Tuesday 22 January 2019

MAKONDA,GWAJIMA USO KWA USO

Josephat Gwajima (kushoto) na Paul Makonda (kulia).

Katika mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es salaam , RC Makonda alisimsimamisha Askofu Gwajima Mbele ya Rais John Pombe Magufuli ambae ni mgeni rasmi.

"Nimemuona rafiki yangu Gwajima hapa, simama kidogo wakuone", amesema Makonda na baada ya Askofu Gwajima kusimama, ukumbi mzima ulikaripuka kwa shangwe.

"Mimi na yeye tuna historia ndefu kidogo, wameninoa wengi kuanzia enzi za umoja wa vijana, kwa hiyo kama kuna mapambano, unaweza kunituma tu", ameongeza Makonda.

Ikumbukwe kuwa wawili hao walizua gumzo mwanzoni mwa mwaka uliopita kutokana na suala la uhalali wa elimu ya Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es salaam, ambapo Askofu Gwajima alitumia mikutano yake mingi kuelezea jinsi alivyokuwa akimfahamu.

Chanzo:Eatv
Share:

MAKONDA AMUOMBEA LISSU MSAMAHA KWA SPIKA

Share:

Ripoti : MABILIONEA 26 DUNIANI WANA UTAJIRI SAWA NA NUSU YA MASKINI DUNIANI

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la hisani la kimataifa la Oxfam, inaonyesha kuwa mabilionea 26 duniani wanamiliki utajiri ulio sawa na nusu ya binadamu maskini zaidi duniani, na kutaka matajiri watozwe kodi zaidi.

Ripoti hiyo ya Oxfam imetolewa Jumatatu januari 21, 2019, kuelekea kongamano la kimataifa la kila mwaka la kiuchumi litakalofanyika mjini Davos Uswisi. Ripoti hiyo pia inasema mabilionea duniani wameshuhudia utajiri wao ukiongezeka kwa dola bilioni 2.5 kwa siku mwaka 2018.

Watu bilioni 3.8 walio chini ya kiwango, utajiri wao ulishuka kwa asilimia 11 mwaka jana, kwa mujibu wa Oxfam. Shirika hilo limesisitiza kuongezeka kwa pengo baina ya matajiri na maskini, linalochangia kuzorotesha mapambano dhidi ya umaskini, kuharibu uchumi na kuchochea hasira ya umma.

Tajiri namba moja duniani ambaye ni mkurugenzi wa Amazon Jeff Bezoz aliongeza utajiri wake hadi dola bilioni 112 mwaka jana, ambapo asilimia moja ya utajiri wake ni sawa na bajeti nzima ya afya ya Ethiopia, nchi iliyo na wakazi milioni 105. 

Mkurugenzi wa Oxfam Winnie Byanyima ametoa akisema, "Watu matajiri duniani, watu walio na nguvu duniani, viongozi wa kisiasa duniani ni lazima wachukue hatua za kupunguza pengo la usawa kwasababu limekithiri. Watu wanaoshiriki kongamano la Davos, viongozi wa makampuni makubwa na viongozi wa kisiasa nao ni sehemu ya tatizo.

 Tunawataka waje na suluhisho la kupunguza pengo la usawa, ambalo linazidi kuwa kubwa, linaumiza uchumi, na kudhoofisha demokrasia, hivyo ninatoa wito wa kuchukuliwa hatua ."

Oxfam imeonya kwamba serikali zinazidisha kukosekana usawa kwa kutoboresha huduma za umma kama vile huduma za afya na elimu wakati huo zikiwatoza matajiri kodi kidogo.

Wataalamu wa Oxfam wamekiri kwamba idadi ya watu maskini duniani ilipungua kwa nusu kati ya mwaka 1990 hadi 2010, na tangu wakati huo imeshuka zaidi hadi watu milioni 736. Viwango vya kodi miongoni mwa watu wa kima cha juu vimeshuka katika mataifa tajiri miongo iliyopita.

Shirika hilo linapendekeza kuwa ikiwa watu tajiri duniani watalipa asilimia 0.5 ya ziada katika utajiri wao, itatosha kuwapatia elimu watoto milioni 262 ambao hivi sasa hawahudhurii shule na kutoa huduma za afya na kuokoa maisha ya watu milioni 3.3.

Ripoti hiyo imetolewa leo wakati viongozi wa dunia, matajiri na watu mashuhuri wakiwasili katika mji wa kifahari wa Davos, Uswisi katika kongamano la kila mwaka la kiuchumi.

Share:

DC MASASI ANENA ZAHANATI KUTUMIA CHOO CHA NYANSI

Share:

TETESI ZA SOKA ULAYA JAN 22,2019 , PAUL POGBA KUONGEZA MKATABA MAN U


Kiungo wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba , 25, yuko tayari kuketi chini na klabu yake kuzungumzia kuongezwa muda wa mkataba wake. (Sun)

Mshambuliaji wa United na Ufaransa Anthony Martial , 23, yuko karibu kuukubali mkataba mpya ugani Old Trafford. (ESPN)

Arsenal wanachunguza uwezakano wa kumsajili mchezaji wa Real Madrid na Colombia James Ridriguez kwa mkopo. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa hivi sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Bayern Munich. (Independent)

Eden Hazard , 28, amesema hatojiunga na Manchester United hata iwapo Zinedine Zidane atakuchua nafasi ya kuwa meneja na kudokeza kwamba atasalia Chelsea.(Star)

Bayern Munich wanachochewa kutoa ombi la £10m kwa mshambuliaji wa Manchester City na Wales Rabbi Matondo,18, ambaye mkataba wake utakamilika mwishoni mwa msimu.(Sun)Rabbi Matondo( wa pili kutoka kulia) Manchester City

Ombi la West Ham la yuro milioni 40 (£35.28m) lilikataliwa na Atalanta la kumsajili mshambuliaji wa kimataifa Duvan Zapata, 27. (Tuttosport, kupitia Calciomercato)

Cardiff wanajitayarisha kutoa ofa ya £2m kwa mshambuliaji wa Sunderland Josh Maja, lakini paka hao weusi wanahitaji £4m kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20. (Sun)

Manchester United wangependa kumuajiri mkurugezi wa soka kabla uamuzi maalum kuchukuliwa wa kumuajiri meneja wa kudumu kwa msimu huu. (Independent)

West Ham wamemwambia mshambuliaji Marko Arnautovic, 29, kwamba watamruhusu kuondoka , lakini hawatamuuza mwezi Januari- hata iwapo raia huyo wa Austria akikataa kucheza.(London Evening Standard)

Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata anatarajiwa kujiunga na Atletico Madrid kwa mkopo kwa siku zilizosalia za msimu huu , na matarajio ya klabu hiyo ya Ufaransa kumnunua kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26.(Sky Sports)

Nahodha wa Paris St-Germain,Thiago Silva amesema haitakuwa makosa kumruhusu kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot kuondoka katika klabu hiyo. Rabiot, 23, analengwa na klabu tofauti zinazoshiriki ligi ya Premia. (Telefoot, kupitia Talksport)

Mshambuliji wa Fulham Aboubakar Kamara, 23, yuko katika mazungumzo na upande wa Uturuki wa Yeni Malatyaspor kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu huu.(Mail)

Taaluma ya kiungo wa Fulham Kamara inaonekana kufikia kikomo pale kiungo huyo alipoamriwa kufanya mazoezi na klabu ya soka ya wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 23. (Telegraph)Aboubakar Kamara wa Fulham

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy yuko tayari kuchukua £5m kumuuza mshambuliaji Vincent Janssen, 24, mwezi huu, baada ya kumsaini mchezaji wa kimataifa kutoka Uholanzi kwa kitita cha £17m. (Telegraph)

Liverpool wanatarajiwa kuwa klabu ya kwanza ulimwenguni kuripoti faida waliyoipata kwa mwaka ya zaidi ya yuro milioni 100 (£88.3m). (Telegraph)

Winga wa Stewart Downing atajaribu kuutatua mzozo kati yake na klabu ya Middlesbrough wiki hii. Mchezaji huyo wa zamani wa England , 34, ambaye kwa hivi sasa hashiriki katika mchezo wowote kutokana na sababu kwamba klabu hiyo haitaki kujihusisha na mazungumzo ya kumuongezea mkataba wake wa mwaka mmoja, ambao unatarajiwa kuanza baada ya mkataba wa hapo awali. (Mail)

West Brom imehusishwa na beki wa Ipswich Jonas Knudsen, 26, ambaye mkataba wake unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa msimu huu.(Birmingham Mail)

Beki Tosin Adarabioyo, 21, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo na klabu ya West Brom anaweza kurudi Manchester City, kwani klabu hiyo inajaribu kumtafutia nafasi ya kushiriki michezo tofauti katika klabu nyengine.(Birmingham Mail)Romelu Lukaku (kushoto) na Alexis Sanchez (kulia)

Beki wa Stade de Reims Bjorn Engels, 24, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu inayoshiriki ligi ya Ligue 1 ya Olympiakos na anahusishwa na Everton , amedokeza itakuwa 'ndoto' kuichezea Arsenal.(Mirror)

Aston Villa inamnyemelea beki wa klabu ya Ufaransa ya Le Havre, Harold Moukoudi, 21, lakini ajenti wa mchezaji huyo amedokeza kwamba mchezaji huyo atajiunga na Ligue 1 msimu huu.(Birmingham Mail)

Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku , 25, alichapisha kwenye mtandao wa kijamii akikemea fununu za kuihamia Juventus.(Star)

Nottingham Forest wanaonekana kumzingatia kiungo wa kati raia wa Ubeligiji anayeichezea Scunthorpe Funso Ojo, 27 ambaye pia anahusishwa na klabu ya soka ya Derby County.(Nottingham Post)

Millwall wako karibu kufikia makubaliano na maafisa katika eneo la Lewisham kuikubali klabu hiyo kusalia kusini mwa London ili kuimarisha uwanja wao wa nyumbani wa New Den . (Guardian)
Share:

MKURUGENZI AZITAKA YANGA NA SIMBA KUTODHARAU MICHUANO YA SPORTPESA

Michuano ya SportPesa Super Cup mwaka 2019, inatarajia kuzinduliwa leo katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam kwa michezo miwili kupigwa.

Mchezo wa kwanza wa leo utakuwa ni kati ya Singida United na Bandari ya Kenya, majira ya saa 8:00 mchana huku Yanga ikiwakaribisha Kariobang Sharks ya hukohuko Kenya huku katika mchezo wa pili wa saa 10:00 jioni.

Kuelekea ufunguzi wa michuano hiyo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa SportPesa nchini, Abbas Tarimba, amevitaka klabu za Simba na Yanga kutumia vikosi vya kwanza ili kuepusha aibu ambayo imekuwa zikiionesha katika misimu miwili iliyopita.

"Imekuwa ni utamaduni wetu, Samahani nitatumia neno 'kudharau' haya mashindano, awamu hii hatutaki utani, tunataka kombe libaki nyumbani kwa maana kila siku limekuwa likienda nchi jirani. Tunavitaka vilabu vyote vya hapa nyumbani kuhakikisha vinafanya vizuri", amesema Tarimba.

"Nilivyokuwa naingia hapa nilikutana na kocha wa Yanga, nikamsisitiza kuwa hatutaki utani katika mashindano ya mwaka huu", ameongeza.

Awali, michuano hii ilikuwa ikifanyika mwezi Juni baada ya ligi kumalizika lakini Tarimba amesema kuwa imekuwa ikilalamikiwa na vilabu hasa vya Tanzania kuwa inapofika mwishoni mwa msimu, wachezaji wengi mikataba yao huwa inamalizika kwahiyo kukosa fursa ya kushiriki. 

Pia ameitaja sababu nyingine kuwa ni klabu hizo kutokuwa na muda mrefu wa maandalizi kutokana na ligi kumalizika, tofauti na timu za Kenya ambazo katika kipindi hicho ligi yao inakuwa inaendelea.

Mshindi wa michuano hiyo atajinyakulia kitita cha Dola za Kimarekani 30,000 ambazo ni takribani shilingi milioni 65 za Kitanzania, huku mshindi wa pili akijinyakulia Dola 10,000, wa tatu atapata Dola 7,500 na mshindi wa nne atapata Dola 5,000.
Share:

HATMA YA UBUNGE WA TUNDU LISSU NDUGAI ATAKAPOVAA JOHO


Hatma ya ubunge wa Tundu Lissu itajulikana kuanzia Januari 29 wakati Job Ndugai atakapovaa “joho” la uspika kuongoza Mkutano wa 14 wa chombo hicho cha kutunga sheria.

Ndugai amemtaka Lissu arejee nyumbani kuendelea na majukumu yake ya kuwawakilisha wananchi wa Singida Mashariki, akisema hana kibali baada ya mbunge huyo kutoa tamko mwishoni mwa wiki akituhumu kuwepo na mpango wa kumvua ubunge.

Lissu yuko nchini Ubelgiji kumalizia matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa ndani ya gari, nje ya makazi yake Area D mjini Dodoma, ikiwa ni saa chache baada ya kuhudhuria kikao cha Bunge.

Baada ya shambulio hilo la Septemba 7, mwaka juzi alipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kabla ya kusafirishwa kwa ndege kwenda Nairobi, Kenya usiku wa siku hiyo.

Mkutano huo wa 14 wa Bunge la Kumi na Moja utaanza Januari 29, siku saba kuanzia leo, pamoja na mambo mengine unatarajiwa kupokea ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), aliyehojiwa jana na Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge.

Majibizano kati ya Lissu na Spika Ndugai yamekuwa yakipamba moto siku hadi siku tangu alipotoa waraka alioupa jina la “Baada ya Risasi Kushindwa, Sasa Wanataka Kunivua Ubunge”. Katika waraka huo, Lissu anatuhumu uongozi wa Bunge na Serikali kuandaa mpango huo, jambo ambalo Ndugai amesema “ni uzushi”.

Jana, Mwananchi ilimuhoji tena Spika Ndugai kuhusu madai ya Lissu kuwa anafahamu taarifa za matatizo yake na kwamba alishiriki katika hatua za awali za kumuwezesha kupata matibabu, jambo ambalo alikubaliana nalo.

“Alipopata matatizo wote tulishuhudia na Bunge lilitimiza wajibu wake katika zile saa chache ambazo ni muhimu katika kuokoa maisha yake. Na hilo lilifanikiwa. Tunatambua kwamba mwenzetu aliumizwa na alikuwa hospitalini,” alisema Spika Ndugai.

“Ila sasa hivi tunavyoongea ametoka hospitali yuko huko aliko. Inaelekea ameruhusiwa. Amekuwa akitumia mwanya huo kuzunguka na kuchafua sifa ya nchi yetu. Kwani nani amempa ruhusa?

“Sasa nimwambie tu kwamba sisi tunamuhitaji maana mpaka sasa hajawahi kuniandikia chochote mimi kama kiongozi wake bungeni na wala daktari wake hajasema kitu. Kwa maana hiyo, mimi namuhesabu kama ni mtoro.”

Alipoulizwa sababu za muhimili huo kushindwa kumuhudumia Lissu licha ya familia yake kuandika barua mara nne, Ndugai alijibu kwa kifupi: “Hayo ya nyuma tuyaache. Atakapokuja mwenyewe tutayazungumza.”

‘Nilienda BBC nikitokea hospitali’

Na Tausi Mbowe, Mwananchi 
Share:

WAHAMIAJI HARAMU 81 WANASWA DAR MSAKO SEHEMU ZA KAZI, NYUMBANI

Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, imeanza kusaka wahamiaji haramu kwenye makazi na sehemu za kazi, ikiwamo kuwachukuliwa hatua za kisheria.


Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Ofisa Uhamiaji Mkoa, Kamishna Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiani, Novaita Mroso, alisema operesheni maalum imefanyika na inaendelea.

Alisema wameamua kuwasaka wahamiaji haramu kwenye mitaa, ili kuweza kuwadhibiti zaidi.

“Tukishindwa kukupata eneo la kazi tutakufuata nyumbani, kwa utaratibu tuliojiwekea Dar es Salaam, siyo sehemu salama kuwa maficho kwa wahamiaji haramu. Yeyote anayeajiri raia wa kigeni ahakikishe ana vibali vyote vya kuishi nchini,” alisema.

Alisema ilianza Januari 17 mwaka huu, na hadi jana ilikuwa na siku tano na jumla ya wahamiaji 81, ambao wanatuhumiwa kwa makosa mbalimbali walitiwa mbaroni.

“Kati yao tumebaini 35 wanatoka nchini Burundi, waliobaki wanatoka Somalia na Congo, wengine 46 wanaendelea kuchunguzwa na baada ya kukamilika tutabaini uhalali wao wa kuwapo nchini,” alisema.


Mroso alisema waliobainika kuwa ni wahamiaji haramu watachukuliwa hatua za kuwafikisha mahakamani na kuwafukuza nchini.


“Operesheni maalum ni sehemu ya jukumu letu la udhibiti wa wahamiaji haramu. Pia tumekuwa tukifanya uhakiki wa taarifa za wageni waliopo Mkoa wa Dar es Salaam ambao wamejiajiri au kuajiriwa,” alisema.
Share:

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO JANUARI 22,2019.

Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 22, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Source

Share:

Monday 21 January 2019

KAMATI YA MAADILI YA BUNGE YAMHOJI CAG

Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge imemhoji Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuhusu kauli yake ya “udhaifu wa Bunge.” CAG amehojiwa mapema leo Januari 21, 2019 ambapo mara baada ya mahojiano hayo Mwenyekiti wa kamati hiyo, Emmanuel  Mwakasaka amesema atawaeleza waandishi wa habari kilichojiri katika kikao hicho. Prof. Assad ameitwa mbele ya kamati hiyo kujieleza kuhusu kauli aliyoitoa wakati akijibu swali la mwandishi wa televisheni ya UN, Anord Kayanda kuhusu kutoshughulikiwa ipasavyo kwa ripoti zake zinazoonyesha ufisadi. “Kama tunatoa ripoti na…

Source

Share:

WHATSAPP NA FACEBOOK ZAWEKA KIKOMO IDAIDI YA MESEJI

Watoa huduma wa mitandao ya kijamii ya 'Whatsapp' na 'Facebook' wamepunguza kiwango cha kusambaza ujumbe mfupi wa maandishi ambapo sasa mtumiaji hatoweza kusambaza ujumbe kwa watu zaidi ya watano.
Watoa huduma wamefikia hatua hiyo ili kupunguza tabia za watu kuzusha na kuibua taharuki katika mitandao, kupitia taarifa wanazosambaza.

Hapo awali, mtumiaji wa Whatsapp angeweza kupeleka ujumbe kwa watu 20 au makundi zaidi ya moja kulingana na makundi aliyonayo.

Whatsapp, ambayo ina watumiaji wapatao bilioni 1.5, imekuwa ikijaribu kutafuta njia za kuacha matumizi mabaya ya programu, kufuatia wasiwasi wa kimataifa kuwa jukwaa hilo lilikuwa linatumika kueneza habari zisizo na ukweli.
Share:

SERIKALI YAKANUSHA KIKUNDI KUITISHIA TANZANIA

Kwa siku kadhaa za hivi karibuni kumekuwa na taarifa inayosambaa kwa njia ya video ambayo inaonesha kikundi cha watu wakiwa wameketi, wakitumia lugha ya Kiswahili kutishia kuvamia na kushambulia baadhi ya nchi kadhaa za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania.
Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Serikali imesema, "baada ya uchunguzi wetu tumebaini ilirushwa mwaka 2016 na Kituo cha Televisheni cha China (CCTV-Afrika), ikielezea hisia za uwepo wa viashiria vya kundi la Al-Shaabab nchini Tanzania.

Imeendelea kusema taarifa hiyo kuwa, msingi wa taarifa hiyo ya mwaka 2016 ni ripoti yenye kurasa 53 iliyoandaliwa na wataalamu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Mashariki mwa Afrika (IGAD), ambayo hata hivyo haikujikita kwenye utafiti wowote wa moja kwa moja kuhusu Tanzania bali hisia za watu na makundi mbalimbali katika nchi za Kenya, Ethiopia na Somalia.

"Tumewasiliana na wamiliki wa CCTV-Afrika na wamekiri kuwa sio wao walioisambaza tena video hiyo, ikionekana dhahiri kuwa kuna watu wenye nia mbaya na nchi yetu wameitumiavideo hiyo ya mwaka 2016 kwa malengo yao hasi dhidi ya Tanzania".

Serikali imesema kuwa kwa kushirikiana na CCTV yenyewe inawataka wananchi kupuuzia taarifa zozote zenye lengo la kuipaka matope Tanzania na kuihusisha na kundi lolote la kigaidi.

Pia serikali imeusisitizia umma kuwa Tanzania iko salama, na vyombo vyake vya ulinzi na usalama viko makini kufuatilia na kuchukua hatua iwapo kuna viashiria vyovyote vya kuharibu amani.
Chanzo : Eatv
Share:

IFAHAMU RATIBA YA VIPORO VYA SIMBA

Klabu ya soka ya Simba inakabiliwa na ratiba ngumu ya michezo yake ya ligi kuu pamoja na ile ya kimatafa ambapo mara baada ya michuano ya Sportpesa Super Cup inayoanza 22/01/2018 hadi 27/01/2019 timu hiyo itaondoka kwenda Misri kwa ajili ya kukipiga na Al Ahly.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Februari 2, 2019 saa 3 usiku kwa saa za Misri na saa 4 usiku kwa saa za Tanzania na baada ya mechi hiyo Simba itarejea nchini kucheza na Mwadui FC Februari 6, 2019 kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam.

Baada ya mchezo dhidi ya Mwadui Simba itajiandaa na mchezo wa marudiano na Al Ahly utakaopigwa jijini Dar es salaam Februari 12, 2019 10:00 jioni.

Baada ya mchezo dhidi ya Al Ahly Simba itakuwa na siku 4 za kujiandaa na mchezo dhidi ya Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara timu ya Yanga mchezo ambao utapigwa Februari 16, 2019 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Ratiba ya mechi zingine.
19/02/2019
Africa Lyon Vs Simba - Dsm
22/02/2019
Azam Vs Simba - Dsm
26/02/2019
Lipuli vs Simba - Iringa
03/03/2019
Stand United Vs Simba - Shinyanga

Baada ya hapo Simba itarejea Dar es salaam kujiandaa na michezo ya klabu bingwa Afrika ambapo Machi 9, 2019 itakuwa ugenini kucheza na JS Saoura utakaopigwa saa 2:00 usiku kwa saa za Algeria na saa 4:00 usiku kwa saa za Tanzania.

Kisha itacheza mchezo wa misho kwenye makundi ambao utapigwa jijini Dar es salaam Machi 16, 2019 dhidi ya AS Vita Club kwenye uwanja wa taifa. Kisha itamaliza mwezi Machi kwa kucheza mechi mbili za ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting na Mbao FC ambazo zote zitapigwa Dar es salaam.
Share:

SIASA ZAKWAMISHA UJENZI WA KITUO CHA AFYA HAMAI

Na,mwandishi Wetu Jumla ya milion 600 zilizotengwa kwenye  Mradi wa  ujenzi wa kituo cha afya Hamai wilayani chemba mkoani Dodoma  zimeshindwa kutumika ipasavyo kufuatia halimashauri kukosa wahandisi pamoja na kuchelewa kwa manunuzi ya vifaa vya ujezi na ufuatiliaji hafifu huku siasa zikichangia kwa kiasi kikubwa.   Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la ujenzi wa kituo hicho, Mganga Mkuu wa Wilaya ya chemba  Dk Olden Ngassa amesema moja ya changamoto imechangiwa na halimashauri kukosa wahandisi wa ujenzi kwa muda mrefu ambao ndio wasimamizi wakuu wa kazi za ujenzi pamoja na ushiriki…

Source

Share:

BILLIONI 5.4 KUJENGA MAGHALA MAKUBWA YA KISASA WILAYANI RUANGWA.

Na Bakari Chijumba, Mtwara. Utiaji wa saini kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa na Mkandarasi Tendar International constraction company limited, watakaotelekeza kandarasi yote ya ujenzi wa maghala ya kisasa wilayani Ruangwa Mkoani Lindi, umefanyika leo Jumatatu, 21 Januari 2019. Halfa fupi ya kusaini kandarasi hiyo imefanyika katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, ambapo jumla ya majengo nane muhimu yatajengwa, likiwemo jengo la utawala, maghala mawili, Kantini, Majengo ya kupimia uzito, Mnara wa kuwekea matanki ya maji na jengo kuhifadhia vitu vya umeme, ambayo yote kwa pamoja yanatarajiwa kukamilika ndani ya…

Source

Share:

BARAZA LA MAWAZIRI LARIDHIA KUIFUTIA ZECO DENI LA VAT LA BILIONI 22.9

Baraza la Mawaziri limeridhia utozwaji wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa kiwango cha asilimia sifuri kwenye umeme unaouzwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa Shirika la Umeme la Zanzibar (ZECO) na kufuta malimbikizo ya deni la kodi ya VAT lililofikia shilingi Bilioni 22.9 kwa TANESCO kwenye umeme uliouzwa ZECO. Baraza la Mawaziri limefanya uamuzi huo leo tarehe 21 Januari, 2019 Ikulu Jijini Dar es Salaam, katika kikao kilichoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais…

Source

Share:

KATIBU WA CCM WILAYA AKAMATWA KWENYE MAANDAMANO

Katibu wa CCM wilaya ya Hai, Laurence Kumotola, amekamatwa na polisi kwa tuhuma ya kuwazuia askari kufanya kazi yao ya ulinzi, wakati wakitaka kuingia katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Hai.

Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 5:45 asubuhi, wakati katibu huyo akiwa ameambatana na wafuasi wa chama hicho pamoja na viongozi mbalimbali, walipodaiwa kuvamia ofisi ya mkuu wa wilaya kwa maandamano na kuzuia watu kuingia katika ofisi hizo hadi wao watakaporuhusiwa na kusikilizwa na mkuu wa wilaya hiyo, Lengai Ole Sabaya.

Katibu huyo akiwa na wafuasi hao, walitumia zaidi ya dakika 10 wakiwa katika geti la kuingia katika ofisi hizo, hadi pale mkuu wa wilaya ya Hai alipotoka na kuruhusu wafunguliwe awasikilize.

Wakati mkuu huyo wa wilaya akizungumza na watu hao, ndipo mkuu wa polisi wilaya ya Hai, Lwelwe Mpina alipoingia na kumwambia mkuu wa wilaya kuwa anamkamata katibu wa CCM kwa kuwa amemzuia kufanya kazi yake.

"Mkuu naomba kumchukua katibu, amenizuia kuingia hapa wakati mimi ndiye nasimamia ulinzi na usalama hapa," alisema OCD.

Akizungumza na waandamanaji hao, Lengai Ole Sabaya amesema hakuna kiongozi yeyote atakayeruhusiwa kulizuia jeshi kufanya kazi na yeyote atakayefanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.

"Tumesitisha ufanyaji wa siasa kwa vyama vyote kwa sababu uchaguzi bado haujafika na hata tulipofikia kwa sasa mtu yeyote atakayehusika kulizuia jeshi la polisi achukuliwe hatua."

"Na nyinyi CCM kama mnalalamika mtumie njia ambayo ni rasmi lakini si kufanya maandamano." ameongeza Sabaya
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger