Wednesday 27 May 2020

Mabasi Ya Mwendokasi Yaagizwa kurejesha huduma ya usafiri kama kawaida Kabla ya June 01

Waziri wa Nchi , ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI) Selemani Jafo amemuagiza wakala wa mabasi yaendayo haraka UDART kuhakikisha usafiri wa mabasi hayo unarejea kama kawaida kabla ya Juni Mosi, mwaka huu na kuondoa kero ya sasa inayowakumba abiria wanaotumia usafiri huo.

Selemani Jafo amesema kuwa kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na msongamano mkubwa wa abiria kwenye vituo vya mabasi hayo kutokana na watu wengi kuanza kurejea kwenye shughuli zao mbalimbali kufuatia kupungua kwa ugonjwa wa corona.

“Ni kweli, baada ya Rais wetu, Dk John Pombe Magufuli kueleza matumaini makubwa ya idadi ya maambukizi kupungua nchini, watu wamerejea kwa kasi katika shughuli za kiuchumi, hii imechangia msongamano pale Kimara nyakati za asubuhi hasa tukikumbuka pia kuwa ni ‘level seat’,” amesema Jafo akizungumza na gazeti la Habarileo.

Jafo amesema kuwa wasimamizi wa mradi huo wamemueleza kuwa mbali na idadi ya watu kuongezeka, lakini idadi ya magari yanayotoa hudumu nayo imepungua, kwani mabasi marefu 30 yapo katika matengenezo.

Aidha, ameagiza magari hayo kufanyiwa matengenezo haraka, kwani kutokana na maisha kuanza kurudi katika hali kawaida, na vyuo kufunguliwa, usafiri huo utahitajika sana kuhakikisha watu wanawahi kwenye shughuli zao.


Share:

Rais Donald Trump wa Marekani Akosolewa na Mtandao wa Twitter Baada Ya Kutoa Ujumbe wa Upotoshaji

Mtandao wa kijamii Twitter umemkosoa Rais Donald Trump wa Marekani kwa kuchapisha katika mtandao huo wa kijamii taarifa za kupotosha kuhusu uchaguzi mkuu ujao wa nchi hiyo.

Twitter imesema ujumbe wa Trump kwamba kufanyika uchaguzi wa Novemba mwaka huu kwa njia ya kutuma baruapepe kutasababisha uchakachuaji wa matokeo; hauna ukweli wowote. 

Trump anadai kuwa hizo ni njama za chama cha Democrats za kuiba kura katika uchaguzi huo.

Mwanasiasa huyo wa Repulican ameutishia na kuukosoa mtandao huo wa kijamii kwa kuuainisha ujumbe wake huo kuwa wa upotoshaji, na kuandika: Twitter inabinya kabisa uhuru wa kujieleza, na mimi kama Rais, sitokubali hilo lifanyike.

Trump amekuwa akiutumia mtandao huo wa kijamii kama jukwaa lake kuu la kutoa taarifa rasmi na zisizo rasmi, na hata kuwakebehi na kuwakejeli wapinzani na wakosoaji wake.


Share:

Mkutano Wa Baraza La Mawaziri Wa Sadc Ngazi Ya Makatibu Wakuu Wafanyika Kwa Nia Ya Mtandao

Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umefanyika leo jijini Dar es Salaam kwa njia ya Mtandao (Video Conferencing) katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) 
 
Mkutano huo umefunguliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Maafisa Waandamizi/ Makatibu Wakuu, Balozi Kanali Wilbert Ibuge Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 
Wajumbe wengine ni waliohudhuria ni Katibu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Prof. Abel Makubi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utaii Dkt. Aloyce Nzuki pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipago, Bi Amina K. Shaaban.
 
Mkutano wa Baraza la Mawaziri utafanyika Mei 29, 2020 baada ya kukamilika kwa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Maafisa Waandamizi/Makatibu Wakuu ambapo pamoja na mambo menine, Kikao cha Maafisa waandamizi kimejadili masuala mbalimbali ndani ya Jumuiya ikiwemo Mlipuko wa Virusi vya Corona ndani ya SADC.
 
Mkutano huo utaangalia utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri kilichofanyika mwezi Aprili 2020 kuhusu COVID 19 na athari zake katika utekelezaji wa programu za SADC, athari za kijamii na kiuchumi za COVID -19 na madhara yake ndani ya Jumuiya.
 
Aidha, Mkutano huu pia umejadili Hali ya kifedha ndani ya Jumuiya, Utekelezaji wa Maazimio yaliyotokana na kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC ambayo ni Menejimenti ya Maafa, utekelezaji wa kaulimbiu ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC isemayo "Mazingira Wezeshi kwa ajili ya Maendeleo Endelevu na Jumuishi ya Viwanda, Kukuza Biashara na Ajira ndani ya SADC" na mapitio ya hali halisi ya biashara baina ya nchi, maendeleo ya viwanda ndani ya Jumuiya na taarifa ya utekelezaji wa Mkakati wa Maendeleo ya Viwanda wa Jumuiya na Mpango kazi wake.
 
Mkutano huo umehusisha wataalamu kutoka nchi  wanachama 12 wa SADC kutoka sekta za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Fedha na Mipango, Uchukuzi na Mawasiliano, Viwanda na Biashara, Maliasili na Utalii pamoja na Afya.
 
Nchi zilizoshiriki Mkutano huo ni Angola, Afrika Kusini, Comoro, Eswatini, Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia, Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Zimbabwe na Mwenyekiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Share:

Mashitaka Mawili Yanayowakabili Idris Sultan na Mwenzake

Msanii wa vichekesho, Idris Sultan, na mwenzake, Innocent Maiga wamefikishwa katika Mahakama ya Kisutu leo Mei 27, 2020, na kusomewa mashtaka yanayowakabili likiwemo la kumiliki laini ya simu ya Maiga na kushindwa kuripoti mabadiliko ya umiliki wa laini hiyo.

Washitakiwa wamesomewa mashitaka yao na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, Matilda Mushi na Estazia Wilson mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu. Kosa la kwanza la kushindwa kufanya usajili wa simu wa kadi iliyokuwa inamilikiwa na mtu mwingine linamkabili Idris Sultan.

Katika kesi hiyo ya jinai, inadaiwa ametenda kosa hilo kati ya Desemba 1, 2019 na Mei 19, 2020, maeneo ya Mbezi Beach Kinondoni ambapo alitumia kadi ya simu iliyomilikiwa na Innocent Maiga bila kuripoti kwa mtoa leseni.

Kosa jingine ni kushindwa kutoa taarifa ya mabadiliko ya kadi ya simu ambapo linamkabili Innocent Maiga ambaye anadaiwa amelitenda Desemba 1, 2019 na Mei 19, 2020 Mbezi Beach Kinondoni ambapo ni kinyume na sheria kwani alishindwa kutoa taarifa ya mabadiliko ya namba ya simu kama inatumiwa na Idris Sultan.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, washitakiwa walikana makosa yao, ambapo upelelezi wa kesi hiyo umekamilika. Hata hivyo, washitakiwa hao wameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili waliosaini bondi ya Sh. mil. 15 kila mmoja.

Hata hivyo, Wakili wa Idris Sultan, Benedict Ishabakaki, ameondolewa kumwakilisha mshitakiwa huyo kwa sababu atatumika kama sehemu ya ushahidi wa upande wa Jamhuri kutokana na kushuhudia mshitakiwa wake akichukuliwa maelezo polisi, hivyo anabakia wakili mmoja ambaye ni Jebrah Kambole.


Share:

OPPORTUNITIES FOR INTERNSHIP PROGRAM at Tanzania Bureau of Standards (TBS)

OPPORTUNITIES FOR INTERNSHIP PROGRAM at Tanzania Bureau of Standards (TBS) OPPORTUNITIES FOR INTERNSHIP PROGRAM Tanzania Bureau of Standards (TBS) is Tanzania’s sole Standards body, formerly established by the Standards Act No. 3 of 1975, which was repealed and replaced by the Standards Act No. 2 of 2009. It is a Parastatal Organization under the Ministry of Industry and… Read More »

The post OPPORTUNITIES FOR INTERNSHIP PROGRAM at Tanzania Bureau of Standards (TBS) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Msanii Idris Sultan Afikishwa Mahakamani

Msanii Idris Sultan  amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa mashtaka yanayomkabili baada ya kushikiliwa na Polisi kwa takriban siku nane. 

Katika viunga vya mahakama hiyo ameonekana mwanasheria wa msanii huyo, Benedict Ishabakakiba, baba yake Idris na watu wengine

Tutaendelea kukujuza


Share:

Tafiti Katika Vyuo Vya Kilimo Kutimiza Adhma Ya Uchumi Wa Viwanda

Na Ismail Ngayonga-MAELEZO
SEKTA ya Kilimo nchini imeendelea kuwa ni Sekta muhimu katika maendeleo ya uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla hususan katika wakati huu tunapojizatiti kufikia uchumi wa viwanda.
 
Katika  kipindi  cha  miaka mitano, Pato la Taifa linalotokana na kilimo, kwa kutumia  bei  za  Mwaka  2015  limeongezeka  kwa asilimia 17 kutoka Tsh. Trilioni 25.2 Mwaka 2015 hadi Tsh. Trilioni 29.5 Mwaka 2019.
 
Vilevile, sekta imeendelea kutoa ajira kwa Watanzania kwa asilimia 58 Mwaka 2018 na kuchangia asilimia 28.2 ya Pato la Taifa huku sekta ndogo ya mazao ikichangia asilimia 16.2 na hiyo imetokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zikiwemo vyakula vinavyotokana na mazao ya kilimo.
 
Ili kufikia kiwango malengo makubwa ya uzalishaji wa mazao, Sera zinazoongoza utafiti zina mchango mkubwa katika kupanga maendeleo ya sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na ya kuboreshea viwango vya maisha ya wananchi kwa kuchochea ukuaji na kuongeza tija katika sekta muhimu za uzalishaji za uchumi wa taifa.
 
Historia inaonyesha kuwa nchi zilizozingatia sera zenye mwelekeo wa utafiti thabiti zimefanikiwa kujenga uchumi wenye ushindani kwa kutumia rasilimali walizonazo, na kuziendeleza kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi wao.
 
Katika jitihada hizo, Serikali kupitia Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) imeendelea kuboresha uzalishaji wa mazao ya kilimo, mifugo, misitu na uvuvi katika eneo la Tafiti na Ushauri elekezi ili kutoa huduma ya elimu ya ushauri wa kitaalamu kwa wakulima.
 
Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2020/2021, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako anasema Serikali kupitia SUA imeendelea na miradi mipya 13 ya utafiti yenye lengo la kuboresha uzalishaji wa mazao ya kilimo, mifugo, misitu na uvuvi  ili kuwezesha wananchi kuzalisha mali na malighafi za mazao ya kilimo kwa ajili ya viwanda.
 
Prof. Ndalichako anasema Chuo hicho pia kimeweza huduma ya elimu ya ushauri wa kitaalamu kwa wakulima 9,500 kwa kutumia vituo atamizi, mashamba darasa, semina, kozi fupi, runinga na redio kwa lengo la kuongeza uzalishaji wenye tija na kupunguza umaskini kwa wananchi.
 
‘Mafunzo hayo yametolewa kwa wakulima katika mikoa ya Mwanza, Dar es Salaam, Iringa, Dodoma, Tabora, Tanga, Pwani na Morogoro kwa lengo la kutoa elimu kuhusu kilimo na ufugaji’’ anasema Prof. Ndalichako.
 
Aidha Prof. Ndalichako anasema SUA pia ) imepima jumla ya sampuli 1,553 zikiwemo sampuli za udongo 1,180, za mimea 297, za mbolea za viwandani 20, za samadi tisa (9) na sampuli za maji 47 kutoka kwa watafiti mashirika ya kilimo, Viwanda na Taasisi mbalimbali pamoja na wakulima binafsi.
 
Waziri Ndalichako anasema kuwa Serikali imeingia mikataba mipya 13 ya mahusiano na Taasisi nyingine za ndani na nje ya nchi ili kuwajengea uwezo wafanyakazi na wanafunzi katika kufanya tafiti za kisayansi na kilimo kwa lengo la kuongeza uzalishaji wenye tija katika shughuli mbalimbali za maendeleo kwa wananchi.
 
Anazitaja taasisi hizo kuwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Sophia kilichopo Japan; National Institute of Health - Korea; Foundation Pierre Fabre - France; Kunming Institute of Zoology,  Chinese Academy of Science; Silverlands Tanzania Limited - Iringa, Tanzania; College of Animal Science and Technology Nanjing Agricultural University - China; Agronomos Sin Fronteras Foundation (ASFF ) - Iringa Tanzania; University of Leeds – UK; na Wuhan University (WHU) – China.
 
Akifafanua zaidi Prof. Ndalichako anasema katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia Serikali imejenga jengo lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,400 kwa wakati mmoja litakalokuwa na maabara nane zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 100 kila moja.
Prof. Ndalichako anasema Serikali pia imekamilisha ujenzi wa jengo la utafiti wa wanyama na wadudu kwa ufadhili wa mradi wa Eastern and Southern Africa Centers of Excellence for Innovative Rodent Pest Management and Biosensor Technology Development (ACE II, IRPM and BTD) na kuendelea na ukarabati wa madarasa likiwemo jengo la Hay Building kwa lengo la kuongeza nafasi za kufundishia na kujifunzia.
Mazao ya Kilimo ni malighafi muhimu sana katika viwanda, hivyo ni utafiti ni nguzo muhimu sana inayoweza kuleta kuleta ubunifu wa bidhaa, uboreshaji wa bidhaa, kuongeza ufanisi wa huduma, tija na ubora wa utendaji katika soko.

MWISHO



Share:

NHIF TANGA YAKABIDHI MASHUKA 50 KWA WILAYA YA PANGANI

MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akimkabidhi Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Seif Ally mashuka yaliyotolewa na mfuko huo kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya wilaya katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella halfa hiyo ilifanyika mjini Pangani
 MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akimkabidhi Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Seif Ally mashuka yaliyotolewa na mfuko huo kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya wilaya katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella halfa hiyo ilifanyika mjini Pangan
 MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akizungumza mara baada ya kukabidhi mashuka hayo katika anayemsikiliza ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella  na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Seif Ally
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akizungumza mara baada ya kukabidhi mashuka hayo katika anayesimamia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kushoto ni  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella 
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) umekabidhi mashuka 50 kwa ajili ya vituo vya kutoka huduma ya Afya wilayani Pangani ikiwa ni kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa bora kwa wagonjwa wanapokwenda kupata matibabu kwenye maeneo hayo

Makabidhiano hayo yalifanywa na Meneja wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Seif Ally katika halfa iliyoshuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Meneja Mwakababu alisema wamemkabidhi Mwenyekiti huyo kwa ajili ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Isaya Mbenje na vituo vya afya vinavyotoa huduma ya afya wilayani Pangani wakiwa na dhamira ya bima ya afya ni kuhakikisha huduma zinakuwa bora.

Alisema ili pia lengo kubwa ni kuhakikisha wagonjwa wanapokwenda kupata huduma wakute mahali safi na salama ambayo yawawawezesha kupata matibabu kwenye mazingira mazuri yanayovutia.

“Kama mnavyojua NHIF tunajua Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ni mdau wetu mkubwa na Pangani ni eneo lake NHIF ikaona tumsapoti kwa upande wa afya kwamba anapopambana na maji kuhakikisha maji yanapatikana lakini pia kuhakikisha mazingira ya wananchi kwenye kupata huduma yaweze kuwa salama”Alisema Meneja huyo.


 Hata hivyo alisema kwamba wataendelea kushirikiana na wadu wengine katika kuhakikisha huduma za bima ya afya zinaboreka huku akieleza kwamba wanataka wananchi wakifika kwenye maeneo ya kupata matibabu waweze kuona namna yalivyokuwa mazuri na safi wakati wote.
Share:

Mkemia Fidelis Segumba atoa ushahidi kesi ya Shamim Mwasha na mumewe

Mkemia, Fidelis Segumba amedai mahakamani kwamba katika bahasha tano alizochunguza katika kesi ya Shamim Mwasha na mumewe, mbili zimebainika kuwa ni dawa za kulevya aina ya heroine.

Segumba ambaye ni mkemia daraja la kwanza na shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, alidai hayo jana Mahakama Kuu Kitengo cha Rushwa na Uhujumu Uchumi mbele ya Jaji Elinaza Luvanda, wakati akitoa ushahidi kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula.

Mstakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Abdul Nsembo ambapo wanadaiwa Mei mosi mwaka 2019 walikutwa na dawa za kulevya nyumbani maeneo ya Mbezi Beach.

Jana Segumba akitoa ushahidi wake alidai alikabidhiwa bahasha tano na ofisa kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Suleiman Juma Mei 2 mwaka jana.

Alidai bahasha hizo zilipewa majina A ikiwa na gramu za unga 232.70, B unga gramu 68.52, C gramu 8.27, D gramu 42.70 na E gramu 7.

Anadai katika uchunguzi alibaini bahasha A na D zilikuwa na unga wa dawa za kulevya aina ya heroine wakati bahasha zingine tatu hazikuwa na dawa za kulevya.

Alidai, heroin husababisha ulevi usioponeka kirahisi, ulemavu wa akili na ipo katika orodha ya kwanza ya dawa zenye sumu.

“Bahasha A kulikuwa na unga uliofungwa kwenye kitambaa cheupe kilichofungwa na nailoni angavu ndani kulikuwa na unga mweupe, bahasha B hadi E ndani kulikuwa na kikopo kilichokuwa na unga, baada ya kusajili bahasaha hizo ndipo nilipoanza uchunguzi,”alidai.

Alidai baada ya kumaliza uchunguzi aliandika ripoti na kuisaini ambapo aliiomba mahakama iipokee ripoti hiyo kama kielelezo.

Hata hivyo mawakili wa utetezi walipinga ombi hilo kwa madai kuwa shahidi hakufata sheria ya kuwasilisha kielelezo hicho mahakamani kwani ripoti hiyo haikuwa chini ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali bali alipewaa mwendesha mashtaka mahakamani.

Mawakili hao ni Juma Nassoro, Josephat Mabula na Hajra  Mungula.

Akijibu Wakili Kakula alidai hoja hizo zimewasilishwa mapema kabla ya muda, walipaswa kusubiri hadi shahidi wa mwisho hivyo alidai hazina mashiko zitupwe.

Hata hivyo mahakama ilitupilia mbali pingamizi hilo na kupokea ripoti hiyo kama kielelezo namba moja baada ya kukubaliana na hoja za upande wa mashtaka kwamba hoja ziliwasilishwa mapema kabla ya muda wake.


Share:

Jeshi La Polisi Mkoani Dodoma Lakamata Magari 17 Ya Wizi

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limekamata magari 17 yadhaniwayo kuwa ya wizi katika msako wa siku nne uliofanyika kati ya tarehe 19.5.2020 hadi tarehe 22.5 2020.

Hayo yamesemwa  Mei 26,2020   na  kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa walimkamata Helman Stephen akiwa na gari namba T.891 BXY Toyota PREMIO gari ambalo linatumia kadi na usajili wa kubatizwa za gari lingine huku akisema kuwa walimkamata Athuman Juma Pambagu mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa Nzuguni mwenye gari  namba T.864 CQA TOYOTA IST  chassis imekatwa na kuungwa kibati kiingine vioo vimefutwa na kubandikwa namba nyingine ambalo limebatizwa namba na card ya gari nyingine.

Aidha amesema kuwa wamekamata gari lenye namba ya T.237 DSJ aina ya SUBARU ni gari la transit {IT} lilikuwa linasafirishwa kwenda Uganda ambalo dereva alipakia abiria wawili huko MISUGUSUGU Pwani kwenda Kahama Shinyanga ambapo dereva alitishiwa silaha na kuporwa gari na kufungwa kamba na kutupwa porini eneo la Pandambili kongwa .

Sanajari na hayo Kamanda  Muroto amesema kuwa walimkamata Festo Castory Lalika akiwa na vifaa vya pikipiki 4, jenereta mbili  na engine moja ya bajaji huku pia akikamatwa Lello Michael Ringo akiwa na Tv 3 aina ya SAMSUNG,SUBWOFER 1 Vichwa vya cherehani 2,laptop 1 HP Stabilizer 2 ambazo ni mali  za wizi na vifaa vya kuvunjia drill 1 na  panga .

Hivyo amesisitiza watu  waache kujihusisha na uhalifu wa aina yoyote ikiwa ni pamoja na wizi , na magari ya wizi wayasalimishe haraka  katika kituo cha polisi kabla ya kukamatwa huku akiwashauri watu ambao wananunua magari wahakikishe wanayakagua magari hayo kabla ya kununua ili wasiingie katika matatizo ya kumiliki chombo cha  wizi.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MEI 27,2020


Share:

Tuesday 26 May 2020

Mwanamke Ajitosa Kuwania Urais Kupitia CHADEMA

Dk. Mayrose Majinge, amekuwa mwanachama wa kwanza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza jana, Dk. Mayrose alisema kuwa lengo la kuwania nafasi hiyo ni kutaka kuona Tanzania inakuwa taifa imara lenye watu wenye afya bora na wenye uhuru kamili.

Alisema tangu mwaka 2005 alianza harakati hizo akiwa miongoni mwa watia nia kuwania nafasi ya kugombea ubunge wa Jimbo la Ukonga, kabla halijagawanywa na kuwa majimbo mawili (Segerea na Ukonga), lakini kura hazikutosha jambo ambalo alidai limempa uzoefu mkubwa wa kisiasa.

“Nilipata uzoefu mwingine wakati nilipowania nafasi ya ubunge Bunge la kwanza la Afrika Mashariki, ndiyo maana  kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 na 2015 sikuonekana  katika ulingo tena, siyo kama niliacha kwa kutopenda ubunge, bali niliamua kujikita katika maandalizi ya kuwania nafasi ya juu ya uongozi wa nchi,” alisema Dk. Mayrose.

Alisema uongozi ni dhamana, ni lazima watu wakujue na kukuamini kwa kujitolea kusaidia katika nyanja mbalimbali ili waweze kukupa dhamana ya kuongoza nchi.

Dk. Mayrose alisema mwaka 2014/2019 alifanya kazi kubwa ya kuzuru nchi mbalimbali duniani kwa lengo la kujenga uhusiano wa kimataifa.

Alisema katika masuala ya diplomasia pia ameshiriki mijadala ya nchi zaidi 51 duniani iliyomsaidia kupata taarifa na uzoefu kuhusu masuala ya utawala bora, haki na usalama wa raia.

“Nimeamua kwenda nje na kuwaacha watoto wangu wanne na mume wangu ili kukisaidia chama changu kupata uzoefu katika uwendeshaji wa vyombo vya maamuzi, utungaji wa sera na shughuli za siasa kwa vyama vya siasa ndani ya jamii kutoka kwa mataifa yaliyoendelea.

“Uwezo wa kuongoza ninao. Ili tuondokane na umaskini ni lazima jitihada za makusudi za kushughulikia upatikanaji na utumiaji wa silaha sahihi (siasa safi) zitiliwe mkazo,.

“Ni vema tutambue kuwa siasa safi ni nguzo ya uongozi bora ambayo ni chachu ya maendeleo endelevu,” alisema Dk. Mayrose.

Alisema Chadema inaamini kuwa kanuni miongozo pamoja na katiba ya chama hicho vinatoa haki kwa mwanachama yeyote mwenye sifa kuwania nafasi ya uongozi wa dola ikiwamo urais.

Dk. Mayrose alisema kuwa amejipima na kuona kwa hakika anatosha kuwa mwakilishi sahihi kama chama kitamteua kuwania nafasi hiyo ili aweze kupambana na wagombea wa vyama vingine.


Share:

WATANZANIA WALIOKWAMA AFRIKA KUSINI KWA LOCKDOWN WAREJEA NYUMBANI


Na Mwandishi Maalumu
Balozi wa Tanzania nchini Afrka Kusini Meja Jenerali (Mst) Gaudence Milanzi Jumatatu Mei 25, 2020 amesimamia zoezi la repatriation (usafirishaji) wa dharura) ya Watanzania pamoja na raia kadhaa wa nchi hiyo waliokwama kutokana na Lockdown na kusitishwa safari za ndege inayoendelea huko, kutoka Johannesburg kuja Dar es salaam.


Taarifa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini humo zinasema kwamba Balozi Milanzi aliratibu na kusimamia zoezi hilo ambapo Watanzania 14 ambao walikwama nchini humo kwa miezi miwili kufuatia Lockdown hiyo.

Raia 12 wa Afrika Kusini pamoja nna raia mmjoa wa Uingereza nao wakajiunga kwenya msafara huo baada ya kuona ni afadhali warejee Tanzania ambako hakuna Lockdown ili kuendelea kufanya kazi kwenye makampuni na taasisi za nchi hiyo.


Akiwasindikiza abiria hao walioondoka kwa ndege ya kukodi ya kampuni ya AS SALAAM AIR ya Zanzibar, Balozi Milanzi aliwapa pole kwa kuwa katika Lockdown ya miezi miwili na kuwatakia safari njema na maisha ya furaha watakapowasili Tanzania ambayo ni nchi pekee ambayo imekuwa namsimamo thabiti wa kupambana na gonjwa la COVID 19 lililosababisha nchi zingine kufungia kila mtu ndani.

Hili ni tukio la tatu la repatriation tokea gonjwa hilo liikumbe dunia
 na kusababisha sintofahamu kila pembe, kufuatia zile safari za India na Falme za Kiarabu ambapo serikali ilituma ndege maalumu kwenda kuchukua wananchi wake waliokwama huko kutokana na Lockdown katika nchi hizo.

Zoezi hilo limekuja wakati Tanzania imefungua rasmi anga lake na
kuruhusu utalii pamoja na safari za ndege za kimataifa viendelee kama kawaida, ambapo tayari mamia ya watalii wameendelea kumimimika nchini, huku wengine wakitarajiwa kuwasili kwa wingi baada ya mashirika ya ndege ya kimataifa kuanzisha safari zao.













Share:

Uteuzi Mpya Wizara Ya Maji




Share:

Maafisa wawili wa TRA Manyara wadakwa na TAKUKURU kwa kumuomba Mteja wao Rushwa ya Milioni kumi

Na John Walter-Manyara
Mkuu  wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoa wa Manyara (TAKUKURU) Holle Mkungu, amesema wanatarajia kuwafikisha katika Mahakama ya hakimu mkazi Manyara, maafisa wawili wa TRA mkoani hapa kwa makosa ya kudai na kupokea Rushwa ya shilingi Milioni kumi.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Subilaga Mwangama na Ojungu Mollel,  na kwamba  makosa hayo ni kinyume cha kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa namba 11/2007.

 Akizungumza na  waandishi wa habari  ofisini kwake,  amesema kuwa Uchunguzi wa Takukuru  ulibaini kwamba mlalamikaji  (jina linahifadhiwa kwa sababu kwa za kiusalama)  ni mlipakodi mzuri kwa mamlaka ya mapato  kituo cha  wilaya ya Mbulu ambapo kwa kipindi  cha mwaka 2018 alilipa kodi zaidi ya million 9.

Hata hivyo mwezi machi 2020  mlalamikaji alipigiwa simu na washtakiwa  hao wakimtaka  afike ofisi za mamlaka ya mapato  mjini Babati,  ambapo mlalamikaji alifika na kukutana na  Maafisa  hao wawili kutoka mamlaka ya mapato Tanzania ambao walimfahamisha kuwa wamefanya ukaguzi wa biashara yake  na kugundua kuwa alikadiriwa  vibaya na hivyo kumtaka  kulipa ongezeko la zaidi ya shillingi millioni tano [Sh.5.812,544,00.]

Makungu ameeleza kuwa  mfanyabiashara huyo (mlalamikaji)  alikubali ongezeko hilo na alianza kulipa kwa awamu  baada ya kuomba na kukubaliwa kulipa kwa awamu na Meneja  wa mamlaka ya mapato Wilaya ya mbulu, ambapo uchunguzi wa Takukuru mkoani hapa ulibaini kuwa mlalamikaji akiwa amelipa awamu ya kwanza ya ongezeko hilo  na baadae alipigiwa tena simu na washitakiwa na kutakiwa kwenda Babati kwa ajili ya mahojiano kuhusu ulipaji kodi wa mwaka  huo  wa 2018 ambao ulikuwa tayari wamemkadiria ongezeko.

Aidha mlalamikaji huyo alikuwa na washitakiwa katika ofisi za mamlaka za mapato  Babati na akajulishwa kuwa kuna ongezeko tena kwenye kodi ya biashara yake ya kiasi cha shilingi millioni arobaini  na tano (45,000,000).

‘’Ongezeko hilo lilimuweka mfanyabiashara huyo  kwenye wakati mgumu  lakini hata hivyo washitakiwa walimpooza  mfanyabiashara huyo kwa maelezo  kuwa wanaweza kumpunguzia kutoka million 45  hadi kufikia ongezeko la million 9  endapo angekubali kutoa  rushwa’’alisema Makungu .

Hata hivyo uchunguzi wa Takukuru  uliendelea kubainisha kuwa mjadala wa kiasi gani  cha rushwa atoe ili apunguziwe ongezeko   uliendelea kati ya washtakiwa na mfanyabiashara  huyo, ambapo dau la shilingi  million 20 (20,000,000)  waliloanzia lilipungua hadi  kufikia million 10 (10,000,000)  ambapo mfanyabiashara huyo alielekezwa kuzipeleka  kwa mmoja wa mawakala waliopo mjini Babati  na ilipofikia hatua hiyo ndipo makachero wa Takukuru walipoandaa mtego uliopelekea watuhumiwa kukamatwa.

Hata hivyo mkuu wa TAKUKURU  mkoani hapa Holle Makungu   ametoa wito kwa mamlaka ya  ya mapato mkoa wa manyara  na Tanzania kwa ujumla  kwamba kuna haja ya kuangalia upya mfumo wa ulipaji  wa kodi ili kuwa na mfumo unaoeleweka kwa wafanyabiashara wote wa biashara za aina zote  ili kudhibiti vitendo vya rushwa na kuondoa mianya inayotumiwa  na baadhi ya maafisa wachache  wa mamlaka hiyo  waliokosa uadilifu kwa kuwabambikia wafanyabiashara kodi  zisizolipika  kwa nia ya kuwatisha  kisha kujipatia rushwa  kama walivyofanya watuhumiwa hao.


Share:

Msajili wa vyama vya siasa Avikumbusha Vyama Vya Siasa kukabidhi ratiba zake Mapema

Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mtungi, amevikumbusha vyama vya siasa kukabidhi ratiba zake za mchakato wa mambo mbalimbali wanapoelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Amesema kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa vinapaswa kumshirikisha Msajili kwenye ratiba zao ndani ya vyama kuhusu mchakato wa uchaguzi.

Amesema hadi sasa hakuna mabadiliko ya Uchaguzi Mkuu na kwamba licha ya uwapo wa ugonjwa wa corona, shughuli zitaendelea kama kawaida, lakini kwa tahadhari kubwa.

“Tulishawaandikia  kwa mujibu wa sheria ya vyama vikifikia kwenye mchakato wa uchaguzi wakumbuke kutupatia ratiba zao

“Hatuvizii  ili wakosee bali tunawakumbusha mapema kuweka wazi ratiba zao ili nasi tushiriki…wakienda kinyume tumepewa nguvu kisheria kuweka pingamizi,” alibainisha.

Hivi karibuni, vyama vya CCM, Chadema na ACT Wazalendo, vilitangaza kuanza michakato ya ndani kuelekea uchaguzi mkuu ambao umebakisha miezi mitano

Majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni kusajili chama cha siasa kinachokidhi vigezo vya usajili kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, ikiwamo kufuta chama chenye usajili wa muda au kudumu ambacho kwa mujibu wa sheria kimepoteza sifa ya usajili.


Share:

Video Mpya : BHUHULU LUSAFISHA - MUNGU



Ninayo hapa ngoma mpya ya Manju/Msanii Bhuhulu Lusafisha kutoka Shinyanga inaitwa Mungu...Itazame hapa chini

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger