga Venance Mahona akitoa ushuhuda kuhusu umuhimu wa Chanjo ya polio kwa mtoto wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Mkazi wa Shinyanga Lighness Mnuo akitoa ushuhuda kuhusu umuhimu wa Chanjo ya polio kwa mtoto wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Mkazi wa Shinyanga Betisheba George akitoa ushuhuda kuhusu umuhimu wa Chanjo ya polio kwa mtoto wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Wazazi wakiwa kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga.

Wadau wakiwa kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga.

Wadau wakiwa kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akisalimiana  na Mwakilishi Wizara ya  Afya, Aziz Sheshe (katikati) Afisa Ufuatiliaji wa Magonjwa ya Milipuko - Shirika la Afya Duniani (WHO) Ofisi ya Tanzania Dkt. George Kauki (kulia) na Mwakilishi wa OR- TAMISEMI, Carle Silas Lyimo (kushoto) wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga.

 Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

Tuesday 17 May 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MEI 18,2022























Share:

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE CHANGARA MAKISATU


Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa maonesho haya.
Mbunifu Ashirafu Madai Selemani kutoka chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere aliyegundua mfumo wa kuwezesha magari ya dharura kubadili taa za barabarani 'Traffic Light Control for emergency Vehicle"
Mbunifu Nauriya Abbdallah Kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere aliyegundua mfumo wa kisasa wa ukusanyaji taka.

Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere leo kimeshiriki ufunguzi wa maonesho ya Wiki ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) 2022 yanayofanyika Mkoani Dodoma.

Akizungumza wakati akifungua maonesho hayo mgeni rasmi Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman amewataka watu mbalimbali wenye uwezo wa kuonesha bunifu mbalimbali kuendelea kujitokeza ili serikali ione namna itakavyowaunga mkono.

Akizungumza akiwa kwenye banda la Chuo hicho Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila amesema Chuo kimeendelea kuibua bunifu nyingi zaidi ambazo zitasaidia Serikali katika kuchangia Uchumi wa Kati wa Viwanda.

Prof. Mwakalila amesema Zaidi ya bunifu 20 zinashiriki maonesho ya Wiki ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.(MAKISATU).

Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni Ubunifu kwa Maendeleo Endelevu.


Imetolewa na:

Kitengo cha Habari na Mawasiliano

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

16.05.2022
Share:

SHAKA ASEMA UONGOZI WA RAIS SAMIA UNASIMAMIA MISINGI YA HAKI, DEMOKRASIA NA UTAWALA BORA


KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka akizungumza kwenye moja ya mikutano yake ya ndani mjini Babati,mkoani Manyara akiwa kwenye ziara yake ya kujitambulisha mbele ya wanachama wa ccm , kama mlezi mpya wa chama hicho akichukua nafasi ya Waziri mkuu mstaafu Mzee Mizengo Pinda.
Wanachama wa CCM mjini Babati wakimsikiliza Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza nao kwenye kikao cha ndani
Wanachama wa CCM mjini Babati wakifurahia jambo baada ya kumsikiliza Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza nao kwenye kikao cha ndani. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG

***

*Awahimiza watanzania kuunga mkono jududi za Serikali za kuleta maendeleo


Said Mwishehe,Michuzi TV-Manyara

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka ameendelea kuhimiza wananchi wote kuhakikisha wanashirikiana na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo na uongozi wa Rais umekuwa kinara katika kutenda haki, demokrasia na utawala bora.

Aidha amesema tangu Rais Samia ameingia madarakani amekuwa na uthubutu wa kufanya mambo makubwa kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wanakuwa na maendeleo huku akiwataka wananchi na shaka yoyote kwani Rais atawavusha salama na ataendelea kuwatumikia kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo mkubwa.

Akizungumza kwenye mikutano yake aliyofanya mkoani Manyara kwa nyakati tofauti Shaka amesema uongozi wa Rais Samia pamoja na mambo mengine ya kimaendeleo umekwenda kufungua uhuru, haki na demokrasia kwa kila mmoja wetu na lengo ni kuhakikisha wananchi wanashiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa taifa la Tanzania.

“Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara katika kuheshimu misingi yakutenda haki, demokrasia na utawala bora na tangu alipoingia madarakani ameweka mazingira mazuri ya kufanya siasa hapa nchini.

Shaka amesema wananchi hivi sasa ni mashahidi wameshuhudia vyama vya siasa na wanasiasa wakiwa huru kufanya shughuli zao za kisiasa bila kusumbuliwa tofauti na huko nyuma.“Rais Samia ametoa uhuru mkubwa kwa wanasiasa na vyama vya siasa kufanya siasa kiungwana na kuvumiliana” amesema Shaka na kuongeza

“Rais Samia tangu aingie madarakani ameshakutana mara mbili na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe lakini pamoja viongozi wengine wa upinzani.Tunaposema Rais Samia amekuwa kinara wa haki, kinara wa demokrasia na kinara wa utawala bora tunayo mifano.

“Ndio maana husikii wanasiasa wakilalamika lakini hata yale mambo ya kusikia fulani kapotea , haonekani siku hizi hayapo tena.Watu wako huru kufanya shughuli zao na wala hawasumbuli, Rais Samia nia yake ni njema kwa taifa hili hivyo ni wajibu wetu kumuunga mkono na kumpa ushirikiano.”amesema Shaka.

Pamoja na hayo Shaka amewataka wananchi wote ujumla kujiandaa kwa mambo makubwa zaidi ya kufurahisha ndani ya utawala wa Rais Samia na kwa uthubutu ambao amekuwa akiuonesha ni imani yake yajayo yanafurahisha zaidi.

Hata hivyo katika ziara yake kwenye Mkoa huo shaka ameendelea kuwakumbusha wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanaelezea mafanikikio yaliyopatikana kwenye maeneo yao kotokana na fedha wanazopewa na Serikali badala ya kukaa kimya wakati kuna mambo makubwa ya maendeleo yamefanyika.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger