Sunday 29 September 2019

Waziri Mkuu: Tusikwepe Jukumu La Kuwatunza Wazee

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana na jamii kwa ujumla wasikwepe jukumu la kuwatunza wazee kwa sababu nguvu zao za uzalishaji mali zimepungua kutokana na kazi waliyoifanya wakiwa vijana kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa familia zao na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee uliozinduliwa Januari, 2019 ili  kwa kutokomeza ukatili kwa wazee ifikapo 2023 na kuhakikisha wazee na watu wenye ulemavu wanatambuliwa na kulindwa dhidi ya ubaguzi, uonevu, ukatili na mila potofu.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Septemba 29, 2019) wakati akizindua kambi ya utoaji wa huduma za afya kwa wazee na watu wenye ulemavu katika viwanja vya Kichanganimjini Iringa. Kambi hiyo imeandaliwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Dkt. Ritta Kabati katika kuadhimisha siku ya Wazee Duniani.

Amesema wajibu wa kuwahudumia au kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ni wa kila mmoja na wanapaswa watambue kwamba wazee hao wamelitumikia Taifa kwa muda mrefu tena kwa namna mbalimbali ikiwemo kuwaletea na kuhakikisha wanapata mafanikio hayo ambayo wanajivunia sasa.

“Kwa msingi huo, tunao wajibu wa kuwajali wazee wetu kwa hali na mali ikiwa ni sehemu ya matunda ya uwajibikaji wao kwetu na kwa Taifa kwa ujumla. Hivyo basi, tutumie vema Kambi hii kuwasaidia wazee wetu na watu wenye ulemavu kwa kutambua afya zao na kuwapatia matibabu ya kiafaya ili waendelee kuwa salama na wenye furaha nasi tuvune busara zao.”

Kutokana na umuhimu wa kuwatunza wazee na kuwasaidia watu wenye ulemavu, Waziri Mkuu ametoa rai kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa, wananchi na wadau mbalimbali kuendelea kuimarisha upatikanaji wa fursa, haki na ustawi wa wazee ikiwemo kuondokana kabisa na vitendo vya ukatili dhidi yao.

“Vituo vyote vya kutoa huduma za afya vya umma kutoa huduma bora na za haraka kwa wazee wetu wenye vitambulisho. Tengeni dirisha maalumu kwa ajili ya kuwahudumia ili wasikae kwenye foleni muda mrefu. Serikali itaendelea kuweka miundombinu na mazingira rafiki ili kuwawezesha kupata mahitaji yao.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kusimamia maelekezo yake kwa Halmashauri zote nchini kuwatambua wazee wasiojiweza na kuwapatia vitambulisho vya matibabu bila malipo. “Namshukuru Mbunge wa Viti Maalum Ritha Kabati amebainisha mafanikio yanayoendelea kupatikana kutokana na utekelezaji wa agizo hilo.

“Haidhuru nasi tukiiga mfano wa Mheshimiwa Ritta Kabati, Mbunge wa Viti Maalumu na kaka yangu Mheshimiwa Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu kwa moyo wao wa kizalendo kabisa kuona kuna haja ya kusaidia na kuunga mkono juhudi za Rais wetu mpendwa Dkt. John Magufuli za kuwahudumia wanyonge.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameendelea kuziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zoezi hilo linakuwa endelevu kwa kuwatambua na kuwapatia vitambulisho wazee wote nchini wasio na uwezo ili waweze kunufaika na huduma ya matibabu bila malipo pamoja na huduma zingine za kijamii.

Vilevile, Waziri Mkuu amesema kwa kuwa Novemba 2019 nchi inatarajia kufanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wazee kama sehemu ya jamii wana haki ya kushiriki katika uchaguzi huo kwa kuchagua viongozi wanaoona watafaa kuwaongoza na wao kuchaguliwa kuongoza katika nafasi mbalimbali. Hivyo wasaidiwe kushiriki zoezi hilo.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Mstaafu na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa, Peter Pinda alimpongeza Dkt. Ritta kwa uamuzi wake wa kuandaa kambi hiyo ambayo itatoa fursa kwa wazee kupima afya zao na kupatiwa huduma pamoja na kutoa viungo bandia kwa baadhi ya walemavu.

“Uzee ni hali siyokwepeka upende usipende ila unaweza kucheleweshwa kutegemea na aina ya matunzo wanayopatiwa. Nashauri wazee wapate vyakula bora tena kwa uwiano sahihi, vyakula hivyo ni pamoja na vya jamii ya mizizi, mikunde, nafaka, mbogamboga na nyama ili waweze kuimarisha afya zao.”

Awali, Waziri Mkuu alipokea taariza za ujenzi wa jengo la Ustawi wa Jamii Manispaa ya Iringa lilojengwa kwa ufadhili wa Mkurugenzi wa Kundi la Makampuni ya Asas, Salim Abri kwa gharama ya sh. milioni 60.

Kwa upande wake,Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Iringa Tiniel Mmbaga alisema kukamilika kwa jengo hilo kutawawezesha kutoa huduma bora kwa jamii na kwa wakati kwani awali maafisa watano walikuwa wakilundikana katika chumba kimoja hali iliyosababisha wateja kushindwa kueleza matatizo yao baada ya kukosekana kwa usiri.

Alisema kwa siku wanashughulikia malalamiko yahusuyo masuala ya migogoro ya familia ikiwemo matunzo ya watoto kuanzia 15 hadi 30 pamoja na wanawake zaidi ya 50 ambao kila mwezi wanakwenda kuchukua fedha kwa ajili ya matunzo ya watoto zinazotolewa na wenza wao kufuatia kuwepo kwa migogoro baina yao.

Shughuli hiyo, imehudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI Josephat Kandege, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye UlemavuStela Ikupa pamoja na Maafisa wengine wa Serikali.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Rais wa China amtunuku Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Dr Salim Ahmed Salim Nishani ya Juu ya Urafiki

Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Xi Jinping, leo asubuhi tarehe 29 Septemba 2019 amemtunukia Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa. Dk. Salim Ahmed Salim, Nishani ya Juu ya Urafiki ya Jamhuri ya Watu wa China ikiwa ni sehemu ya matukio ya maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China iliyofanyika jijini Beijing.  Mheshimiwa Dkt. Salim anakuwa mwafrika wa kwanza kupewa heshima na tuzo hiyo ya juu katika historia ya China.

Nishani hiyo ilipokelewa na Bi. Maryam Salim, Binti ya Dk. Salim Ahmed Salim ambaye pia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Albania kwa niaba ya Baba yake kutokana na kushindwa kuhudhuria kwa sababu za kiafya. Katika tukio hilo, Serikali ya Tanzania iliwakilisha na Balozi wa Tanzania nchini China Mheshimiwa Mbelwa Kairuki.

Hafla hiyo kubwa ya kitaifa ya kukabidhi nishani ilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Chama na Serikali ya China akiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Wang Qishan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Li Keqiang, Spika wa Bunge Mheshimiwa Li Zhanshu na Wajumbe wote wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Baraza la Taifa.

Mbali na Dk.Salim,  wengine waliotunukiwa Nishani ya Urafiki ni pamoja na Kiongozi wa Chama cha Kikoministi cha Cuba Jenerali Raul Castro, Dada wa Mfalme wa Thailand Maha Chakri Sirindhorn, Kiongozi wa Jumuiya ya Urafiki ya China na Urusi Ndugu Galina Kulikova, Waziri Mkuu Mstaafu wa Ufaransa Jean-Pierre Raffarin na Bi  Isabel Crook  kutoka Canada.

Vilevile  Rais Xi alitoa Nishani  ya Jamhuri na Nishani ya Heshima ya Taifa kwa raia 36 wa China kwa kutambua mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa la China kupitia kazi zao katika fani mbalimbali.

Nishani ya Juu ya Urafiki ya Taifa la China imetolewa kwa Dkt. Salim  kutokana na mchango wake wa kuiwezesha Jamhuri ya Watu wa China kuwa Mwanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 1971 alipokuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.  Aidha, mchango wa Dk. Salim katika kuimarisha mahusiano kati ya China na Tanzania wakati aliposhikilia nyadhifa mbalimbali umetajwa kama sababu ya kutunukiwa Nishani hiyo. Vilevile, mchango wa Dk.Salim katika kujenga mahusiano kati ya China na Afrika akiwa na nafasi ya Katibu Mkuu wa OAU umetajwa kuwa sababu nyingine ya kutunukiwa Nishani.

Tukio la Kutoa Nishani limetangazwa moja kwa moja na Televisheni zote za Jamhuri ya Watu wa China na kushuhudiwa na watu zaidi ya Milioni 500.

Kwa mujibu wa maelezo ya Balozi wa Tanzania nchini China Ndugu Mbelwa Kairuki Kupitia tukio la leo, mamilioni ya Wachina hususan vijana wamepata fursa ya kufahamu nafasi na mchango wa Tanzania na Bara la Afrika katika historia ya taifa lao. Aidha, tukio la leo limeifanya Tanzania kufahamika kwa watu wengi zaidi nchini China kupitia tukio mara moja. Hatua hiyo itaamsha udadisi na hamasa miongoni mwa Wachina wengi wa kizazi kipya kutaka kuifahamu zaidi Tanzania. Hali hii yaweza kujitafsiri katika fursa kubwa ya kukua kwa utalii, biashara na wawekezaji ikizingatiwa kuwa  wananchi wa China hutoa mwitikio mkubwa kwa nchi ambazo husemwa vizuri na kuthaminiwa na Serikali yao.

Aidha Balozi Kairuki ameeleza kwamba maadhimisho ya miaka 70 ya Jamhuri ya Watu wa China mwaka huu yanaambatana na maadhimisho ya miaka 55 ya urafiki na udugu kati ya China na Tanzania kufuatia kuanzishwa kwa mahusiano rasmi ya kidiplomasia mwaka 1964. Uhusiano wa China na Tanzania uliotokana na uhusiano mzuri wa waasisi wa mataifa haya mawili, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mao Tsetung. Uhusiano huo umeendelezwa na viongozi wa pande zote mbili ambao umekuwa ukiimarika siku hadi siku. Uhusiano huu umekwenda mbali zaidi ya uhusiano kati ya Serikali na Serikali na kushamiri kwa uhusiano wa watu kwa watu.

Ni kwasababu hiyo, katika maadhimisho ya miaka 70 ya Taifa la China, Jumuiya ya Urafiki wa watu wa China na Tanzania ni miongoni mwa Jumuiya za mataifa 17 yenye urafiki wa majira yote na China walioalikwa  kushiriki kwenye maadhimisho hayo na tarehe 1 Oktoba 2019 watakuwa na gwaride lao maalum. Katika jumuiya hizo 17, Kutoka Barani Afrika ni Tanzania na Zambia ndio watahudhuria.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,


Share:

Kabudi: Tanzania tumedhamiria kubadili maisha ya watu wetu

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Profesa Palamagamba John Kabudi amesema Tanzania imedhamiria kubadili maisha ya wananchi wake ikijitahidi kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

Akihutubia mjadala Mkuu wa Baraza Kuu laUmoja wa Mataifa kikao cha 74 mjini New York Marekani Ijumaa usiku Profesa Kabudi amesema Tanzania imeweka ajenda kuu za kuzitekeleza ambazo ni pamoja na “kutokomeza ufisadi, kurejesha haki na heshma katika sekta za umma, na kuimarisha ukusanyaji kodi kama mbinu ya kufikiwa kwa haraka ukuaji wa kiuchumi." 

Mengine wanayoyapa kipaumbele ni “elimu bora kwa wote, huduma za afya, na uwajibikaji.”

Waziri huyo amesema  hivi juhudi hizo pia zinalenga kuboresha kiwango cha elimu nchini , kutokomeza umasikini, na kukabiliana na kushughulikia tatizo la ajira, uandikishaji watoto wanaoingia shule kimepanda kwa asilimia 35.2 ikiwa imechangiwa na hatua ya serikali ya kutoa elimu bure kwa shule za msingi hadi kitato cha nne.

Hatua zinazochukuliwa
Waziri Kabudi amesema serikali imechukua hatua madhubuti kukabiliana na ufisadi ambazo ni pamoja na “kuanzisha kitengo cha kupambana na uhalifu na ufisadi katika mahakama kuu, na kuimarisha suala la uwajibikaji na uwazi katika serikali. "

Katika miaka minne iliyopita Profesa Kabudi amesema serikali imetekeleza mabadiliko kadhaa yanayojumuisha kudhibiti utajiri na mali asili ya nchi hiyo kwa kupitia mikataba mbalimbali na hatua hizo zitasaidia kuongeza pato la taifa kwa ukusanyaji mapato, pia sheria mpya za madini zimeisaidia Tanzania kukusanya mabilioni ya fedha ambayo yameisaidia serikali kuongeza kiasi cha bajeti yake hadi asilimia 40 mwaka 2019 ukilinganisha na asilia 25 mwaka 2016.

Profesa Kabudi ameongeza kuwa mapato hayo yamesaidia kuboresha miradi mbalimbali ya miundombinu na kuinua hali ya wananchi kuanzia katika afya, maji, na usafi. Hatua hizo pia zimesaida kutoa elimu bure kwa shule za umma za msingi na sekondari akitolea mfani shule za msingi uandikishaji Watoto umeongezeka kwa asilimia 35.2.

Amesema serikali pia inahakikisha uhifadhi mazingira na kujumuisha kila mwananchi katika mchakato wa SDGs ikiwemo makundi yasiyojiweza.

Na katika upande wa nishati ambayo awali ilikuwa ni bidhaa adimu sasa takriban asilimia 67 ya wananchi wa Tanzania wana nishati ya umeme kutokana na mradi maalum wa kusambaza umeme vijijini, REA .

Pia kuna ujenzi wa bwawa kubwa kabisa la kuzalisha umeme unaoendelea  ambao utakuwa  mkombozi sio tu kwa wananchi wa taifa hilo bali hata nchi jirani.

Pia amesema mbali ya uhifadhi wa mazingira kuna masuala mengine yanayozingatiwa ikiwemo nishati endelevu na kuhakikisha teknolojia hiyo inawasaidia mengi.
Uhuru wa vyombo vya habari

Prosesa Kabudi amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika suala la uhuru wa vyombo vya habari na kuongeza kiwango cha utoaji leseni akitolea mfano kwamba taifa hilo lina jumla ya vituo vya redio 152 na ni vitatu tu ndivyo vinamilikiwa na serikali, huku vituo vya televisheni vikiwa 34 na viwili tu ndivyo vinavyomilikiwa na serikali. Kwa upande wa magazeti serikali imetoa jumla ya leseni 172.

Na mwisho ametoa wito kwa nchi zote wanachama kukumbatia ushirikiano wa kimataifa sio tu kwa ajili ya kutomoza umasikini, kuboresha kiwango cha elimu, kukabiliana na mabadiliko yatabianchi na kufikia uwajibikaji bali pia katika kudumisha amani na usalama lakini pia katika kuleta haki na kuwa na dunia bora.


Share:

Waziri Mkuu: Waliokula Fedha Za Maji Wakamatwe

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza kukamatwa na kuwekwa ndani viongozi wa kamati ya watumiaji maji wa mradi wa maji wa Matunguru uliopo katika Kijiji cha Tungamalenga wilayani Iringa kwa tuhuma za ubadhilifu wa sh. milioni saba.

Ametoa agizo hilo jana jioni (Jumamosi, Septemba 28, 2019) baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakati akihutubia  mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Idodi wilayani Iringa.

Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela afuatilie suala hilo kwa kuwa kamati nyingi za watumiaji maji zimekuwa na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha zinazokusanywa kutoka kwa wananchi jambo ambalo si sahihi.

Alisema ifikapo saa 4.00 asubuhi ya leo watuhumiwa wote wanaohusika na ubadhilifu huo wawe wameshakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola kwa ajili ya kwenda kujibu tuhuma zinazowakabili.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema kwamba Serikali itajenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Iringa hadi Ruaha yenye urefu wa kilomita 104 ili kuboresha huduma za usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo na kuinua uchumi.

Waziri Mkuu aliyasema hayo baada ya kupokea malalamiko ya ubovu wa barabara hiyo kutoka kwa mbunge wa jimbo la Ismani, William Lukuvu ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Mbunge huyo alisema licha ya Serikali kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo ikiwemo ya maji, afya na umeme, lakini wanakabiliwa na tatizo la ubovu wa barabara ambapo aliomba Serikali iwasaidie.

Baada ya Waziri Mkuu kusema kuwa Serikali itahakikisha barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami wananchi walifurahi na kuishukuru Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuwajali wananchi wake.

Awali, Waziri Mkuu alikagua na kuzindua majengo matano ya kituo cha afya Idodi ambayo yamegharimu sh. milioni 400. Pia Serikali iliongeza sh. milioni 300 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba. Waziri Mkuu alisema ameridhishwa na ujenzi wa mradi huo.

Kwa upande waobaadhi ya wagonjwa waliolazwa katika wodi ya Mama na Mtoto ambao walikuwa wajifungua kwa njia ya upasuaji waliishukuru Serikali kwa kuboresha na kusogeza huduma za afya karibu na makazi ya wananchi.

Mmoja wa wagonjwa hao, Agusta Nyagawa alisema awali walikuwa wanalazimika kwenda hadi Iringa mjini kwa ajili ya kufuata huduma za afya lakini kwa sasa huduma hizo zikiwemo za kujifungua pamoja na vipimo wanazipata kituoni hapo.

Naye, Chipe Ngugi alisema anaishukuru Serikali kwa kuwa huduma za afya zimeboreshwa katika hospitali yao ya kata, hivyo hawatalazimika tena kusafiri umbali mrefu hadi Iringa kwa ajili ya kufuata huduma za afya zikiwemo za  upasuaji.

Alisema yeye alijifungua kwa njia ya upasuaji na anawashuwashukuru madaktari na wauguzi  kituoni hapo kwa huduma nzuri ambazo zimeokoa  Maisha yake na mtoto. Aliiomba Serikali iendelee kuboresha huduma kwa kuwa wapo mbali na mjini.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Wakandarasi Mradi Wa Maji Same-mwanga Watakiwa Kuongeza Kasi

Wakandarasi wanaotekeleza mradi wa maji wa Same-Mwanga wametakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji wake ili ukamilike kwa wakati.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga ametoa maelekezo hayo Septemba 28, 2019 wakati wa ziara yake iliyolenga kukagua hatua ya ujenzi iliyofikiwa na Wakandarasi wanaotekeleza mradi huo ambao ni kampuni ya M.A Kharafi & Sons na kampuni ya Badr East Africa Enterprises.

Mara baada ya kujionea shughuli zilizokuwa zikiendelea na kupokea taarifa ya mradi kutoka kwa wakandarasi hao, Mhandisi Sanga alieleza kutoridhishwa na kasi ya utekelezwaji wake na aliwasisitiza kuhakikisha kuwa mradi unakamilika kwa wakati.

Mhandisi Sanga aliwataka Wakandarasi kuwa wepesi kwenye kufanya mawasiliano na Wizara kila wanapokutana na changamoto yoyote ambayo ipo nje ya uwezo wao ili ufumbuzi upatikane haraka bila kuchelewesha shughuli za ujenzi wa mradi.

“Sijaridhishwa na kasi yenu ya ujenzi wa mradi. Kama kuna changamoto mnakutana nazo zilizo nje ya uwezo wenu mhakikishe mnawasiliana na Wizara mapema iwezekanavyo ili tupate ufumbuzi,” alisema Mhandisi Sanga.

Aliongeza kwamba Serikali inachohitaji ni kuona matokeo na haipo tayari kumvumilia mkandarasi ambaye anachelewesha mradi bila ya kuwa na sababu za msingi.

“Wanachohitaji wananchi ni maji, Serikali haitomvumilia Mkandarasi ambaye atashindwa kwenda na kasi inayokubalika,” alibainisha Mhandisi Sanga.

Mhandisi Sanga vilevile aliwakumbusha wakandarasi hao kuhakikisha manunuzi ya vifaa vinavyohitajika kwenye ujenzi wa mradi huo yanafanyika hapa nchini badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi hasa ikizingatiwa kwamba vingi vinapatikana hapa hapa Nchini.

Wakandarasi hao kwa nyakati tofauti walimuahidi Naibu Katibu Mkuu Sanga kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi sambamba na kuzingatia maelekezo aliyoyatoa.

Mradi wa Same-Mwanga ni miongoni mwa miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali kwa lengo la kuondoa kero ya maji kwa wakazi wa Miji ya Same na Mwanga, Mkoani Kilimanjaro na baadaye Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga.

Ziara hiyo ya Naibu Katibu Mkuu Sanga kwenye mradi huo ni ya kwanza tangu ameteuliwa na kuapishwa kushika wadhifa huo Septemba 22, 2019




Share:

Kituo Cha Uchenjuaji Dhahabu Jema Afrika Chapewa Onyo La Mwisho

Waziri wa Madini Doto Biteko ametoa Onyo la Mwisho la Kukifungia Kituo cha Uchenjuaji Dhahabu cha Jema Afrika kilichopo Wilayani Kahama.

Hatua hiyo inafuatia kubainika kwa jaribio la wizi wa dhahabu uliofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa  kituo hicho kutaka kuiba dhahabu ya mteja.

Akizungumzia tukio hilo, Waziri Biteko amewataka wamiliki wa kituo hicho kuandika barua ya kuweka makubaliano na Serikali ya kutojirudia tena kwa vitendo  vya wizi kituoni hapo.

‘’Ni jicho la huruma tu  tukiwapeleka mahakamani mali zenu zitataifishwa. Tunajua mmewekeza mitaji yenu na mna mikopo.  Nilishamwambia mmiliki kuwa kituo  chako kina rekodi ya wizi. Rais anawapenda, anawapigania ili watanzania wamiliki uchumi wa madini lakini mnamuangusha kwa kutofuata taratibu,’’ amesisitiza Waziri Biteko.

Amewatahadharisha wamiliki wa vituo vya uchenjuaji nchini kuhusu wizi wote wa dhahabu  unaofanyika na kuwasisitiza kwamba, unafahamika na kuwataka  wote wanaojihusisha na vitendo hivyo  kujiepusha  na  kwa wale wasiotaka kufanya kazi zao kwa  uaminifu watafute biashara nyingine.

Mbali na kutembelea kituo hicho,  pia, Waziri Biteko  na ujumbe wake  wametembelea Kituo Kidogo cha  Ununuzi   wa dhahabu kilichopo katika eneo la Wachimbaji wadogo wa Mwime  ambapo amewapongeza kwa kufuata taratibu na Sheria na kuwataka kufanya kazi zao kwa amani.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga  Zainab Taleck amesema  Mkoa huo unahitaji wawekezaji lakini walio waaminifu.

Ameongeza kuwa, wizi na udanganyifu katika kiwand cha uchenjuaji Jema Afrika ulibainiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama na kutumia fursa hiyo kuwatahadharisha wote wasiofuata taratibu kuwa serikali inawaona na itawafikia.

Katika ziara hiyo, Waziri Biteko pia ameongozana na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga, Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa na Watalaam kutoka Tume ya Madini.

Aidha, ziara hiyo imefanywa wakati ambapo wizara na wadau wengine wa madini wanashiriki Maonesho ya Pili ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini Mkoani Geita yanayotarajiwa kuhitimishwa Septemba 29, 2019.

Ziara hiyo imefanyika Septemba 28, 2019


Share:

CHANJO ITAKAYOMALIZA MAAMBUKIZI MAPYA YA VIRUSI VYA UKIMWI 'HIV' KUZINDULIWA

Kituo cha udhibiti wa magonjwa na maambukizi kimeannza kuifanyia kazi chanjo ya virusi vya Ukimwi ambayo itasaidia kumaliza maambukizi mapya ya HIV nchini Kenya, kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya.

Chanjo hiyo kwa jina HPTN-081 ni kinga inayohusisha protini ya damu inayoweza kupigana dhidi ya virusi vya HIV.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya 40 ya kituo hicho kwa ushirikiano na Kenya mjini Kisumu siku ya Ijumaa, Mkurugenzi mkuu wa kituo hicho nchini Kenya Marc Bultery alisema kwamba utafiti utahakikisha kuwa chanjo hiyo inaweza kusambazwa hadi maeneo mengine.

Tayari tumemailiza vipimo vyetu vya awamu tatu za chanjo hiyo na tunaelekea katika kupiga hatua kubwa zaidi ambazo zinaweza kwa kamili kuzuia virusi vya HIV, alisema Bultery.

''Tunaangazia wanawake kwasababu ni miongoni mwa makundi yalio na hatari kubwa ya kuambukizwa'', alinukuliwa na Daily Nation akisema.

Daktari Bultery pia alisema kwamba kituo hicho kitasaidia katika mpango wa afya kwa wote nchini Kenya UHC.

''Ni lengo letu kuhakikisha kuwa makundi yote yanaweza kupata matibabu ya bure ikiwemo makundi yaliobaguliwa kama vile wapenzi wa jinsia moja'', alisema bwana Bultery.

Naibu mjumbe maalum wa Marekani nchini Kenya Eric Kneedler alisema kwamba serikali ya Marekani imejizatiti kusaidia mpango wa afya kwa wote ikiwa miongoni mwa ajenda nne za serikali.

''Lengo ni kuona kwamba serikali ya Kenya inakuwa kutoka katika taifa linalotarajia kufaidika hadi taifa lililofaidika'', alisema bwana Kneedler.

Sherehe hizo za maadhimisho zilifanyika kukumbuka mafanikio yakituo hicho nchini Kenya kwa kipindi cha miaka 40.

Baadhi ya ufanisi huo ni pamoja na chanjo ya malaria iliozinduliwa hivi karibuni ambayo imeifanya Kenya na mataifa mengine ya Afrika kufaidika.

Chanjo ya HIV yaonyesha matumaini miongoni mwa binadamu

Chanjo hiyo yenye wezo wa kuwalinda watu duniani kutokana na virusi hivyo ilionyesha matumaini.

Tiba hiyo inayolenga kutoa kinga dhidi ya virusi kadhaa, ilitoa kinga ya HIV katika majaribio yaliofanyiwa watu 339, kulingana na utafiti mmoja uliochapishwa katika jarida la Lancet.

Pia iliwalinda tumbili dhidi ya virusi vinavyofanana na HIV.

Majaribio zaidi tayari yamefanywa kubaini iwapo kinga iliotolewa inaweza kuwalinda watu dhidi ya maambukizi ya HIV.

Takriban watu milioni 37 duniani wanaishi na virusi vya ya HIV au Aids na kuna takriban visa vipya milioni 1.8 kila mwaka.

Lakini licha ya kupiga hatua dhidi ya HIV , tiba yake na chanjo haijapatikana.

Dawa kwa jina Prep ni nzuri katika kuzuia maambukizi ya HIV lakini ikilinganishwa na chanjo inafaa kutumiwa mara kwa mara, hata kila siku ili kuzuia virusi hivyo kuzaana .

Uvumbuzi wa chanjo yake umekuwa changamoto kubwa kwa wanasayansi , kwa sababu kuna aina nyingi za virusi vyake vinavyopatikana katika maeneo kadhaa ya dunia.

Lakini kwa chanjo hii wanasayansi wameweza kutengeneza vipande vya tiba vinayoendana na aina tofauti za virusi vya HIV.

Matumaini ni kwamba inaweza kutoa kinga bora zaidi dhidi ya aina tofauti za virusi vya HIV vinavyopatikana katika maeneo mbali mbali ya dunia.

Washirika kutoka Marekani, Uganda, Afrika Kusini na Thailand walipewa chanjo nne katika kipindi cha wiki 48.

Mchanganyiko wa chanjo hizo ulisababisha kutokea kwa kinga ya HIV na wakaonekana wako salama.

Wanasayansi pia waliwafanyia utafiti kama huo tumbili ambao hawana maambukizi ya HIV ili kuwalinda dhidi ya kuambukizwa virusi vinavyofanana na HIV.

Chanjo hiyo ilionyesha kwa inaweza kuwalinda asilimia 67 ya tumbili 72 kutopata ugonjwa huo.

Wanasayansi waliwafanyia majaribio watu walio kati ya umri wa miaka 18 hadi 50 ambao hawakuwa na HIV na walikuwa na afya.

''Matokeo haya yanawakilisha hatua kubwa iliyopigwa'', alisema Dan Barouch , Profesa wa matibabu katika chuo kikuu cha matibabu cha Havard na kiongozi wa utafiti huo.

Hatahaivyo Profesa Barouch pia ametahadharisha kwamba matokeo hayo yanafaa kuchanganuliwa na tahadhari.

Ijapokuwa chanjo hiyo ilifanikiwa kuimarisha kinga ya watu waliojitolea kufanya majaribio hayo, haijulikani iwapo itatosha kukabiliana na virusi hivyo na kuzuia maambukizi.

''Changamoto katika kutengeza chanjo ya HIV ni nyingi, na uwezo wa kuziimarisha kinga haimaanishi kwamba chanjo hiyo itawalinda binaadamu dhidi ya maambukizi ya HIV'', aliongezea.


Share:

ROBERT MUGABE AZIKWA NYUMBANI KWAKE

Aliyekuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amezikwa nyumbani kwake huko Zvimba.

Kiongozi huyo wa zamani aliiongoza nchi yake kujipatia Uhuru lakini baadaye akashutumiwa kwa kukiuka haki za kibinaadamu na kuharibu uchumi wa taifa lililokuwa likinawiri.

Alifariki akiwa na umri wa miaka 95 nchini Singapore mapema mwezi Septemba. Jeneza lake lililokuwa na rangi ya shaba lilishushwa kaburini.

Robert Mugabe alikuwa amezungukwa na mkewe Grace, watoto na watu wa karibu wa familia yake. Ni marafikize wachache wa zamani waliohudhuria mazishi hayo.

Alizikwa katika eneo la nyumba ya familia yake. Ni wachache ambao wangedhania mtu mwenye haiba kama yake angezikwa na watu wachache.

Baadhi wanasema kwamba ilikuwa taarifa yake ya mwisho ya kisiasa. Kitu ambacho kitakumbukwa katika historia ni kwamba Mugabe alikuwa mchezaji wa chess ambaye hakukubali kushindwa

Wakati alipopinduliwa mwezi Novemba aliondoka bila kutaka. Amezikwa mbali na marafikize ambao anaamini walimsaliti.

Baada ya kifo chake familia yake ililamika hadharani kuwa haikushauriwa kuhusu mipango ya mazishi yake ya kitaifa.

Katika taarifa familia hiyo iliilaumu serikali kwa kutumia nguvu kupanga mazishi ya Mugabe katika makaburi ya mashujaa kinyume na "matakwa yake [Mugabe]".

Taarifa hiyo aidha ilisema kuwa ombi lake la mwisho lilikua la mke wake , Grace Mugabe, kutoondoka kando ya jeneza lake hadi atakapozikwa.
Familia yake inasemekana kughabishwa na jinsi kiongozi huyo alivyong'olewa madarakani na mshirika wake, wa zamani Rais Mnangagwa, miaka miwili iliyopita- halia mbayo huenda imesababisha mvutano kuhusu mahali atakapozikwa.

Bw. Mnangagwa alipendekeza kiongozi huyo azikwe Heroes Acre.

Mugabe, alikua Rais wa kwanza wa Zimbabwe baada ya nchi hiyo kupata uhuru 1980.

Miaka ya awali ya uongozi wake, alisifiwa kwa kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya na elimu kwa Waafrika walio wengi

Lakini baadae utawala wake ulikumbwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi na ukandamizaji wa wapinzani wake.

Alikuwa madarakani kwa karibu miongo minne kabla ya kuondolewa kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 2017 na wadhifa wake kuchukuliwa na Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa.
Je Mugabe ni nani?

Robert Mugabe alikuwa rais wa kwanza wa Zimbabwe

Mwaka 1980, Bw Mugabe alishinda uchaguzi na kuwa waziri mkuu.

Mwaka 1982 aliushutumu upinzani kwa kujaribu kupindua serikali.

Maelfu ya watu waliuawa alipolituma jeshi lake lililopata mafunzo Korea Kaskizini, kuwakandamiza maadui zake.

Mwaka 1987,alibadilisha katiba ili imruhusu kuwa rais na kuongeza mamlaka yake.

Uchumi ulidororeka baada ya mwaka 2000…

Wakati Mugabe aliagiza kunyakua mashamba yaliomilikiwa na watu weupe yaliyokuwa kinara katika uchumi.

Mfumuko wa bei ulipelekea sarufi ya taifa kuwa bila thamani na hali nchini humo ikazidi kudororeka.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2008, Mugabe alilazimika kugawanya mamlaka na kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai.

Japo kulikuwa na ghasia dhidi ya wafuasi wa Bw Tsvangirai katika kampeni za uchaguzi.

Ndoa yake na Grace Mugabe ,anayemzidi kwa maika 40, yaweza kuwa iliyomponza, Wengi walikasirishwa na Grace kuandaliwa kuwa mrithi wake.

Mugabe aliapa kuwa Mungu peke yake ndio angeweza kumtoa madarakani.
Chanzo - BBC
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili Septemba 29




Share:

Saturday 28 September 2019

ZESCO UNITED WAICHAPA YANGA 2-1 , LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Na mpiira, umekwisha, Yanga inaondolewa rasmi kwenye mashindano ambapo itacheza Shirikisho na Zesco inaingia hatua ya makundi.

Dak ya 90+4, Zesco wanacheza kwa akili ya kumaliza dakika zilizoongezwa.
Dak ya 90, Moro anapewa kadi nyekundu kwa kucheza madhambi, sasa Yanag wamebaki pungufu. Dakika nne za nyongezwa zinaoneshwa na Mwamuzi wa mezani.

Dak ya 85, Kamusoko anapiga faulo, inaokolewa.
Dak ya 84, faulo nyingine karibu kabisa na eneo la hatari mwa Yanga inapigwa na Zesco. Kamusoko anaonekana na mpira. Muda huo Ally Ally anatoka na Kalengo anaingia kuchukua nafasi yake.
Dak ya 83, Maybin Kalengo anaokena akiandaliwa, bila shaka anataka kuingizwa kuchukua nafasi ya mtu mwingine.
Dak ya 82, hali inakuwa ngumu sasa kwa Yanga, wanapaswa kusawazisha ili mechi iongezwe dakika 30 za ziada.

Dak ya 78, Makame anaizawadia Zesco bao la pili kwa kujifunga, sasa ni 2-1.
Dak ya 69, Yanga wanakosa utulivu wa kutengeneza bao la pili, ni baada ya krosi safi kupigwa engo ya kushoto mwa uwanja lakini inakosa wa kuifanyia kazi.
Dak ya 69, kina nyingine kwa Zesco kipindi hiki cha pili, inapigwa na inaokolewa.
Dak ya 63, Metacha anaanza tena upya.
Dak ya 62, hatari nyingine inatokea katika lango la Yanga, mipira yao ya vichwa inashindwa kufanya walichodhamiria. 

Dak ya 59, Zesco wamekuwa wakifanya mashambulizi mengi japo yamekuwa yakikosa utulivu na ubora wa Yanga eneo la ulizi unakuwa vizuri.
Dak ya 56, Faulo nyingine inapigwa kuelekezwa Yanga, pigwa pale Yanga wanaokoa, unatanguliwa mbele kwake Sadney, unamkuta kipa Banda, anaanza upya.
Dak ya 54, faulo inapigwa na Yanga wanaokoa, wakati huo mchezaji mmoja wa Yanga ameodondoka.
Dak ya 54, Kelvin Yondani anapewa kadi ya njano kwa kucheza madhambi, inakuwa kadi ya nne katika mchezo huu, Yanga wana tatu na Zesco moja.

Dak ya 51, Zesco sasa wanamiliki, mpira anakwenda kwake Kamusoko, hatari kule, Yanga wanaokoa, ilikuwa hatari aisee.
Dak ya 49, Yanga wanafanya shambulizi jingine lango ni mwa Zesco lakini linashindwa kuzaa matunda.
Dak ya 49, Ally Ally anarusha mpira kuelekea Zesco baada ya kutolewa nje.
Dak ya 48, mpira upo kwake Mnata hivi sasa, anaanzisha upya.
Dakika 45 za kipindi cha pili kimeanza

MAPUMZIKO: ZESCO 1-1 YANGA

Dak ya 43, Zesco wanapata faulo karibu kabisa na eneo la penati, ni baada ya Ally Ally kucheza sivyo, wakati huo kuna mchezaji wa Yanga ameanguka chini.
Dak ya 42, Zesco wanajaribu kusaka lango la Yanga kwa nguvu lakini mabeki wake wanapambana kuwazuia, wameongeza kasi.
Dak ya 41, Mpira unarushwa kuelekezwa Yanga.

Dak ya 39, Yanga wanapata kona, inapigwa lakini inashindwa kuzaa matunda.
Dak ya 37, ni faulo, kadi nyingine na ya pili kwa Yanga inenda kwa Moro baada ya kucheza madhambi.
Dak ya 35, Zesco wnafanya shambulizi jingine, Kamusoko anao mpira, Yanga wanaokoa.
Dak ya 34, Yondani anafanyiwa faulo na mpira unapigwa kuelekea Zesco United.
Dak ya 30, Yanga wanakosa nafasi nyingine, inakuwa kona, anakwenda kupiga Sibomana, kwake Sadneeeey, gooli, wanasawazisha.

Dak ya 27, Kaseka anapata kadi ya njano kwa kucheza madhambi, ni kadi ya kwanza kwa dakika 45 za kwanza.
Dak ya 24, Goooli, Zesco wanapata bao la kwanza kupitia kwa Jesse Were akifunga kwa kichwa.
Dak ya 22, Zesco wanazidi kutawala, mpira unarushwa kuelekezwa langoni kwao.
Dak ya 21, Zesco wanaonekana kutawala eneo la kati, wakipambana kusaka namna ya kuipenya ngome ya Yanga.
Dak ya 20, Zesco wanarusha mpira kuelekea Yanga, ni faulo tena Akumu anachezewa, hapana ni offside, Yanga wanacheza.

Dak ya 19, Kamusoko anapiga lakini mabeki wa Yanga wanaokoa.
Dak ya 18, Zesco wanapata faulo, anaenda kupiga Kamusoko, ni kushoto kidogo, mita chache karibu na eneo la hatari.
Dak ya 16, Kaseke anapasiana na Ally Ally kulia kwenye kona ya kulia mwa kibendera lilipo lango la Zesco lakini wanashindwa kuwa watulivu na wapinzani wanauchukua.
Dak ya 14, mlinda mlango wa Zesco Jacob Banda anaonekana akituliza mpira kwa madaha, ni dalili za kupoteza muda ikiwa ni dakika za mapema.
Dak ya 12, Levy Mwanawasa hakuna watu, idadi ndogo ya mashabiki inaonekana.

Dak ya 11, Sadney Urikhob anatoa mpira nje ambao kama angeutuliza vizuri ungeweza kuwa na faida kwa Yanga.
Dak ya 10, ni goli-kiki, kipa Mtacha anonekana akiwaambia jambo wachezaji wake.
Dak ya 09, Tshishimbi anatoa mpira nje, unarushwa kuelekezwa Yanga.
Dak ya 09, Yanga wanafanya shambulizi kali lakini umakini wa kumalizia kambani unakosekana.
Dak ya 08, bado mchezo haujawaa na utulivu kwa timu zote mbili.

Dak ya 07, kona nyingine wanapata Zesco united, wanapiga na Yanga wanaokoa, Lamine Moro anapiga kichwa.
Dak ya 06, Zesco wanapata kona ya kwanza.
Dak ya 05, Tshishimbi anapata nafasi ya kutengeneza shambulizi lakini mabeki wa Zesco wanakuwa mahiri, wanamzuia.
Dak ya 04, faulo inapigwa kuelekezwa katika lango la Yanga.
Dakika 45 za kwanza zimeanza katika uwanja wa Levy Mwanawasa, Ndola, Zambia.
Share:

PICHA: Nyoka Mkubwa Avamia Mkutano wa Waziri Mkuu.....Askari Polisi Aliyemdhibiti Apewa Zawadi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemzawadia  Askari Polisi PC Alphonce Daniel Mwambenga sh. 200,000 kutokana na ujasiri wake wa kumdhibiti kwa kumkanyaga nyoka mkubwa aliyekuwa akieleakea jukwaa kuu wakati Waziri Mkuu akihutubia katika Kilele cha Wiki  ya Viziwi Duniani kwenye Uwanja wa Kichangani, Kihesa mjini Iringa, Sepotemba 28, 2019. 

 Kitendo hicho kilifanyika kimyakimya hivyo hapakuwa na taharuki yoyote .  Pichani, Mheshimiwa  Majaliwa akimkabidhi Mwambenga fedha hizo. Wapili kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa na kulia  ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara y a Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Dkt.Avemaria Semakafu.  Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na wa nne kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel  Nyamkahanga.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Share:

Waziri Mkuu Majaliwa Azindua Urasimishaji Wa Lugha Ya Alama Tanzania

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inatambua umuhimu wa kuwa na lugha moja ya alama ili kuwezesha mawasiliano ya watumiaji wa lugha hiyo, hivyo itaendelea kusimamia uendelezaji, usanifu na urasimishaji wa Lugha ya Alama ya Tanzania, ambao ameuzindua leo(Jumamosi, Septemba 28, 2019).

Amesema hatua hiyo itawezesha utoaji wa elimu katika ngazi mbalimbali pamoja na kuboresha mawasiliano katika jamii na tayari imetoa mafunzo ya lugha hiyo awamu ya kwanza kwa walimu 82 wa shule za Sekondari nchini na kwamba zoezi hilo ni endelevu.


Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Septemba 28, 2019) wakati akihutubia wananchi kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Viziwi Duniani katika Uwanja wa Kichangani – Kihesa, wilayani Iringaakiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Iringa.

Kaulimbiu ya siku ya Viziwi Duniani kwa mwaka huu inasema “Haki ya Matumizi ya Lugha ya Alama kwa wote”. Kaulimbiu hiyo inalenga kuondoa vikwazo vya mawasiliano miongoni mwa Watanzania ambao ni Viziwi.

“Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeanza kurasimisha Lugha ya Tanzania, kutayarisha vifaa vya kufundishia Lugha ya Alama ya Tanzania na kufundisha walimu katika shule za Msingi na Sekondari nchini. Mchakato huo utachukua muda wa takribani miaka miwili kukamilika.”

Amesema Serikali itahakikisha kuwa lugha ya alama ya Tanzania inatambulika na kutumika kikamilifu kama chombo cha mawasiliano miongoni mwa Viziwi nchini ili kuwawezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa lao.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria na inatekeleza kwa dhati jitihada za kutoa kipaumbele kwa Watanzania wanyonge ambao hawakuwa wakinufaika ipasavyo na rasilimali za nchi.

“Serikali yenu sikivu inatambua vikwazo vya aina hiyo na inatekeleza maelekezo ya Ilani ya CCM ya 2015/2020, ambayo inaielekeza Serikali ihakikishe watu wenye ulemavu wanapata elimu kwa kupata vifaa maalumu na kushiriki katika shughuli za kijamii.”

Hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuwekeza kwenye miundombinu na mazingira rafiki yatakayowawezesha watu wenye ulemavu kwenda wanapotaka, kutumia vyombo vya usafiri na kupata habari kama walivyo wengine. Amesema katika ofisi yake ataajiri mkalimani wa lugha za alama.

Amesema Serikali itaendelea kuboresha mahitaji maalumu ya watu wenye ulemavu kwa kuwawezesha kupata taarifa mbalimbali kwa urahisi kwa kutumia lugha ya alama, alama mguso, maandishi ya nukta nundu, maandishi yaliyokuzwa au njia nyingine zinazofaa.

Waziri Mkuu amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeanza kurasimisha Lugha ya Tanzania, kutayarisha vifaa vya kufundishia Lugha ya Alama ya Tanzania na kufundisha walimu katika shule za Msingi na Sekondari nchini. Mchakato huo utachukua  takribani miaka miwili kukamilika.

“Serikali kwa kutambua umuhimu wa kuwa na shule maalumu ya Serikali ambayo inahudumia watoto wenye mahitaji maalumu imeanza ujenzi wa Shule Maalumu Patandi katika Mkoa wa Arusha. Shule hiyo inatarajiwa kuchukua wanafunzi 600 wa Msingi na Sekondari na itagharimu sh. bilioni 2.8.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema katika mapitio ya Kanuni za Maudhui ya Vyombo vya Habari, Kanuni za mwaka 2011, Serikali imeingiza kipengele kipya kinachovitaka vyombo vyote vya habari kuwa na wakalimani wa lugha ya alama kwa vipindi muhimu. Baadhi ya vyombo vya habari ikiwemo Shirika la Habari Tanzania (TBC) vimekuwa vikitekeleza agizo hilo.

“Napenda kutumia maadhimisho haya kuagiza vyombo vyote vya habari kuhakikisha kwamba agizo hili linatekelezwa ipasavyo. Serikali kwa upande wake itaendelea kuhakikisha kuwa haki na mahitaji ya Watu wenye Ulemavu vinapatiwa ufumbuzi kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Watu wenye Ulemavu Na. 9 ya Mwaka 2010.”

Amesema anajua ajua changamoto wanazokumbana nazo viziwi wanapotaka kupata huduma mbali mbali katika vituo vya kutolea huduma za afya, mahakama, vituo vya polisi, nyumba za ibada na maeneo mengine muhimu kwa kuwa hayana wakalimani wa lugha ya alama.

Waziri Mkuu ametoa wito kwa taasisi zote za Serikali na binafsi zihakikishe zinakuwa na wakalimani wa lugha ya alama. “Pia naagiza kwamba mitaala ya vyuo vya Afya, Polisi, Mahakama na vinginevyo ihakikishe inazingatia kuongeza kozi ya Lugha ya Alama kama somo la lazima. Hii itasaidia kuzalisha watalaamu wa lugha ya alama ambao wataweza kuwahudumia wenzetu viziwi ipasavyo.”

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Nidrosy

Mlawa ameishukuru Serikali kwa kuwaamini watu wenye ulemavu na kuwateuwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi, lakini waomba iongeze nafasi za ajira kwa watu wenye ulemavu ili nao waweze kujikwamua kiuchumi na kusaidia Taifa.

Pia, ameiomba Serikali iwe na wakalimani wa lugha za alama kwa ajili ya kuwawezesha watu wenye ulemavu waweze kupata taarifa zinazolewa na viongozi wao. Wameomba Serikali ikamilishe mchakato wa urasimishaji wa Lugha ya Alama ya Tanzania. WaziriMkuu amesemamaombi na mapendekezo yao ni ya msingi na muhimu kwa maisha ya Viziwi. Lengo la Serikali ni kuboresha huduma zetu kwa Viziwi hapa nchini.

Maadhimisho hayo yamehudhuliwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI Josephat Kandege, Naibu Waziri - Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na wenye UlemavuStela Ikupa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu pamoja na viongozi wa CHAVITA.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Waziri Lugola Awakatalia Waliopewa Uraia Makazi Ya Wakimbizi Kushiriki Uchaguzi Serikali Za Mitaa Nchini

Na Mwandishi Wetu, Katavi
WAZIRI wa Mambo ya ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema wananchi waliopewa uraia katika Makazi ya Wakimbizi ya Katumba, Ulyankulu na Mishamo nchini hawatashiriki kugombea na kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni, kwa kuwa maombi yao bado yanafanyiwa kazi.

Akijibu maombi ya raia hao waliopo Kata ya Katumba, Mkoani Katavi, Waziri Lugola alisema maombi yao wanayo na Serikali inayafanyia kazi kwa ukaribu zaidi, hivyo wanapaswa kuwa wavumilivu kusubiri majibu yao.

“Serikali inawajali, inawathamini, na pia maombi yenu tunayo, na tunayafanyia kazi kwa ukaribu zaidi kwa kuwa Serikali ya Rais Dkt. Magufuli ni sikivu, naomba muendelee kusubiri bila kuwa na uharaka wowote,” alisema Lugola.

Akisoma hotuba ya wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Ndui Station, Diwani wa Kata hiyo, Seneta Baraka alisema wananchi hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo kutopata haki ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu 2019.

“Ombi letu kwako mheshimiwa Waziri ni kuturuhusu kufanya uchaguzi katika mazingira haya sawa na ilivyofanyika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, ikiwa haiwezekani basi ombi letu na  changamoto zitatuliwe na tupewe fursa ya kufanya uchaguzi mara baada ya changamoto hizo kutatuliwa,” alisema Baraka.

Baraka alisema raia hao walimuomba Waziri huyo, kubalidilisha hadhi ya eneo la Katumba, Mishamo Mkoani Katavi, na Ulyankulu Mkoani Tabora, kuwa na hadhi ya Serikali ya Mitaa kwa kuwa hadhi ya makazi ya wakimbizi inawanyima fursa nyingi za kimaendeleo.

Maombi mengine waliyoyatoa kwa Waziri huyo ni kukamilisha mchakato wa uraia kwa vijana wao uliofanyika mwaka 2017, wakidai kuwa Serikali ilikamilisha mchakato wa uraia wa awamu ya kwanza uliofanyika mwaka 2007, wapo ambao maombi yao hayajakamilika hadi sasa.

Pia waliomba usajili wa laini za simu kwa wenzao ambao hawajakamilisha mchakato wa uraia ili waweze kupata vitambulisho vya taifa.

Akijibu changamoto hizo, Waziri Lugola aliwaambia raia hao maombi hayo yapo mezani kwake na Serikali inayafanyia kazi kwa ukaribu na watapewa majibu mara watakapomaliza kuyafanyia kazi.

Kwa ombi la usajili wa laini za simu, Lugola alisema hiyo ni haki yao kupata vitambulisho, nakuwaahidi kuwa suala hilo litashughuliwa kwa kuwa zoezi hilo ni endelevu.

Kwa upande wake, Mkazi wa Kata hiyo ambaye alikimbia vita mwaka 1972 akitokea nchini Burundi, Zephania Mshinga ambaye ana umri wa miaka 84, alisema Tanzania ni nchi salama, na pia hayupo tayari kuiacha nchi hiyo ambayo ina amani, utulivu, na watu wakarimu.

“Msiombee vita jamani, nilifika hapa Tanzania mwaka 1972 wakati Burundi kulipokuwa na vita, nashukuru nimepewa uraia na kama nikinyang’anywa uraia huu sina mahali pa kwenda, siwezi kurudi nilipotoka maana miaka mingi imepita, sasa ni mkazi wa hapa, naishukuru Serikali ya Tanzania,” alisema Mshinga.

Waziri Lugola yupo Mkoani Katavi kwa ziara ya siku tano ya kikazi, akikagua miradi ya maendeleo, kuzungumza na askari na watumishi wa Wizara yake, pamoja na kusikiliza kero za wananchi katika mikutano ya hadhara mkoani humo.


Share:

Ongeza Nguvu Za Kiume, Maumbire Madogo Pamoja Na Tiba Mbalimbali

MASISA 3 POWER nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoazaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wara kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20-40

SUPER MONGERA  Hurefusha na kunenepesha maumbile madogo yaliosinyaa. Matatizi haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguluma na kujaa gesi,ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia ninadawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

Ni DR CHIPUPA  pekee mwenye uwezo wa kumrudisha mume , mke ,mchumb.

Kwa nini uhangaike na matatizo ya uzazi;   ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,

 wasiliana na DR. CHIPUPA 

Call+255 0673878343

watsap +255 0620510598

Huduma hii inakufikia popote ulipo


Share:

Iran yaikosoa Marekani kwa kumyima ruhusa waziri wake wa mambo ya Nje Javad Zarif kumtembelea hospitalini Balozi wa Iran

Iran imeikosoa Marekani kwa uamuzi wa kikatili wa kumzuia waziri wake wa mambo ya kigeni Javad Zarif kumtembelea hospitalini Balozi wa Iran kwenye Umoja wa Mataifa Majid Takht Ravanchi anaetibiwa ugonjwa wa saratani mjini New York. 

Zarif anahudhuria mkutano wa kilele wa hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa mjini humo. 

Shirika la habari la kitaifa nchini humo IRNA limemnukuu naibu waziri wa mambo ya kigeni Abbas Araghchi akisema Marekani imeligeuza suala hilo la kibinaadamu kuwa la kisiasa. 

Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani imesema itamruhusu iwapo Iran itamuachia huru mmoja wa raia wengi wa Marekani wanaodaiwa kushikiliwa kimakosa nchini Iran. 

Mwezi Julai Marekani ilitangaza kumzuia waziri huyo kuingia nchini humo, ikiwa ni miongoni mwa vikwazo vyake dhidi ya taifa hilo.

-DW


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger