Wednesday 29 May 2019

Rais Magufuli awasili nchini zimbabwe kwa ziara rasmi ya kitaifa ya siku 2




Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya May 29




Share:

Tuesday 28 May 2019

USHIRIKINA WATESA WALIMU NJOMBE

Na Amiri kilagalila-Njombe
Imani za kishirikina mkoani njombe zimetajwa kuwa ndio chanzo cha walimu kukaa kwa muda mfupi katika vituo vya kazi pamoja na wanafunzi kutokufika mashuleni (utoro).

Aidha imeelezwa kuwa kutokana na uwepo wa imani za kishirikina kwa baadhi ya shule zilipo pembezoni mwa mji inapelekea wanafunzi kufanya vibaya katika masomo yao hali ambayo ina athiri kiwango cha taaluma kwa wanafunzi.


Hayo yamebanishwa na afisa elimu kata ya mlowa Nitson Damian Mkate halmashauri ya mji wa makambako mkoani njombe wakati akizungumza na mtandao huu mara baada ya kuisha kwa mkutano wa hadhara katika mtaa wa Idofi , amesema kuwa katika kata hiyo kuna mtoto ambaye ameshindwa kuendelea na masomo kutokana na kila anapotaka kwenda shuleni anapatwa na tatizo la kuvimba usoni.


“Ni kweli ushirikina upo lakini ni tofauti na miaka ya nyuma kwa mfano mwaka jana mwalimu mkuu wa shule ya msingi Idofi alichukua walimu wa kujitolea kutoka Lungemba akawaleta hapa lakini usiku walikutana na sintofahamu ambayo hawakujua ni nini,walilala na suruali wakaamka asubuhi suruali zipo nje wengine walilalia mito wakamka asubuhi wakaona mito ina damu lakini hakuna mchubuko wa aina yoyote”alisema afisa elimu


Rajab Shomari ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi idofi amesema licha ya tabia hizo za kishirikina kupungua kwa kiasi kikubwa ikiwa nitofauti na miaka ya nyuma bado kuna tatizo hilo kwa baadhi ya watoto wanao jihusisha na vitendo hivyo pamoja na wazazi.


“Kuna watoto ambao wana tabia hizo na kuna wazazi ambao pia wanatabia hivyo,kwa miaka ya nyuma kulikuwa na asilimia kubwa sana lakini kwa sasa kutokana na kukemea kemea vitendo hivi vimepungua,kwa upande wa wanafunzi mtoto anaweza akaanguka chini anapoulizwa katika hali ile anataja baadhi ya watu wanaofanya vitendo hivyo sasa inakuwa ngumu kuthibitisha lakini huwa inakuwa hivyo”alisema Shomari


Festo Mwalongo ni diwani wa kata hiyo ya mlowa amesema kuwa imani za kishirikina hazipo katani kwake pekee bali zipo kila mahali ambazo zinasababishwa na uelewa mdogo kwa baadhi ya jamii na kuwataka walimu waendelee kumtumikia Mungu.


“Habari ya ushirikina sio inaanzia kwenye kata ya Mlowa,sasa hawa watu wachache wanao jihusisha ni kwa kukosa elimu,sasa hivi watu wengi wana nguvu ya Mungu itafika mahala hawa washirikina wataenda nyumba nyingine watateketea kwa moto,sasa sihitaji wakafika mahala wakaanza kutaabika, pamoja na ushirikina huo wawaone wachungaji ili wateketeze huo ushirikina wao”alisema Diwani


Wananchi wa mtaa huo wameitaka serikali kufanyia kazi malalamiko yanayotolewa na wananchi hao juu ya uwepo wa imani hizo za kishirikina kwa kuwa zimepelekea kudidimiza shughuli za kimaendeleo katika mtaa huo.
Share:

RUVU YAKOMAA... AFRICAN LYON,STAND UNITED ZASHUKA DARAJA,MATOKEO YOTE HAYA HAPA

Leo Ligi Kuu Bara Tanzania ilikuwa inafika tamati ambapo mbivu na mbichi zimejulikana kuanzia kwa zile zitakazoshuka daraja.

Bingwa ni Simba ambaye amemaliza ligi akiwa na jumla ya pointi 93.

African Lyon mwenye pointi 23 na Stand United yenye pointi 44 zimeshuka daraja moja kwa moja.

Kagera Sugar ipo nafasi ya 18 ikiwa na pointi 44 ikiwa na tofauti ya mabao ya kufungwa ambapo Stand United wamefungwa jumla ya mabao 50 na Kagera Sugar imefungwa jumla ya mabao 43.

Mwadui FC imemaliza ikiwa nafasi ya 17 hivyo nayo itacheza play of kama Kagera Sugar.

Matokeo ya leo kiujumla ni haya hapa:


FT: Coastal Union 0-0 Singida United.

FT: Mbeya City 0-0 Biashara United.

FT: Mtibwa Sugar 0-0 Simba SC.

FT: Ruvu Shooting 1-0 Alliance FC (Fully Zullu Maganga 25’ p) . 

FT: JKT Tanzania 2-0 Stand United (Samweli Kamuntu 51’, Najimu Maguli 73’).

FT: Ndanda SC 1-3 Mwadui FC (Kigi Makasi : Ottu Joseph 39’, 41’, Salim Aiyee 61’) .

FT: Yanga SC 0-2 Azam FC (Daniel Amoah 45’+2, Mudathir Yahya 50’).

FT: Mbao FC 1-1 Kagera Sugar (Hebert Lukindo 60’ : Ally Ramadhan 20’).

FT: Tanzania Prisons 3-1 Lipuli FC (Benjamini Asukile 29’, Adam Adam 48’, 85’ : Seif Rashid 46’).

FT: African Lyon 0-2 KMC FC (Cliff Buyoya 21’, 17’)
Share:

BOMU LAGUNDULIWA KWENYE GARI KUUZWA KAMA VYUMA CHAKAVU SERENGETI


Picha hii haihusiani na tukio.

Bomu lililokuwa linasafirishwa kutoka Serengeti kwenda Mkoa wa Mwanza kuuzwa kama vyuma chakavu limegundulika katika gari la mfanyabiashara wa vyuma chakavu.

Mfanyabiashara huyo mkazi wa Mugumu Serengeti mkoani Mara, Jonas Marwa anasema wakati anapakia mzigo kwenye gari ndipo alipogundua kuwa kuna chuma ambacho sicho cha kawaida kwenye mzigo huo.

Naye Mkuu wa Polisi wilaya ya Serengeti, Methiew Mgema anasema, "mara baada ya kuona chuma kisicho cha kawaida, mfanyabiashara huyo alikuja kutoa taarifa kituoni na tukaenda kukagua tukabaini kuwa ni bomu".

Mara baada ya kuliteketeza bomu ilo na maafisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kikosi cha 27, Afisa wa Kikosi hicho, Meja Patrick Kitosi ametoa wito kwa wafanyabiashara wa vyuma chakavu na wananchi wote kutoa taarifa pindi wanapoona vyuma ambavyo siyo vya kawaida.

Bomu hilo linalokadiriwa kuwa na uzito wa kilo 10, limeteketezwa hadi mwisho mbele ya maafisa hao wa polisi na jeshi.
Chanzo - EATV
Share:

NYALANDU ASIMULIA JINSI ALIVYOKAMATWA NA KULALA POLISI

Aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amesimulia namna alivyokamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kuhojiwa kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa kwa dhamana leo mchana Mei 28, 2019 na kutakiwa kuripoti polisi kesho.

Nyalandu amesema alikamatwa jana saa 8 mchana akiwa kwenye kikao cha ndani na vijana 29 katika kijiji cha Itaja jimbo la Singida Kaskazini.

Amesema walivamiwa na watu walioanza kuuliza alipo Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Singida, Shaban Lyimo ambaye alisimama na kuwaeleza watu hao kuwa walikuwa katika kikao cha ndani cha Chadema.

“Kwanza walituliza kibali (cha kikao), Lyimo akawajibu kuwa hatuna na ni kikao cha ndani hakihitaji kibali. Wakasema kuwa wao wametoka Takukuru Mkoa wanawahitaji watu wakaninyooshea kidole mimi (Nyalandu) na David Jumbe pamoja na mwenyekiti (Lyimo),” amesema Nyalandu.


Amesema walielezwa kuwa wanahitajika kwa ajili ya mahojiano Singida mjini na walipofika wakaelezwa kuwa wanafuatilia masuala ya rushwa.

“Tulipofika polisi tulihojiwa zaidi ya masaa mawili tukapewa dhamana ilikuwa imefika saa 4 usiku tuliambiwa kwamba twende kisha turudi asubuhi (leo), wakati tukijiandaa kuondoka, mkuu wa kile kituo akapigiwa simu na kutakiwa kufuta dhamana zetu, hivyo tukalala ndani hadi leo.”

“Kwa tunachofanyiwa ni dhahiri watu wanakihofia Chadema ndio maana wanatumika kutubughudhi na kutukatisha tamaa, kwa kuwa wakati tunafanya kikao pale pembeni mwa barabara kulikuwa na wanachama wa chama fulani (akakitaja) wakiwa katika kikao kama chetu lakini huko hawakwenda,” amesema Nyalandu.

Na Gasper Andrew, Mwananchi 
Share:

KUTANA NA CHURA ANAYETAMBUA KAMA UNA UJAUZITO AU LA!

Chura huyo huyu wa Kiafrika aliishi kwa maisha ya amani katika maji tulivu ya kusini mwa jangwa la sahara kwa miaka mamilioni . Hadi katika miaka ya 1930, mwanasayansi wa Kiingereza alipoamua kumdunga sindano ya mkojo, na hapo ndiyo ikawa mwisho wake.

Lancelot Hogben alikuwa ni mtaalamu wa viumbe wa majini aliyekuwa akiwadunga wanyama kwa kemikali mbali mbali, nyingi zikiwa ni za homoni, lengo lake ni kuangalia matokeo yake yatakuwa ni yapi kwa wanyama.

Baada ya kufanya moja ya vipimo hivi vya uchunguzi, aligundua bila kukusudia kwamba homoni za ujauzito zinaweza kusababisha kutungwa kwa mayai miongoni mwa wanyama hawa.Vipimo viligundulika kuwa vilikuwa sahihi kabisa kiasi kwamba kwa miongo miwili iliyofuatia, maelfu ya vyura walidungwa sindano za mkojo wa binadamu

Maureen Symons anakumbuka alipopata matokeo ya ujauzito wake baada ya kupimwa kwa kutumia chura aina ya Xenopus katika miaka ya -1960 .

"Nina picha akilini, nilipimwa walau mara mbili , daktari aliyekuwa amevalia koti jeupe akija kuniambaia akiwa ameridhika , 'una ujauzito - chura ametotoa mayai ',"aliiambia BBC.Kipimo kilikuwa rahisi : Kudunga mkojo ambao haukuchanganywa na kitu chochote chini ya ngozi ya chura jike aina ya Xenopus, halafu unasubiri baada ya saa 5 hadi 12 , na kama ni mjamzito atakuwa ametaga mayai kwa kipindi hicho

Vipimo vya chura aina ya Xenopus havikuwa vinapatikana kwa umma. Vilikuwa vinatunzwa kwa ajili ya matumizi ya dharura, ya kimatibabu - kwa mfano, kutofautisha ukuaji wa kijusi na ukuaji wa uvimbe.

Mimba mbili za Maureen zilikuwa zimetoka, na ni vyura tu walioweza kueleza ukweli.

"Nimegundua sasa kuwa nilikuwa na bahati kufanyiwa vipimo vyote hivi ," anasemaKutokana na umaarufu wake, kulikuwa na vituo maalum vya upimaji wa kutumia vipimo vya vyura aina ya Xenopus

Mwanahistoria wa masuala ya tiba Jesse Olszynko-Gryn wa chuo kikuu cha Strathclyde anasema ingawa wazo lenyewe linaonekana kuwa si la kawaida maskioni mwa watu wa kizazi hiki cha kisasa , kanuni za kimsingi za kipimo ni sawa tu na zile za kipimo cha nyumbani kwa sasa . Kile hasa kilichobadilika vile vile tunavyozungumzia ujauzito.

"Hebu rejea katika miaka ya 1930 na wakati huo ujauzito ulikuwa ni jambo ambalo halikuzungumziwa . Usingeweza kuchapisha neno 'ujauzito ' kwenye gazeti. Lilikuwa ni neno la kibaiolojia sana na lilionekana ni neno ambalo haikuwa la staha."

Alikuri kuwa kipimo hicho kiliweza kusaidia kuelezea jauzito.
Chura anayetafutiwa 'mchumba' BoliviaVipimo vya kisasa vya ujausito havikuweza kuutambua ujauzito hadi ilipofika miaka ya 1990

" Upimaji wa ujauzito ni ubunifu wa utamaduni mpya katika jamii tunazoishi kwa leo ambao kusema ukweli umeweka wazi suala la ujauzito na uzazi pamoja na elimu ya uzali kwa ujumla ."
Vyura hatimae wakaachwa katika maisha yao ya amani wakati vipimo vya kwanza vya ujauzito vya nyumbani vilipopatikana miaka ya 1970. Kwa nini mwezi utabadilika na kuwa mwekundu Jumatatu
Share:

Korea Kaskazini: Tutaendelea kufanya majaribio ya makombora yetu na haturudi nyuma

Serikali ya Korea Kaskazini imesisitiza kwamba, itaendelea kufanya majaribio ya makombora yake na haitorudi nyuma katika suala hilo.

Taarifa iliyotolewa leo na Pyongyang imesema kuwa, kuacha kufanya majaribio ya makombora ya nchi hiyo, kuna maana ya kupuuza haki yake ya kujilinda. 

Kadhalika serikali ya Korea Kaskazini imeyataja kuwa yasiyo sahihi madai ya John Bolton, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani kwamba majaribio hayo yanakiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa. 

Ameongeza kwamba, majaribio ya makombora ya nchi hiyo ni jibu kwa vitisho na mashinikizo ya Washington na washirika wake katika eneo dhidi ya Pyongyang.

Imesema kuwa, imeamua kuanzisha majaribio ya silaha zake kutokana na kitendo cha Marekani cha kutofungamana na ahadi zake kwa ajili ya kuiondolea vikwazo Pyongyang na kadhalika hatua yake ya kufanya mazoezi ya kijeshi katika Rasi ya Korea kwa kushirikiana na waitifaki wake ambao ni Korea Kusini na Japan. 

Hivi karibuni pia serikali ya Korea Kaskazini ilitangaza kuwa Washington inapaswa kubadili siasa zake za upande mmoja kama sharti la kurejea kwenye meza ya mazungumzo kati yake na Marekani. 

Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini ilisema kuwa Pyongyang haitarejea kwenye meza ya mazungumzo iwapo serikali ya Marekani haitafutilia mbali matakwa yake ya upande mmoja katika mchakato wa mazungumzo ya kudhibiti silaha za nyuklia.


Share:

NYALANDU NA WENZAKE WAACHIWA..POLISI WAMTAKA MDOGO WAKE

Jeshi la Polisi mkoani Singida limewatoa mahabusu Lazaro Nyalandu na wenzake wawili, David Jumbe na mmoja aliyetajwa kwa jina la Samson, kwa dhamana pia kutakiwa kuripoti kesho asubuhi. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, Nyalandu, Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii na wenzake, wameachwa leo tarehe 28 Mei 2019 ikiwa ni siku moja tangu walipowekwa mahabusu na jeshi hilo baada ya kukamatwa katika mkutano wa ndani wa chama hicho kwenye Kata ya Itaja, Singida.

Taarifa ya Makene inaeleza kwamba, Nyalandu na wenzake wameachwa kwa dhamana yenye masharti kwa kila mmoja kudhaminiwa na watu wawili na amana ya kiasi cha Sh. 5 milioni kwa kila mdhamini.

Nyalandu ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo kabla ya kujivua uanachama wa CCM na kutimkia Chadema, pia wenzake wametakiwa kuripoti polisi mkoani Singida kesho tarehe 29 Mei 2019 saa tatu asubuhi.

Aidha, taarifa ya Makene imesema Jeshi la Polisi mkoani Singida wamemtaka mdogo wake Nyalandu, anayefahamika kwa jina la Peter Nyalandu kufika kituoni mara moja kwa ajili ya mahojiano ambayo hayajabainishwa.
Share:

Kesi ya vigogo 11 wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) Yapigwa Kalenda

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuendelea kusikiliza kesi inayowakabili vigogo 11 wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) baada ya wakili wa utetezi kuomba muda kupitia jalada.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kukiuka sheria wakati wa ununuzi wa mabehewa 25.

Wakili wa utetezi, Tibita Muganga amedai leo Jumanne Mei 28, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Maghela Ndimbo kueleza kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya usikilizwaji na shahidi yupo.

"Kati shauri hili nashiriki kwa mara ya kwanza baada ya wakili, Malamsha aliyekuwepo awali kujitoa nimeshaanza kazi ya kulipitia jalada ninaomba nipewe muda kidogo kwa ajili ya kumalizia kazi hiyo,” amedai wakili Muganga.

Hakimu Shahidi amekubali ombi hilo na kupanga shauri hilo kusikilizwa Mei 29, 2019 na washtakiwa wapo nje kwa dhamana.

Vigogo hao ni aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa TRL, Kipallo Kisamfu; mkuu wa kitengo cha makenika na mhasibu mkuu, Jasper Kisiraga; kaimu meneja wa usafiri, Mathias Massae; kaimu mhandisi wa ufundi na meneja ujenzi, Muungano Kaupunda na mkuu wa ufundi na meneja ujenzi, Ngoso Ngosomwiles.

Wengine ni mhandisi mkuu wa ufundi, Paschal Mafikiri;  mhandisi mipango,  Kedmo Mapunda;  kaimu mhandisi wa mawasiliano, Felix Kashaingili; mkuu wa usafiri wa reli, Lowland Simtengu; mkuu wa ubunifu na utengenezaji wa nyaraka, Joseph Syaizyagi na kaimu mkuu wa usafirishaji, Charles Ndenge.


Share:

Rais Magufuli atembelea eneo la makaburi ya mashujaa wa Namibia,atembelea kiwanda cha nyama Jijini Windhoek Namibia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Mei, 2019 ametembelea na kuweka shada la maua katika eneo la mashujaa (Heros Acre) waliopigania ukombozi wa Namibia, lililopo nje kidogo ya Jiji la Windhoek nchini humo.

Katika eneo hilo wamezikwa mashujaa wa ukombozi wa Namibia ambao baadhi yao walipata mafunzo katika kambi ya Kongwa nchini Tanzania, wengine walikuwa maafisa wa Chama cha SWAPO ambao ofisi zao zilikuwa Jijini Dar es Salaam na wengine ni viongozi wakuu walioendesha mapambano wakiwa nchini Namibia.

Baadhi ya mashujaa waliozikwa katika eneo hilo ni Ndimo Hamaambo, Peter Nanyemba, Theo-Ben Gurirabo na Toiro ya Toire.

Mhe. Rais Magufuli ameongozana na mwenyeji wake Mhe. Rais Hage Geingob.

Baada ya kutembelea eneo hilo, Mhe. Rais Magufuli ametembelea kiwanda cha nyama cha kampuni Meatco kilichopo Jijini Windhoek na kuelezwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho Bw. Jannie Breytenbach kuwa kiwanda kina uwezo wa kuchinja ng’ombe 630 kwa siku, kimeajiri wafanyakazi 650 na kwamba kampuni hiyo ipo tayari kushirikiana na Tanzania kuanzisha viwanda vya nyama.

Mhe. Rais Magufuli amesema Tanzania ni nchi ya pili kwa idadi kubwa ya mifugo Barani Afrika na ameikaribisha kampuni ya Meatco kuja kuwekeza nchini Tanzania.

Katika ziara hiyo, Mhe. Rais Magufuli ameongozana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.

Kabla ya kuondoka nchini Namibia kwenda nchini Zimbabwe ambako anakwenda kufanya Ziara Rasmi ya Kitaifa kwa mwaliko wa Rais wa Zimbabwe Mhe. Emmerson Mnangagwa, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Pili wa Namibia Mhe. Hifikepunye Pohamba Jijini Windhoek.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Windhoek
28 Mei, 2019


Share:

Iran Yasema haioni uwezekano wa mazungumzo na Marekani

Iran imesema kuwa haioni uwezekano wa kufanya mazungumzo na Marekani. Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za kigeni wa Iran Abbas Mousavi amesema hayo leo, siku moja baada ya rais wa Marekani Donald Trump kusema kuna uwezekano wa makubaliano na Iran kuhusu mpango wake wa silaha za nyuklia. 

Mousavi amenukuliwa na shirika la habari la Fars akisema kuwa Iran haitilii maanani maneno bali kile ambacho ni muhimu kwa Iran na mabadiliko ya namna suala hilo linavyoshughulikiwa. 

Hapo jana, Rais Trump alisema anaamini kuwa Iran itapenda kuwa na makubaliano na anafikiri hilo ni wazo zuri na kuna uwezekano wa hilo kufanyika. 

Mzozo umezidi kuongezeka kati ya Marekani na Iran tangu Marekani ilipozipeleka ndege zake za kivita na silaha nyingine za vita Mashariki ya Kati, na Rais Trump kutangaza mipango ya kuwapeleka wanajeshi 1,500 zaidi katika eneo hilo, hali ambayo imeibua hofu ya vita. 

Marekani ilijiondoa kwenye mkataba wa kimataifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, na ikaongeza vikwazo dhidi ya Iran.


Share:

Dereva Teksi Afikishwa Mahakamani kwa Tuhuma za Kumteka Mo Dewji

Dereva teksi, Mousa Twaleb (46) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne Mei 28, 2019 akikabiliwa  na mashtaka matatu likiwemo la  kumteka mfanyabiashara, Mohamed Dewji ‘Mo’.

Akisomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi kwa kushirikiana na Wakili wa Serikali Simon Wankyo, mshtakiwa anadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mei Mosi mwaka 2018 na Oktoba mwaka huo jijini Dar es Salaam na Johannesburg, nchini Afrika Kusini.

Kadushi amedai mshtakiwa alijihusisha na genge la uhalifu, walimteka Mo katika Hoteli ya Colleseum iliyopo wilayani Kinondoni na kumficha.

Mshtakiwa huyo pia anadaiwa kutakatisha Sh milioni nane ambazo alijipatia huku akijua zinatokana na mazalia ya kosa la uhalifu.

Mshtakiwa huyo hakutakiwa kujibu lolote sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo. Kesi imeahirishwa hadi Juni 11, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.


Share:

MAZOEZI YA KUTUNISHA MISULI YANAATHIRI UWEZO WA KUZAA KWA WANAUME

Wanasayansi wamegundua kuwa baadhi ya wanaume hupunguza uwezo wao wa kupata watoto kutokana na jitihada zao za kutengeneza miili ya kuvutia .

Mazoezi ya kutunisha misuli au kutumia dawa za kuzuia kupata upara zinaweza kuharibu mfumo wa uzazi.

Athari hiyo imetajwa mara baada ya wanasayansi kufafanua madhara hayo.

Wataalamu wanasema kwamba mwanaume anayetumia dawa au anayefanya mazoezi ya kutunisha misuli anaweza kuwa anapata maumivu ya kichwa wakati wa tendo la ndoa na mbegu zake kushindwa kuwa na uwezo wa kuzalisha.

"Nimegundua kuwa baadhi ya wanaume ambao wanakuja kwa ajili ya vipimo miili yao huwa ni mikubwa," alisema Dkt James Mossman, kutoka chuo cha Brown kilichopo Marekani.

Daktari huyo ameiambia BBC kuwa : "Wanaume wanajaribu kutaka kuwa na muonekano mkubwa, huku wanajisababishia madhara ya afya ya uzazi"

"Licha ya kuwa wanajitengeneza wenyewe maumbile yasiyokuwa na uhalisia, lakini wanashindwa kuelewa kuwa wanajiondolea uwezo wao wa kuwa na mbegu za kuzalisha."Dkt. Mossman na Prof Pacey

Miongoni mwa madhara yanayowapata ni homoni zao kushindwa kufanya tendo la kujamiiana kiufasaha kutokana na mazoea yao ya kutengeneza muonekano wa miili yao kuwa chanzo.

Profesa Allan Pacey kutoka chuo chaSheffield ameongeza : " Inashangaza kuona wanaume wanaenda kwenye mazoezi ili kuwa na muonekano mzuri, na mara nyingi lengo ni kuwavutia wanawake na bila kuelewa kuwa wanapunguza uwezo wao wa kuzaa."

Hata hivyo watafiti wanasema kwamba dhana inayofanana na hiyo ya wanaume kutumia dawa ili kutengeneza maumbile yao ina madhara yanayofanana.
Dawa ambazo zinatengeneza maumbile yao na kuzuia nywele zote husababisha madhara katika mfumo wa wa uzazi.

Prof. Pacey aliiambia BBC kuwa : "Ninaweza kusema kuwa kuna wanaume wengi zaidi ya unavyofikiria ambao wanaweza kupata madhara , inaweza kuwa asilimia 90 hivi.

"Mazoezi hayo yanaweza kuongeza tatizo linalofanana kuendelea."

Dkt Mossman amedai kuwa dawa hizo zinaweza kukufanya kuwa na muonekano mzuri wa kuvutia lakini ikakusababishia madhara katika uzazi.

Aliongeza kwamba anadhani kuwa kuna baadhi ambao wanahisi kwamba wanawavutia jinsia nyingine huku wanauwa uwezo wao wa kuzalisha.

Ujumbe mkubwa hapa ni idadi ya vijana wadogo kuwa wahanga wa kuzalisha bado changamoto.
Chanzo - BBC
Share:

DEREVA WA BASI LA ABOOD ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUSABABISHA AJALI


Dereva wa basi la Abood lenye namba za usajili T 269 DBV ambaye jina lake halikufahamika mara moja amenusurika kifo kwa kushambuliwa na wananchi wenye hasira baada ya kugonga pikipiki aina ya Boxer. 

Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mbezi Kwa Msuguri baada ya gari hilo lililokuwa linafukuzana na basi lingine la BM katika barabara mpya na kuigknga pikipiki.

Baada ya tukio hilo dereva wa Abood alishuka kwa lengo la kuangalia kilichotokea, ndipo wananchi walipomvamia na kuanza kumshambulia, kabla ya kufanikiwa kuiombia na kurudi kwenye gari na kujifungia milango.

Hali hiyo ilisababisha usumbufu kwa abiria ambao walikuwa wakitaharuki na kulazikika kutokea madirishani mpaka hapo walipofika polisi na kumuamuru derva kufungua milanho la kutoka nje.

Hakuna aliyefariki katika ajali hiyo, huku abiria wa bodaboda (jina lake halikufahamika) alijeruhiwa kwenye mguu, kichwani na mkononi na amekimbizwa katika hospitaki ya Bochi iliyopo Mbezi kwa Msuguri.
Share:

Trump: Marekani haiko tayari kwa makubaliano ya kibiashara na China

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema nchi yake haiko tayari kufikia makubaliano ya kibiashara na China, lakini anaacha wazi uwezekano wa mataifa hayo mawili siku moja kufikia makubaliano.

Akizungumza jana mjini Tokyo, Trump amesema China iko tayari kufikia makubaliano, lakini Marekani haiko tayari.

Mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa duniani yamekuwa katika mzozo wa kibiashara. Trump anatarajiwa kukutana na Rais wa China, Xi Jinping mwezi ujao katika mkutano wa mataifa yenye nguvu kiuchumi, G20.

Aidha, Trump pia amekutana na Mfalme Naruhito wa Japan katika kasri la kifalme. Mfalme huyo pamoja na mkewe Masako wamemkaribisha Trump, kiongozi wa kwanza wa kigeni tangu Naruhito alipotawazwa hivi karibuni. Trump amekutana pia na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe.


Share:

WAZIRI NDALICHAKO AIPA KAZI NACTE


Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia Prof.Joyce Ndalichako akipokea maelekezo kutoka kwa Mhadhiri wa Chuo Mipango Ezekiel Kanire, juu ya kazi mbalimbali zinazofanywa na Chuo hicho wakati wa maonyesho ya kwanza ya Elimu na mafunzo jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia Prof.Joyce Ndalichako akipokea maelekezo kutoka kwa Mhadhiri wa Chuo Mipango Ezekiel Kanire, juu ya kazi mbalimbali zinazofanywa na Chuo hicho wakati wa maonyesho ya kwanza ya Elimu na mafunzo jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Technologia Prof.Joyce Ndalichako akipokea maelekezo kutoka kwa Mkufunzi wa chuo cha Dare es saalam institute Technology juu ya kazi zinazofanyika chuoni hapo wakati wa maonyesho ya mabanda ya vyuo vya kati jijini Dodoma.
Askari wa kikosi cha zima moto na uokoaji akionyesha namna ya kuzima moto, wakati wa ufunguzi wa wiki ya maonyesho ya kwanza ya Elimu ya ufundi na mafunzo ya nayofanyika Jijini Dodoma.
Msajili wa chuo cha Bandari cha Dar es Saalam wa kwanza kushoto, Jonneo Lugoye akitoa maelezo kwa Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia Prof, Joyce Ndalichako juu ya kazi zinazofanywa na chuo hicho, wakati wa maonyesho kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia, Prof, Joyce Ndalichako katikati akiselebuka pamoja na msanii maarufu Mrisho Mpoto kushoto, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobus Katambi wakati wa ufunguzi wa wiki ya maonyesho ya kwanza ya Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo Jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo Tanzania Adolph Rutayuga, akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Maonyesho Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobus Katambi akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Maonyesho Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Makamu mwenyekiti wa Kamati ya huduma za kijamii, ambaye ni Mbunge wa jimbo la Chemba, Mh, Juma Nkamia akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Maonyesho Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo Bw, John Kondoro akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Maonyesho Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia Pro, Joyce Ndalichako akihutubia mamia ya washiriki wa ufunguzi wiki ya maonyesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia Prof, Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wakati ya ufunguzi wa wiki ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog

......................

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Technolojia Prof. Joyce Ndalichako amelitaka baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi Tanzania, NACTE, kujenga utamaduni wa kuvitembelea mara kwa mara vyuo vilivyo chini ya baraza hilo ili kuhakikisha elimu inayotolewa na vyuo hivyo iwe ya kiwango, ili kufikia malengo ya Serikali.

Prof. Ndalichako ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akifungua maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo, yaliyoandaliwa na baraza hilo yenye lengo la kuvikutanisha vyuo vilivyochini ya balaza hilo.

Amesema ni lazima NACTE ijenge utamaduni wa kuvitembelea vyuo hivyo ili viweze kutoa mafunzo bora yatakayo saidia katika mkakati wa Serikali na kufikia malengo ya ujenzi wa Tanzania ya viwanda.

Amesema kama vyuo hivyo hazitatoa elimu na mafunzo bora lengo la kufikia nchi ya viwanda halitafanikiwa, ni wajibu wa baraza hilo kuhakikisha inasimamia utoaji wa mafunzo yaliyo bora.

“Pia niwatake ninyi baraza kama walezi wa hivi vyuo hebu mjenge utamaduni na tabia ya kuvitembelea vyuo hivyo vilivyochini yenu angalau vitoe elimu bora, kataka kufikia malengo ya serikali kufikia nchi ya viwanda, na tutafikia kwa kuhakikisha vyuo hizi vinatoa mafunzo bora” amesema Prof. Ndalichako.

Pia amesema serikali haitasita kukifungia chuo chochote kitakachokutwa kinaendeshwa kinyume na ithibati iliyotolewa na serikali, kwani itakuwa ni kinyume na taratibu zilizowekwa na serikali.

Pia amevitaka vyuo hivyo kutumia maonyesho kubadilishana mawazo, na namna ya kutoa mafunzo bora na kukuza ushirikiano baina ya taasisi, wadau wa maendeleo pamoja na waajiri mbalimbali katika kuuza sekta hiyo.

Amesema katika kuhakikisha elimu hiyo inakuwa serikali kupitia wizara hiyo imetenga kiasi cha milioni kumi na nane(18,000,000) kujenga chuo kikubwa cha ufundi jijini Dodoma kitakachosaidia kukuza elimu ya ufindi, pia imetengwa bilion arobaini kujenga vyuo vingine ishirini na tano (25) maeneo mbalimbali.

Sambamba na hilo serikali imepanga kukarabati vyuo hamsini na nne(54) vya ufundi ili kufikia kutoa mafunzo yaliyobora, na kuongeza udahili wa wanafunzi wa ufundi mbalimbali hapa nchini.

Kwa upande wake katibu mtendaji wa NACTE Adolph Rutayuga amesema tangu kuanzishwa kwa baraza hilo mwaka 1997 na kuanza rasmi kazi zake mwaka 2001 wamefanikiwa kudhibiti uanzishwaji wa vyuo vya ufundi kiholela.

Amesema jumla ya vyuo vyote ni mia tano arobaini(540) na kati ya hivyo mia mbili hamsini na moja ni vya umma na mia tatu kumi na tisa na vya binafsi na kati ya hivyo vyuo ishirini na moja havikukidhi matakwa na vilifutwa kabisa usajiri wake.

Maonyesho hayo yatakayo dumu kwa siku tano yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma, umebebwa na kauli mbiu isemayo “Elimu ya ufundi na mafunzo kwa maendeleo ya uchumi wa viwanda Tanzania”.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger