Monday 29 April 2019

Rais Magufuli azindua kiwanda cha Maparachichi

Rais Magufuli amezindua kiwanda cha Maparachichi Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya ambapo amewaahidi wawekezaji wa Kiwanda hicho kurejesha VAT zinazodaiwa na wawekezaji baada ya  zoezi la uhakiki kukamilika.

Amesema, Serikali ilizuia kurejesha fedha hizo kutokana na wawekezaji wengi waliwasilisha madeni hewa na hivyo kuisababishia Serikali hasara kubwa.

Aidha Rais Magufuli amemuomba mwekezaji huyo kuwafikiria wakulima kuhusu suala la nyongeza ya bei ya zao lao pamoja na mshahara kwa wafanyakazi. 

==>>Msikilize hapo chini


Share:

CCM yavuna wanachama wapya 500 Dar es Salaam

Na MWANDISHI WETU
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Rodrick Mpogolo, amewapokea wanachama wapya wa chama hicho kupitia kampeni ya Dar ya kijani inayoratibiwa na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam.

Kampeni hiyo ya Dar ya Kijani ina lengo la kurudisha mitaa, kata na majimbo yote katika himaya ya chama, inawataka vijana na wanachama wote kuimarisha ushirikiano na kupata ushindi wa pamoja wenye heshima kwa chama hicho tawala.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwa Wilaya ya Kinondoni, Mpogolo, amewataka vijana kuwa makini na waadilifu kwani wao ndio wataokaojenga hehima ya chama na Taifa kwa ujumla.

“Vijana ndio tunao wategemea katika uchaguzi ujao tunahitaji vijana makini na waadilifu ambao watakitumikia chama chetu cha Mapinduzi na Serikali yetu. jiepushieni mbali na tabia ambazo zitawaondelea maadili yenu. Ili mkawe viongozi makini kwani taifa letu linaitaji viongozi makini na wachapakazi .

Amesema yeye hatoita Dar ya Kijani ila anaitambua Tanzania ya Kijani kutokana na kaz kubwa inayofanywa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi ya kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli.

“Mimi sitaita Dar es Salaam ya Kijani bali nitaita Tanzania ya Kijani kwa sababu Rais wetu mpendwa Dk. John Magufuli anafanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo nchini, tunaona ujenzi wa barabara za juu pale Ubungo na tunashuhudia maendeleo makubwa yanayofanywa katika sekta ya elimu vituo vya afya, kuwasaidia wamachinga kwa kuwapa vitambulisho vya ujasiriamali, bodaboda.

“Pia ameleta usawa kwa Watanzania wote kuwa sawa. Kwahiyo kwa namna hii lazima chama chetu kiendelee kushika hatamu kwa sababu tunawatumikia wananchi ipasavyo kwa namna hii nina uhakika Tanzania inaenda kuwa ya kijani,” amesema Mpogolo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, amesema kuwa lengo la kampeni hiyo ya Dar es Salaam ya Kijani ni kuwaandaa vijana na chaguzi zijazo ikiwamo wa Serikali za Mitaa mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 ili chama hicho kipate ushindi wa kishindo.

“Lengo la Dar es salaam ya Kijani ni kuwaanda vijana wa Mkoa wa Dar es salaam katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa lakini kuwataka vijana kuhakikisha wanajitokeza katika kugombea nafasi lakini pia kuhakikksha CCM kinapata ushindi wa kishindo kwa mkoa wote,” amesema Kilakala

Amesema tangu kampeni hiyo ilipozinduliwa Machi 17, mwaka huu jijini Dar es Salaam imefanikiwa kuvuna zaidi ya wanachama 500  ambao wamejiunga na chama hicho


Share:

Serikali Yazungumzia Dawa za Kuongeza Nguvu za Kiume

Suala la matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu za kiume na makalio limeibuka bungeni huku Waziri wa Ulinzi, Dkt.Hussein Mwinyi akiwataka watanzania wanaotaka kutumia huduma hiyo kufuata taarifa rasmi kabla ya matumizi.

Awali swali hilo liliulizwa na Mbunge wa Viti Maalum, Rukia Kassim ambaye alihoji juu ya Serikali kuzifungia saluni ambazo zinatoa huduma ya kutumia dawa na kuongeza makalio na kubandika kucha bandia.

"Wanawake wengi wameathirika sana kwa dawa za kuongeza makalio, kope na kucha bandia, je Serikali iko tayari kuzifunga saluni zinazofanya hivi?", aliuliza  Mbunge huyo.

Akijibu swali hilo kwa niaba ya Wizara ya Afya, Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi amesema, "TFDA haijawahi kupokea taarifa ya madhara kuhusiana na kucha za kubandika, kukosekana kwa takwimu hizo Serikali haina sababu ya kufunga saluni, wala kuwachukulia hatua watoa huduma".

Kwa upande wa Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga, aliyehoji juu ya kuongezeka kwa matumizi ya dawa za kuongeza nguvu za kiume hususani kwa vijana.

"Tunatambua kuna dawa maalum zilizopitishwa kwa ajili ya kuongeza nguvu za kiume, ushauri wetu ni kwamba  wanaotaka kutumia dawa hizi, wakatumie dawa ambazo zimethibitishwa na wataalam ambazo hazina madhara", amesema Waziri Mwinyi alipokuwa akijibu swali la Mbunge Mlinga.


Share:

Serikali Kuendelea Kulinda Uhuru wa Kuabudu

Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema Serikali itaendelea kulinda uhuru wa kuabudu kwa mujibu wa Katiba huku akiwapongeza Watanzania namna wanavyotumia uhuru huo bila kuuvunja.

Pia ameahidi kuwa Serikali itandelea kushirikiana na dini pamoja na madhehebu yote kwa sababu ni taasisi nyeti na muhimu katika jamii kwa sababu zinasaidia kuwafanya wananchi kuwa raia wema.

Ameyasema hayo  jana Aprili 28, 2019 katika misa ya kumsimika Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga wa kanisa katoliki Jimbo Kuu la Mbeya iliyofanyika katika viwanja vya Sokoine na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Alisema amefurahi kuona katika misa ya kumsimika askofu Nyaisonga kuhudhuriwa na viongozi kutoka madhehebu mbalimbali huku akiamini pia wahudhuriaji ni kutoka sehemu tofauti.


Share:

Kujichua Kwa Muda Mrefu Husababisha Maumbile ya Kiume Kusinyaa na Kupungukiwa Nguvu za Kiume

Wanaume  wengi  waliofanya  mchezo wa  kujichua  kwa  muda  mrefu hupatwa  na  madhara  ya kuwa  na  kusinyaa  na  kudumaa  kwa  maumbile  yao  ya  kiume  ambayo  huenda  pamoja  na  tatizo  a  Ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume.

Tendo  la  kujichua  kwa  mwanaume  linapofanyika  kwa  kipindi  kirefu huathiri na  kuharibu mishipa  na  misuli  ya uume  na  hivyo  kusababisha  kujengeka  kwa mafuta na tishu zisizo vutika  kwenye  mishipa  ya  ateri.  Jambo  hili  husababisha  makuu mawili; 1. Huzuia  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  kuongezeka jambo  linalotajwa  na  wanasayansi  kama jambo  muhimu  sana  katika  kukua  kwa  uume. 2. Huzuika  kutirika  kwa  damu  kuingia  kwenye  misuli  ya  uume.

Mambo  hayo  mawili  huathiri  sana  ukuaji  wa  maumbile ya kiume  kwa  sababu  yanapo tokea huathiri uzalishaji  wa  homoni  muhimu  zinazo  husika  na  ukuaji  wa  misuli  ya  uume na matokeo  yake husababisha  uume  wa  mhusika  kudumaa, kusinyaa,kunywea  na  kurudi ndani  kiasi  cha  kuufanya  uonekane  kama uume  wa  mtoto.
 
Hii ndio  sababu  kwanini watu  wengi  walio athirika  na  punyeto  hulalamika  kwamba  maumbile  yao  ya  kiume  hayajaongezeka  tangu  walipo anza  kujihusisha  na  punyeto  wakiwa  na  umri mdogo. 

Maumbile  yao  huonekana  kama  ya  watoto  kwa  sababu hayakupata  nafasi  ya  kupokea  vichochea  vya  kuyafanya  yakue  na  kuongezeka  tangu  walipo  anza  kujihusisha  na  punyeto.

Suluhisho  La  Tatizo La Maumbile  Ya  Kiume  Yaliyo  Sinyaa  Kwa  Sababu  Ya  Punyeto.
Kama  bado  unaendelea  kujihusisha  na punyeto  basi  jitahidi  uache  tabia  hiyo  mara  moja  kwani  inakuharibu. Inaweza  isiwe  rahisi  sana  kuacha  mara  moja  lakini  ukiweka  nia  thabiti  basi  unaweza  kuacha  kabisa  kama  walivyofanikiwa  kuacha  wengine  ambao  walikuwa  wametopea  kwenye  tabia  hiyo  lakini  wakajitahidi  kujilazimisha  na  hatimaye  wakafanikiwa  kuachana  kabisa  na  tabia  hiyo.

==>> Acha kuangalia video chafu za ngono.
Video hizi ndio chanzo kikuu cha punyeto kwa watu wengi hua zinajenga picha nyingi kwenye ubongo na kila picha unayoiona utataka ukaipigie  punyeto hivyo kuacha kuziangalia tu ndio nafuu yako.. 


Weka mipango ya kuzuia kupiga punyeto wakati wa kuoga: bafuni ndio sehemu ambayo inatumika sana na watu wengi kupiga punyeto hivyo ni vizuri kua na mikakati ya kujizuia ukiwa huko kwa kuoga haraka na kuondoka, kuoga maji ya baridi ambayo mara nyingi hayatoi muhemko wa kupiga punyeto.

==>>Epuka kukaa nyumbani peke yako;
Mara nyingi kukaa peke yako kunakufanya ushawishike kufanya tendo hilo, hebu ondoka na ujichanganye na watu wengine au tafuta majirani wa kukaa na kuongelea mambo mengine. 


Fikiria kuhusu madhara yake: kila aliyewahi kupiga punyeto kuna madhara mabayo ameshayapata kama vile misuli ya uume kulegea, kushindwa kurudia tendo uwapo na mwenzi wako, kuishiwa nguvu za kiume, maumbile kusinyaa, kurudi ndani na kuwa kama ya mtoto mdogo.

Acha kusema eti hii punyeto ni ya mwisho: siku zote wapiga punyeto wana akili moja ya kufikiria eti sasa leo napiga afu sirudii tena. Hicho kitu hakipo, kwani kesho yake utasema hivyohivo, kama unaacha acha mara moja ili utunze heshima yako mbele ya mwenzi au mke wako.

Kama utaona  kuna  ugumu  wa  kuacha  tabia  hiyo  na tayari ushaapata madhara ya maumbile kusinyaa na kupungiwa nguvu za kiume, basi  wasiliana nasi kwa ushauri zaidi; Simu  0716-263605


Share:

Jinsi ya Kumtambua Mpenzi Tapeli na Muongo

Inawezekana upo katika uhusiano na tapeli wa mapenzi bila kujua, hiyo ni sumu na unachotakiwa kufanya sasa ni kuanza kumchunguza mpenzi wako mapema isije kuwa upo kwenye foleni!

Hakuna kitu kibaya kama kuwa katika foleni ya wapenzi kwa mpenzi mmoja, tena mbaya zaidi awe ni yule ambaye moyo wako umempenda kwa dhati.

Kumbuka, kuwa katika uhusiano na mtu ambaye haeleweki ni sawa na kukaribisha matatizo katika maisha yako, huna sababu ya kuishi kwa wasiwasi ukiwa hujui mpenzi wako anakuchukulia vipi.

Anza kumuwekea mitego mapema. Lakini katika mitego yako achana na simu yake kabisa, huna sababu ya kuchunguza simu yake lakini kama ni msaliti utajua tu, unafikiri atajificha mpaka lini?

Atafanya mambo yake gizani mpaka lini? Kuna siku utagundua na kumuacha aendelee na umalaya wake kama ameona ndiyo maisha. Usikubali kabisa kuwa katika penzi la kitumwa, penzi la kisaliti, kuwa na mtu ambaye anakuchanganya wa kazi gani zaidi ya kukupotezea muda na kukukaribishia machozi?

UTAMJUAJE MPENZI LAGHAI?
Hapa ndipo kwenye kazi, kwa bahati mbaya sana kama ikitokea ukampenda mtu sana hata kama akifanya mabaya kiasi gani unaweza usiyaone, kama wewe ni wa aina hii unapaswa kubadilika kifikra. Mwone wa kawaida, fanya uchunguzi wako polepole na kama ukiona moja kati ya mambo yafuatayo, ujue kuna kitu.

(a) Hataki ujulikane na rafiki zake
Hii ni kati ya alama walizonazo matapeli wa mapenzi, ni mtu wa kufanya mambo kwa upekee sana. Kila dakika hakaukiwi na neno nakupenda sana, lakini moyoni mwake hakuna alama hata moja ya mapenzi kwako.

Ni vigumu kumtambua mtu wa aina hii lakini chunguza kuhusu hili, hapendi kabisa kukukutanisha na rafiki zake na hata mkikutana nao kwa bahati mbaya basi hatakutambulisha na kama akikutambulisha hatakutambulisha kama mpenzi wake rasmi. Ataishia kusema ninyi ni marafiki mlioshibana!

Tangu lini mpenzi akatambulishwa kama rafiki? Mtu anapomtambulisha mpenzi wake humtambulisha kwa kujisikia furaha moyoni kwamba anamtambulisha mpenzi wake lakini inakuwaje kwako akutambulishe kama rafiki?

Baadaye utakapomuuliza hawezi kuwa na jibu la maana, atabaki kukuambia hata kama akikutambulisha kama rafiki jamaa ataelewa kuwa ni mpenzi wake, hii inaingia akilini kweli?

Hakuna ukweli kama huo ndugu zangu! Huo ni ulaghai na anaogopa kukutambulisha kama mpenzi maana tayari ameshaonwa akiwa na wapenzi wengine. Sasa kama ndivyo, atatambulisha wangapi? Aseme wewe ni nani? Amka ndugu yangu!

(b) Msiri kupitiliza
Hii ni alama nyingine waliyonayo wanaume wa aina ninayoielezea katika mada hii. Siku zote mambo yake ni kwa siri kubwa, kama mna ahadi ya kukutana, hataki muongozane, atakuambia mkutane moja kwa moja sehemu husika. Hata muda wa kuondoka atafanya kila njia ili kila mmoja aondoke mwenyewe na kama mkiondoka pamoja basi ujue ni usiku na hakuna atakayewaona.

Ikitokea akakubali kuongozana na wewe, hatapenda muongozane pamoja. Atalazimisha utangulie mbele yeye afuate nyuma, kwa nini? Kwa sababu anaogopa kujulikana kuwa yeye ni mpenzi wako na kama anaogopa anakupenda kweli? Mapenzi gani hayo yanafanywa kwa siri? Anakupotezea muda huyo.

(c) Hapendi ndugu wafahamiane
Mpenzi wa aina hii ni mjanja sana, kwanza kabisa atajifanya mtu mwenye ‘ubize’ sana, yote hii ni kukwepa kuwajua ndugu zako au wewe kuwajua ndugu zake! Wakati mwingine anakuwa hapendi ndugu zako na wake wakutane wakijua wazi kuwa nyie mna uhusiano, hili ni tatizo.

Hakuna uhusiano wenye heri na malengo ya kuishi pamoja siku zijazo ukawa wa kificho cha kiasi hicho. Kama ana nia na wewe basi atahakikisha anawafahamu baadhi ya ndugu zako na wewe unawafahamu baadhi ya ndugu zake, hayo ndiyo mapenzi ya kweli.

Mapenzi hayaishii kwa nyie wawili pekee bali hata kwa ndugu zenu. Mnapojuana inakuwa rahisi kusaidiana hata katika mambo mengine ya kawaida.

MWILI wako  una thamani kubwa sana, usiidharau jinsi yako, usijishushe kiasi hicho, huyo anayekupotezea muda na kukuchezea sasa hivi hana thamani kama huyo aliyeandaliwa kwa ajili yako. 

#Pakua App Yetu tukuhabarishe, Sasa Tumerudi Upya




Share:

Kuwa Wakwanza Kupokea Habari Zetu....Download App Yetu Kwa Kubonyeza Hapa, Huhitaji tena kuwa na Computer

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.



Share:

Mkuu wa Wilaya Amtia Ndani Mwenyekiti wa Kijiji Kwa Kutafuta Mamilioni ya Mradi wa REA

Na Ahmed Mahmoud,Longido
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ewor ndeke katika kata ya Kimokokua wilaya ya Longido, Moses Lesikar Leng’ese  Ole Nasuaku, anashikiliwa na jeshi la Polisi wilayani humo kwa amri ya Mkuu wa wilaya hiyo akituhumiwa kujipatia kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 135 zilizolipwa na wakala wa umeme vijijini Rea kama fidia ya kupisha usambazaji wa umeme.

Akiongea na vyombo vya habari Mkuu wa wilaya hiyo ,Frank Mwaisumbe amesema hatua hiyo imekuja kufuatia malalamiko ya wananchi wa kijiji hicho wakimtuhumu mwenyekiti wao kujipatia mamilioni ya fedha kupitia mradi wa Rea baada ya kudanganya  kuwa maeneo yanayopitiwa na mradi huo ni mali yake wakati si kweli.

Mwaisumbe alifafanua kuwa mwenyekiti huyo alilipwa mara mbili akitumia majina tofauti ,ambapo alilipwa kiasi cha sh,milioni 66 kwa hekari saba na sh,milioni 69 kwa hekari 10 huku akitumia majina ya Lesikar Leng’ese na Moses Leng’ese na kujipatia kiasi hicho cha fedha.

Alisema kuwa kabla ya kutiwa mbaroni kwa mwenyekiti huyo Wanakijiji saba waliohojiwa ,watano walidhibitisha  maeneo hayo ni ya kijiji huku wawili ndio walisema ni Mali ya mwenyekiti huyo anayemiliki tangu mwaka 2013 ,ingawa hatua ya upimaji maeneo ya mradi  ilishapita tangu mwaka ,2008 .

“Ni kweli tumemkamata kwa kosa la kujipatia fedha kinyume cha SHERIA na kosa hilo ninaangukia kwenye uhujumu uchumi ,nimempa siku saba arejeshe fedha hizo na baada ya hapo tutampeleka mahakamani” Alisema Mwaisumbe

Aliwataja wengine waliotumia mpango huo  kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia maeneo hayo ya Kijiji ambao wanatafutwa ni pamoja na Elia Shapashina Kool   na Luka Sambeke Ole Mboloso

Wengine ni mwenyekiti wa kitongoji cha Maatiani aliyetambulika kwa jina moja la Kerimboti ,Sindiyo Leakui na Nengolo Sadaka wote wakazi wa Kijiji cha Ewor ndeke.

Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa fedha hizo zimelipwa wiki tatu zilizopita kama fidia kwa maeneo yaliyopitiwa na mradi huo wa Rea baada ya kupimwa na kuthaminishwa   mwaka 2008 ambapo fedha hizo ziliopaswa kuwekwa kwenye akaunti ya Kijiji lakini mwenyekiti huyo na wenzake walitumia akaunti binafsi kujinufaisha.

Wakati mkuu huyo wa wilaya akichukua hatua hiyo wananchi wa Kijiji hicho wakiwemo wanawake wametishia kufunga ofisi ya kijiji hicho kama njia pekee ya kushinikiza kiongozi huyo kuachia ngazi .

Mmoja ya wananchi wa Kijiji hicho, Mbayo Olotito alisema kuwa mwenyekiti wao amekosa uaminifu  kwa muda mrefu na wanajipanga kupeleka kilio chao kwa mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ili kushinikiza kuweza kuchukuliwa hatua zaidi kwa mwenyekiti huyo na wenzake walioshiriki kuhujumu maeneo ya Kijiji na kujinufaisha wenyewe.

“Huyu mwenyekiti kwa muda mrefu amekuwa akichochea migogoro ya Ardhi kwa wananchi na kujinufaisha ” Amesema Olo Tito.


Share:

WATU 27 WAFARIKI DUNIA KWA KUNYWESHWA JIK NA MCHUNGAJI KANISANI



Jinsi JIK ilivyotumika

Watu takriban 27 wamefariki dunia baada ya mchungaji Rufus Phalawa kanisa la kilokole la 'AK Spiritual Christian Church' lililopo Limpopo nchini Zambia, kuwanywesha dawa ya kuondoa madoa 'jik' wakiwa kanisani.

Taarifa kutoka Zambia zilizochapishwa na jarida la Zambia Observer, zinasema kwamba mchungaji Phala aliwaambia waumini wake kuwa jik hiyo inaondoa mapepo, hivyo akaanza kuwanywesha kwa nia ya kuwaombea mapepo yao yaondoke.

Licha ya vifo hivyo, pia waumini wengine 18 hali zao si nzuri, na bado wapo hospitali wakipatiwa matibabu.

Polisi wa Limpopo wameanza uchunguzi juu ya tukio hilo, huku wakioneshwa kushangazwa kwao, ambapo miongoni mwa waliofariki, wapo wauguzi wa afya na walimu.

Source: Zambia Observer 

Share:

SERIKALI YAFUNGUKA KUHUSU DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME NA MAKALIO


Suala la matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu za kiume na makalio limeibuka bungeni huku Waziri wa Ulinzi, Dkt.Hussein Mwinyi akiwataka watanzania wanaotaka kutumia huduma hiyo kufuata taarifa rasmi kabla ya matumizi.

Awali swali hilo liliulizwa na Mbunge wa Viti Maalum, Rukia Kassim ambaye alihoji juu ya Serikali kuzifungia saluni ambazo zinatoa huduma ya kutumia dawa na kuongeza makalio na kubandika kucha bandia.

"Wanawake wengi wameathirika sana kwa dawa za kuongeza makalio, kope na kucha bandia, je Serikali iko tayari kuzifunga saluni zinazofanya hivi?", aliuliza Mbunge huyo.

Akijibu swali hilo kwa niaba ya Wizara ya Afya, Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi amesema, "TFDA haijawahi kupokea taarifa ya madhara kuhusiana na kucha za kubandika, kukosekana kwa takwimu hizo Serikali haina sababu ya kufunga saluni, wala kuwachukulia hatua watoa huduma".

Kwa upande wa Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga, aliyehoji juu ya kuongezeka kwa matumizi ya dawa za kuongeza nguvu za kiume hususani kwa vijana.

"Tunatambua kuna dawa maalum zilizopitishwa kwa ajili ya kuongeza nguvu za kiume, ushauri wetu ni kwamba wanaotaka kutumia dawa hizi, wakatumie dawa ambazo zimethibitishwa na wataalam ambazo hazina madhara", amesema Waziri Mwinyi alipokuwa akijibu swali la Mbunge Mlinga.
Share:

Video Mpya ya Masanja Mkandamizaji – NII

Video Mpya ya Masanja Mkandamizaji – NII


Share:

Profesa Lipumba Afanya Uteuzi wa Viongozi Mbalimbali CUF

Chama Cha Wananchi (CUF) kimewateuwa wanachama 13 kushika nafasi mbalimbali za uongozi ili kusaidia kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, aliwaeleza waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa, wameteua wanachama ambao miongoni mwao ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.

Wanachama walioteuliwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi, Zainab Mndolwa na naibu wake, Omar Mohammed Omar, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, Bunge na Sera, Mohammed Habibu Mnyaa na naibu wake, Mohammed Ngulangwa.

Wengine ni Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Mneke Jafar na naibu wake, Mohammed Vuai Makame, Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma, Abdul Kambaya na naibu wake, Mbarouk Seif Salim.

Wengine ni Haroub Mohammed Shamis aliyeteuliwa Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria, naibu wake Salvatory Magafu wakati Thinney Juma Mohammed akiteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mafunzo na Uhamasishaji na naibu wake, Masoud Omary Mhina.
 

Profesa Lipumba alisema Kamati ya Uongozi imemteua Yusuph Mohammed Mbugiro kuwa Ofisa Tawala wa ofisi kuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti huyo wa CUF pia amefanya uteuzi wa viongozi wa jumuiya za chama huku akisema viongozi hao watakaimu nafasi zao mpaka pale watakapochaguliwa kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali ameteuliwa kuwa kaimu mwenyekiti Jumuiya ya Vijana wa CUF (Juvicuf), makamu wake Faki Suleiman Khatib na kaimu Katibu Mtendaji, Yusuph Kaiza Makame na naibu wake, Mbaraka Chilumba.

Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (Jukecuf) ni Dhifaa Mohammed Bakar na makamu wake ni Kiza Mayeye, kaimu Katibu Mtendaji ni Anna Ryoba na naibu wake ni Leila Jabir Haji.

Kwa upande wa Jumuiya ya Wazee wa Cuf (Juzecuf), kaimu mwenyekiti ni Mzee Chunga na makamu wake ni Hamida Abdallah, kaimu katibu mtendaji ni Hamis Makapa na naibu wake ni Said Ali Salim.


Share:

Iran: Marekani lazima iombe idhini kwa jeshi la Iran la SEPAH kuweza kupita Hormuz

Mkuu wa Majeshi ya Iran amesema kuwa meli za Marekani haziwezi kupita katika Lango Bahari la Hormuz bila ya kuomba idhini kwanza kutoka kwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH.

Meja Jenerali Mohammad Baqeri amewaambia waandishi wa habari kwamba hakuna mabadiliko yoyote yaliyotokea hadi hivi sasa kuhusu meli za kivita, za kibiashara na za mafuta na vyombo vyote vya majini vya Marekani vinavyopita kwenye Lango Bahari la Hormuz. 

Wakati wowote vinapoamua kufanya hivyo lazima viombe idhini kwanza kutoka kwa jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ndipo vinaweza kupita baada ya kuruhusiwa na jeshi hilo.
 
Amesema Iran inataka lango hilo libakie wazi na salama na kuonya kuwa Tehran haitoruhusu mtu yeyote kuhatarisha usalama wa eneo hilo. 

Itakumbukuwa kuwa karibu thuluthi nzima ya mafuta yanayotumika maeneo mbalimbali duniani yanapitia katika Lango Bahari la Hormuz la nchini Iran. 

Jukumu la kulinda usalama wa eneo hilo muhimu mno kiistratijia ni la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ambalo hivi karibuni rais wa Marekani Donald Trump alidai kuwa  jeshi hilo ni taasisi ya kigaidi.

Mkuu huyo wa vikosi vya ulinzi vya Iran ameongeza kuwa, madhali meli za nchi nyingine zinatumia lango hilo kusafirisha mafuta, Iran nayo ni haki yake kabisa kutumia eneo lake hilo kusafirishia mafuta. 

Hata hivyo amesema hii haina maana kwamba Iran inakusudia kulifunga lango hilo. 

Amesema: "Hatuna nia ya kulifunga Lango Bahari la Horumuz isipokuwa kama adui atatulazimisha kufanya hivyo. Na tukiamua kulifunga, basi tunao uwezo wa kufanya hivyo muda wowote ule."

Credit: Parstoday


Share:

LIVE: Fuatilia kipindi cha maswali na majibu kutoka Bundeni Dodoma

LIVE: Fuatilia kipindi cha maswali na majibu kutoka Bundeni Dodoma


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya April 29




Share:

Sunday 28 April 2019

Picha : RAIS MAGUFULI NA MKEWE WASHIRIKI IBADA YA KUSIMIKWA KWA ASKOFU NYAISONGA KUWA ASKOFU MKUU WA JIMBO KUU KATOLIKI MBEYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimpongeza Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga mara baada ya kusimikwa kuwa Mkuu wa Jimbo hilo. PICHA NA IKULU
Mke wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli Mama Janeth Magufuli akimpongeza Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga mara baada ya kusimikwa kuwa Mkuu wa Jimbo hilo.
Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo akiongoza Ibada ya kumsikima Askofu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya katika Ibada iliyofanyika katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga akiwa amekaa kwenye kiti wakati Ibada ya kusimikwa kwake ikiendelea katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga akisalimiana na Mapadre wa Kanisa Katoliki mara baada ya kusimikwa Rasmi kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga akiwa ameketi kwenye Kiti cha Uaskofu pamoja na Maaskofu wengine wa Kanisa Katoliki nchini.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga akipongezwa na Maaskofu mbalimbali wa Kanisa Katoliki mara baada ya kusimikwa Rasmi.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga akiwa amekaa kwenye kiti wakati Ibada ya kusimikwa kwake ikiendelea katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikusanya Sadaka kwa waumini mbalimbali waliokusanyika katika uwanja wa Sokoine katika ibada ya Kumsimika Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger