Monday 31 October 2016
Rais Magufuli afanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)
Rais
wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe
30 Oktoba, 2016 amemteua Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara kuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza tarehe 29 Oktoba, 2016.
Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu.
WAKATI
HUO HUO,Rais Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Eligy Mussa Shirima kuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI)
Uteuzi wa Dkt.Shirima umeanza tarehe 29 Oktoba 2016.
Kabla
ya uteuzi huu Dkt. Eligy Mussa Shirima alikuwa Mtafiti Mkuu na
Msimamizi wa Utafiti wa Nyama ya Ng'ombe Makao Makuu ya TALIRI.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Rais Magufuli kufanya ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Kenya Kuanzia Kesho
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe
31 Oktoba, 2016 ataanza ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Kenya
kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.
Rais
Magufuli anatarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Jomo Kenyatta Jijini Nairobi majira ya saa nne asubuhi na baadaye
kupokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi
ambako viongozi hao watafanya mazungumzo rasmi.
Pamoja
na kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais Magufuli atakwenda
kutoa heshima katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo
Kenyatta na pia anatarajiwa kuhudhuria dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na
mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta Ikulu Jijini Nairobi
Katika
ziara hii Rais Magufuli anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha
Eldoville kilichopo Karen Jijini Nairobi, na pia anatarajiwa kuzindua
barabara mchepuko ya Southern By-pass iliyopo Jijini Nairobi.
Barabara
hiyo mchepuko ya Southern By-pass ni moja kati ya miradi mikubwa ya
barabara nchini Kenya, inaunganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi
kwa barabara za juu na chini na imejengwa kwa lengo la kupunguza
msongamano wa magari katika Jiji hilo.
Rais Magufuli anatarajiwa kumaliza ziara yake tarehe 01 Novemba, 2016 na kurejea Jijini Dar es Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Basi La Abiria Lateketea Kwa Moto Kimara Stop Over Jijini Dar,Mtu mmoja Afariki, 16 Wajeruhiwa
Basi lenye namba za usajili T990 AQF mali ya kampuni ya Safari Njema liililokuwa likitokea Dodoma kuja jijini Dar, jana liliteketea
kwa Moto maeneo ya Kimara Stop Over-Suka, mara baada ya kugongana na
Lori lililokuwa limebeba shehena ya mifuko ya Cement (namba zake za
usajili hazikujulikana mara moja).
Imeelezwa kuwa mali zote zilikuwemo katika basi vimeteketea kabisa kwa moto.
Imeelezwa kuwa mali zote zilikuwemo katika basi vimeteketea kabisa kwa moto.
Jeshi
la Polisi limeeleza kuwa mtu mmoja amefariki Dunia katika ajali hiyo na
wengine 16 wamejeruhiwa na baadae kukimbizwa Hospitali ya Taifa
Muhimbili kwa matibabu.
Sunday 30 October 2016
MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO CHUO KIKUU SAUT 2016/2017,BOOM LARUDISHWA 8500 KWA SIKU
Kama utahitaji kuangaliziwa jina lako kwa "usahihi" na "kasi ya ajabu" (ambapo utajibiwa ndani ya dk 1 tu) kama limepata mkopo tafadhali fanya yafuatayo;
1.TUMA EXAM NAMBA YAKO YA FORM 4 NA MWAKA
ULIOMALIZA MFANO:S3409.0012.2013-HESLB KWENDA
NAMBA 0652740927
2.HUDUMA HII UTATOZWA TSHS 1000 TU(KWA AJILI YA
KUISUPORT MASWAYETU BLOG)
3.TUMA PESA KWENDA 0768260834-MPESA
0652740927 -TIGO PESA
&AIRTEL MONEY
4.UTAJIBIWA NDANI YA DK 1 TU.
5.TUMA PESA KWANZA,NDIO UTAJIBIWA SMS YAKO
KUOANA MAJINA
<<BONYEZA HAPA>>
HESLB yafafanua vigezo utoaji mikopo, Waliokosa sababu zatajwa, wapewa nafasi ya kukata rufaa
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo Bw. Abdul-Razaq Badru akifafanua jambo katika mkutano na wanahabari jijini Dar es Salaam leo (Jumapili, Oktoba 30, 2016). Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi hiyo Bw. Cosmas Mwaisobwa.
HESLB yafafanua vigezo utoaji mikopo, Waliokosa sababu zatajwa, wapewa nafasi ya kukata rufaa
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo Bw. Abdul-Razaq Badru akifafanua jambo katika mkutano na wanahabari jijini Dar es Salaam leo (Jumapili, Oktoba 30, 2016). Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi hiyo Bw. Cosmas Mwaisobwa.
Kimara, Dar: Basi likitokea Dodoma lagongana na Lori; magari yateketea kwa moto
Basi la Kampuni ya Safari njema lililokuwa likitokea Dodoma kuelekea Dar es Salama. Limegongana na Lori katika eneo la Kimara Stopover.
Kuna ajali mbaya sana imetokea hapa eneo la Suca Mbele kidogo ya stop over ikihusisha lori na Basi T 990 ADF liitwalo Safari njema linalofanya safari zake kati ya Dar na Dodoma linaungua. SASA hivi yanaungua na watu waliokuwemo ndani.
Saturday 29 October 2016
Taarifa ya Mamlaka ya Dawa na Chakula TFDA kuhusu Dawa bandia zilizokamatwa
Na Ally Daud-Maelezo
MADAWA
bandia na yasiyo sahihi kwa matumizi ya binadamu yamekamatwa maeneo ya
Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini baada ya kufanyika ukaguzi maalum
wa kutafuta dawa bandia katika maeneo hayo iliyofanyika hivi karibuni.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw.
Hiiti Sillo wakati wa kutoa Matokeo ya ukaguzi maalum wa dawa
uliofanyika katika mikoa ya Kanda za Ziwa na Nyanda za Juu Kusini.
“Kutokana
na ukaguzi maalum tulioufanya katika Kanda za Ziwa pamoja na Nyanda za
Juu Kusini wa kutafuta dawa bandia na zisizo sahihi kwa matumizi ya
binadamu tumefanikiwa kukamata dawa bandia za aina tano ambazo zipo
kwenye makundi mawili ya Dawa za malaria na Viua vijasumu(Antibiotics)” alisema Bw. Sillo.
Aidha
Bw. Sillo amesema kuwa ukaguzi huo maalum umeweza kusaidia kukamata
dawa ya malaria aina ya vidonge vya Quinine ambayo inadaiwa kutengenezwa
katika kiwanda cha Elys Chemical nchini Kenya na nyingine
zinatengenezwa hapa nchini katika kiwanda cha Shelys Phamaceuticals Ltd.
Mbali
na hayo Bw. Sillo amesema kuwa pamoja na kukamata dawa bandia pia zoezi
hilo lilifanikiwa kubaini na kukamata dawa zilizoisha muda wa matumizi ,
zisizosajiliwa na zenye ubora duni zenye thamani ya Tsh. Milioni
17.463.
Bw.
Sillo ameongeza kuwa Ukaguzi huo ulitokana na kuwa na taarifa za awali
ambazo zilionyesha uwepo wa dawa bandia katika maeneo ya Geita na Mara
mwezi Agosti na Septemba mwaka huu na kusistiza kwamba zoezi hilo la
ukaguzi linaendelea nchini kote na watakaokutwa na hatia watachukuliwa
hatua stahiki.
Kwa
upande wa Msajili wa Baraza la famasi Bi. Elizabeth Shekalaghe amesema
kuwa wataalamu wa madawa watakaokutwa na hatia ya kusambaza na
kuhudumia dawa bandia watafutiwa usajili na kuacha kutoa huduma kwa
mujibu wa sheria ya dawa , chakula na vipodozi.
“Wataalamu
wa dawa ambao wanasambaza na kuhudumia dawa bandia watafutiwa usajili
na kuacha kutoa huduma kwa mujibu wa sheria ya dawa , chakula na
vipodozi pindi watapogundulika” alisema Bi. Shekalaghe.