Sunday 25 October 2020

WATU WAUMIZWA,MALI KUHARIBIWA KWENYE VURUGU ZA WAFUASI WA WAGOMBEA UBUNGE CCM NA CHADEMA SHINYANGA MJINI


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kujeruhi na kuharibu mali baada ya kutokea vurugu kati ya wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiandamana na wagombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini wa CCM na CHADEMA wakitoka kwenye mikutano ya Kampeni za Uchaguzi wakielekea kwenye ofisi za vyama vyao. 

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema vurugu hizo zimetokea jana Jumamosi Oktoba 24,2020 majira ya saa moja jioni. 

“Tukio hilo limetokea wakati wagombea wa nafasi ya ubunge jimbo la shinyanga mjini wa CCM na CHADEMA Shinyanga mjini wakiwa wanarudi kutoka kwenye maeneo ya kampeni zao wakielekea katika ofisi zao za vyama vya siasa walikutana katika eneo la Japanise Corner na vurugu zikaanza katika eneo hilo”,ameeleza Kamanda Magiligimba. 

“Vurugu hizo zilipelekea Hasani Tito Masanja (28), mkazi wa Majengo kujeruhiwa na kitu chenye ncha kali kidevuni akiwa na gari alilokuwa anaendesha lenye namba za usajili T. 786 BEK TOYOTA NOAH, gari ya matangazo ya mgombea ubunge CCM nalo lilivunjwa vioo vyote, pia Doto Samweli Joshua (29), mkazi wa Lubaga alivunjiwa kioo cha gari cha mbele gafi ikiwa na namba za usajili T. 444 CFA SUZUKI SWIFT, na pia Secilia Sangaluka, (42), alivunjiwa taa Indicator ya nyuma kushoto”, amesema Kamanda Magiligimba. 

Amesema Jeshi la polisi linawashilikilia watuhumiwa watano ambao ni Ramadhan Mohammed, (20), na mkazi wa Ndembezi, Yuda Kanoku, (22), mkazi wa Ibadakuli, Frank Chiza, (20), mkazi wa Kahama, Timoth Amos (20), mkazi wa Ibadakuli na Mussa Luhende, (21), mkazi wa ibadakuli ambao wanatuhumiwa kwa makosa ya kujeruhi na kuharibu mali. 

Kamanda Magiligimba amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika. 

Kamanda huyo wa polisi mkoa wa Shinyanga anatoa wito kwa wanasiasa pamoja na wafuasi wao kuacha kufanya siasa za vurugu hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi na wafanye kampeni zao kwa amani na utulivu na mara baada ya mikutano kumalizika wananchi wanatakiwa kutawanyika na siyo kufanya maandamano kuelekea kokote kule.
Share:

Angalia Picha : MAELFU WAJITOKEZA JPM AKIMWAGA SERA ZA CCM NA KUOMBA KURA BABATI MKOANI MANYARA


Siku mbili kuelekea Uchaguzi Mkuu, Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli ameendelea kuwafikia Mamilioni kwa Mamilioni ya Watanzania na Kunadi Sera, Ilani ya CCM na kuomba kura kwa Wananchi na Leo ni Zamu ya Manyara ambako amefanya Mkutano Mkubwa Babati ambao umehudhuriwa na Maelfu kwa maelfu ya wananchi
#KuraKwaMagufuli2020#T2020JPM

Share:

RPC SHINYANGA AZUNGUMZIA TUKIO LA OFISI ZA CHADEMA KUDAIWA KUNUSURIKA KUCHOMWA MOTO ....."TUNAMSHIKILIA MLINZI"


Muonekano wa vioo vya dirisha la Ofisi ya CHADEMA Kanda ya Serengeti, Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga limesema linaendelea na uchunguzi wa tukio la ofisi ya CHADEMA Kanda ya Serengeti iliyopo Majengo Mapya mjini Shinyanga kuvunjwa na watu ambao hawajafahamika usiku wa kuamkia leo Jumapili Oktoba,2020. 

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba amesema katika eneo la tukio kumekutwa chupa moja yenye ujazo wa lita 1.5 yenye kimiminika kidhaniwacho ni mafuta ya petroli ndani yake ikiwa na utambi. 

“Mnamo tarehe 25/10/2020 majira ya saa kumi alfajiri huko katika ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti zilizopo Majengo mapya, kata ya Ngokolo, Manispaa na mkoa wa Shinyanga Joseph Ndatala (43), Afisa Organization Mipango na Uchaguzi CHADEMA, mkazi wa Ndala aligundua kioo cha dirisha la ofisi ya ofisa wa organization na uchaguzi kuvunjwa na mtu/watu ambao bado hawajafahamika”,amesema Kamanda Magiligimba. 

Amesema mtuhumiwa mmoja anashikiliwa kwa mahojiano zaidi ambaye ni Edward Andrea (46), na mlinzi wa Shiroh Security Ltd. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi Katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawami amesema: 

“Leo majira ya saa saba usiku ofisi yetu ya Kanda ya Serengeti imenusurika shambulio la kuchomwa moto. Tulipewa taarifa na walinzi wetu kwamba kioo cha dirisha la ofisi ya Katibu kimevunjwa.

Na baadaye tumejaribu kuangalia labda ni vibaka walitaka kuiba lakini tulivyoingia ndani tukakutana na hali ambayo inaonesha kulikuwa na watu wenye nia ovu ya kulipua kwa petroli. Tumekuta chupa yenye mafuta ya petroli kiasi cha lita moja na nusu na utambi ndani na ukiwa umeunguzwa kidogo ikionesha kwamba huyo mtu alikuwa amewasha moto na bahati nzuri moto huo haukuwaka”,ameeleza Mnyawami. 

“Tunalishukuru sana jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa ushirikiano wa kutosha waliotupatia. Mtu wa kwanza kufika hapa baada ya sisi kutoa taarifa polisi ni OCD pamoja na askari wake. Lakini pia nimshukuru Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Shinyanga amefika eneo la tukio kujionea hali halisi. Polisi wametoa ushirikiano mzuri na mambo mengine ya Kiupelelezi tumewaachia wao”,amesema Mnyawami.

Share:

MAGUFULI AUNGURUMA MANYARA AKINADI SERA ZA CCM NA KUOMBA KURA...."VIJANA WANASEMA TUMETOBOA...NA KWELI TUMETOBOA KIMAENDELEO..TUSIKUBALI KUCHONGANISHWA"




NI MAGUFULI DAY: Siku mbili kuelekea Uchaguzi Mkuu, Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli ameendelea kuwafikia Mamilioni kwa Mamilioni ya Watanzania na Kunadi Sera, Ilani ya CCM na kuomba kura kwa Wananchi na Leo ni Zamu ya Manyara ambako amefanya Mkutano Mkubwa uliofana sana pale Babati na haya ndiyo aliyoyazungumza Kwenye Mkutano huo.
#KuraKwaMagufuli2020#T2020JPM

Waziri Mkuu mstaafu Mzee Fedrick Sumaye akizungumza nakumuombea kura mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
Waziri Mkuu mstaafu Mzee Fedrick Sumaye akiwa ameketi na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Rodrick Mpogolo wakishiriki katika mkutano huo wa kampeni uliofanyika mjini babati. 
Picha mbalimbali zikionesha maelfu ya wananchi wakiwa wanamsikiliza mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dk. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi hao kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati.
Share:

Majaliwa: Serikali Hainunui Korosho, Inasadia Upatikanaji Wa Masoko


MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amesema Serikali hainunui korosho wala mazao mengine bali inaweka mazingira mazuri ya upatikanaji wa masoko.

“Serikali hainunui korosho, Serikali hainunui pamba, wala hainunui chai au kahawa. Kazi ya Serikali ni kutengeneza fursa ili wanunuzi waje. Mtu asitumie zao la korosho ili kujipatia umaarufu wa kisiasa,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Oktoba 25, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa kata za Likongowele na Kibutuka wilayani Liwale ambako alienda kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo la Liwale, Bw. Zuberi Kuchauka na madiwani 20 wa kata za jimbo hilo.

“Mwaka 2018, kuna wafanyabiashara waliungana na wakagomea kununua korosho kwa sh. 1,800. Rais Dkt. Magufuli akasema hakuna kununua korosho za wakulima kwa bei hiyo, ndipo akatoa sh. bilioni 900 ili zitumike kununua korosho kwa bei isiyopungua sh. 3,000 kwa kilo.”

“Fedha hizo zimetumika kuwalipa wakulima, wasafirishaji, wenye magunia, kulipia usimamizi wa maghala na sasa imebakia kuwalipa Halmashauri ambao wanadai ushuru wa asilimia 5, na hao ni Serikali wenzetu kwa hiyo watalipwa tu. Kama kuna wakulima waliobakia ni mmoja mmoja sana, hao wanafuatiliwa na Wizara husika.”

Amesema korosho siyo zao pekee lililoathiriwa na kuporomoka kwa bei bali mazao mengine kama pamba, chai, kahawa na tumbaku nayo yameathiriwa na kushuka kwa bei mwaka huu.

“Korosho ni miongoni mwa mazao ya kimkakati nchini yaliyokosa soko msimu uliopita baada ya mataifa ya Ulaya kufunga mipaka yao kutokana na ugonjwa wa corona na hivyo wanunuzi hawawezi kuja nchini.”

“Korosho, pamba, tumbaku, chai na kahawa hayakuwa na bei nzuri kutokana na corona si vinginevyo. Serikali hainunui mazao, kazi yake ni kutengeneza mazingira mazuri ya soko asije mtu akawadanganya na kutumia bei za mazao ili apande chati kisiasa,” alionya.

Akitoa mfano, Mheshimiwa Majaliwa amesema: “Bei ya pamba imeshuka kutoka sh. 1, 200 hadi sh. 800 kwa kilo; kahawa imeshuka kutoka sh. 1,800 has sh. 1,200 kwa kilo, na tumbaku imeshuka kutoka sh. 1,700 hadi sh. 1,400.”

“Wanunuzi wakubwa wa korosho wanatoka China, Singapore, Vietnam na India. Hawa wenzetu sasa hivi bado wameelemewa na ugonjwa huu, hawawezi kutoka na kusafiri. Tuwaombee nchi zao ziondokane na corona ili na sisi tuweze kufanya biashara na nchi nyingine,” alisisitiza.

(mwisho)


Share:

Sekta ya mawasiliano ya simu ilivyo nguzo muhimu kuleta mabadiliko ya kiuchumi Tanzania


Dunia inaendelea kushuhudia maabadiliko makubwa ya kiteknolojia sehemu mbali mbali kwa kasi ya ajabu. Sehemu kubwa ya matunda ya teknolojia mfano matumizi ya simu mkononi ambayo yapo sasa, yasingeweza hata kufikirika mwanzoni mwa karne ya 21.

Ukweli usiopingika ni kwamba, kadiri maendeleo ya teknolojia yanavyozidi kupanuka, ndivyo matumizi ya mtandao wa intaneti yatakavyoongezeka. Kwa mfano, takwimu zilizotolewa na Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo zinaonesha kuwa matumizi ya data yameongezeka toka 46,000GB kwa sekunde mwaka 2017 na yatafikia 150,700 GB kwa sekunde mwaka 2022.

Vijana wanatajwa kuwa kundi lililo katika nafasi ya kunufaika zaidi na maendeleo haya ya kiteknolojia kutokana na uharaka wao katika kuweza kuitumia teknolojia.

Tanzania kama ilivyo nchi nyingine nayo inaendelea kunufaika na maendeleo haya ya kiteknolojia yanayoshamiri kote duniani. Tanzania imeshuhudia mabadiliko makubwa ya kidijitali huku watu wakitumia fursa hiyo kukuza biashara zao na kuendesha maisha.  

Kwa mfano, katika robo ya pili ya mwaka huu wa 2020, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kuwa matumizi ya jumla ya fedha kwa njia ya simu yameendelea kuongezeka ambapo jumla ya akaunti zilizosajiliwa kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu zimeongezeka kutoka milioni 27 mwezi Aprili hadi milioni 29 milioni mwishoni mwa Juni.
Ukuaji huu wa huduma ya fedha kwa njia ya simu umekuwa muhimu sana kwa namna ambavyo watu wanatumia na kuhifadhi fedha zao.

Maendeleo haya yote yanatokana na jitihada zilizofanywa kuwekeza katika sekta hii na wadau mbalimbali. Mfano mzuri ni Tigo Tanzania ambapo huduma ya fedha ya Tigo (Tigo Pesa) imewapatia wateja wake huduma yenye kasi na njia ya kuaminika ya kuweka na kutoa/kutuma fedha, pamoja na faida nyingine lukuki za kuingia katika mfumo rasmi wa kifedha bila urasimu.
 
Ama kwa hakika, sekta hii ya mawasiliano ya simu Tanzania imeonesha kuwa ina uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika nchi kupitia teknolojia.

Tukiwa tunafurahia na kutumia matunda ya sekta hii, tuendelee kuunga mkono sekta kwa kuendelea kuwa na sera rafiki na bora ili sekta hii izidi kukua na kuleta tija zaidi kwenye jamii na uchumi wa Tanzania kwa ujumala.


Share:

IGP Sirro aonya vikundi vilivyopanga kufanya vurugu Arusha.


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro amesema jeshi lake limepata taarifa za kuwepo kwa baadhi ya vikundi vichache katika Jiji la Arusha vyenye nia ya kuharibu amani siku ya uchaguzi na kutoa onyo kali kwe wote wenye mpango huo.

IGP Sirro ametoa kauli hiyo Jijini Arusha baada ya kuzungumza na askari polisi zaidi ya 700 watakaosimamia mchakato wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika nchini kote Jumatano ijayo.

Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi pia ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wa Mkoa wa Arusha kuendelea kuimarsha amani na utulivu siku hiyo ya uchaguzi.


Share:

HAYA NDIYO ALIYOYAZUNGUMZA MAJALIWA AKINADI JPM LEO MKOANI LINDI


 Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Ndugu Kassim Majaliwa ameendelea na Mikutano yake ya Kampeni Kunadi Sera na Ilani ya CCM Kisha kuomba kura. Na Leo Jumapili amefanya Mkutano Mkubwa wa Kampeni Wilayani Liwale Mkoani Lindi na haya ndiyo aliyoyazungumza Kwenye Mkutano huo Mkubwa. Liwale inasema ilikosea na Sasa wametubu, Oktoba 28 wanaenda na CCM tu kwa maendeleo na si ubabaishaji tena.

#KuraKwaMagufuli2020#T2020JPM
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger