Monday 30 May 2016

Naibu Waziri Wa Mambo Ya Ndani Ya Nchi Afanya Ziara Gereza la Msalato – Dodoma

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema Serikali imejipanga kulitumia Jeshi la Magereza kuhakikisha Tanzania inaingia kwenye uchumi wa viwanda.

Lengo hilo ni mkakati wa wizara kutaka kuendana na kauli ya Rais John Magufuli ambaye amekuwa akisisitiza kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kuelekea kwenye uchumi wa kati ifikapo 2025.

Masauni aliyasema hayo jana alipotembelea mradi wa kiwanda cha kokoto cha Gereza la Msalato kilichopo Dodoma. Alisema Magereza ina rasilimali nyingi ambazo zikitumika kikamilifu zinaweza kuifanya nchi kupiga hatua.

 Alisema kuna fursa nyingi ambazo jeshi hilo linaweza kuzitumia kufikia azma hiyo, ikiwamo kuanzisha kiwanda cha viatu kwa ajili ya askari wa majeshi mbalimbali.

 “Inashangaza kuona majeshi yetu yananunua viatu kutoka nje wakati vinaweza kutengenezwa na Magereza. Lazima tujipange na ninaamini Jeshi la Magereza linaweza kuifanya kazi hiyo,” alisema Masauni. 

Akizungumzia mradi wa kokoto wa gereza hilo, alisema zinahitajika Sh2.5 bilioni kwa ajili ya uwekezaji katika mradi huo.

 Alisema kiwanda hicho kikianza kazi kitakuwa na uwezo wa kukusanya mapato ya Sh6.8 bilioni kwa mwaka. Alisema kuna namna mbalimbali jeshi hilo linaweza kupata mtaji huo ikiwa ni pamoja na kuomba mkopo kwenye benki za nchini, kuingia ubia na mwekezaji au kupata ruzuku kutoka serikalini.

“Nataka Magereza watafute namna ya kupata fedha hizo bila kusubiri ruzuku kutoka serikalini. Najua watapata fedha hiyo kwa sababu mradi huu ni mkubwa na utalifanya jeshi hili kuongeza mapato,” alisema.

 Masauni aliongeza kuwa anataka kuona siku moja jeshi hilo linajiendesha kwa kujitegemea kuanzia kwenye chakula cha wafungwa mpaka miundombinu yake.

Alisema hilo litawezekana kama watawekeza kwenye viwanda. Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Patrick Nasola alisema mradi huo utaendeshwa na jeshi hilo na kuwa watakuwa tayari kumuuzia mtu yoyote kokoto watakazozalisha.

Alisema mradi huo ukianza kazi utakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 15 za kokoto kwa siku. Alisema changamoto wanayokabiliana nayo ni uhaba wa fedha kwa ajili ya kutengeneza mtambo wao ambao sasa umeharibika.

“Walikuja wataalamu katika eneo hili la Msalato kupima wakabaini kuna madini mawe mengi na sasa tuna leseni 15 kwa ajili ya madini mawe. Mawe yaliyopo hapa ni kama yale yanayotumika kutengeneza tiles,” alifafanua.

Nasola aliongeza kuwa wataweza kuzalisha fedha nyingi kutokana na mradi huo kwa sababu ni eneo kubwa ambalo kwa ujumla wake lina madini mawe ya kutosha. Alisema wanatarajia kuuza zaidi kokoto ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato utakapoanza.

Kwa upande wake, Mkuu wa Gereza la Msalato, Steven Mwihambi alisema kokoto ni moja ya miradi inayofanyika katika gereza hilo.

Alitaja miradi mingine kuwa ni ufugaji, kilimo na utengenezaji wa samani. “Tutaanzisha viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya mazao tunayozalisha kama vile alizeti. Changamoto kubwa ni uhaba wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mipango yetu,” alisema kiongozi huyo wa gereza.
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATATU MAY 30 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Sunday 29 May 2016

PICHA:HATIMAE HOSTELI ZA WAMI ZAPATA MAJI BAADA KUTOKUWA NA MAJI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY



Share:

HIZI HAPA SIFA ZA KUSOMEA KOZI ZA ARCHTECTURE,CIVIL ENGINEERING,ELECTRONIC,MECHANICAL ,COMPUTER ENGINEERING CHUO KIKUU CHA MBEYA 2016/2017

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


BACHELOR DEGREE PROGRAMMES IN:-
(i) Technology in Architecture
(ii) Civil Engineering
(iii) Electrical and Electronics Engineering
(iv) Mechanical Engineering
(v) Computer Engineering
(vi) Business Administration



<<<<<<<BONYEZA HAPA KUSOMA SIFA HIZO>>>>>
Share:

ANGALIA HAPA ADA ZA KOZI MBALIMBALI CHUO KIKUU CHA ARUSHA UNIVERSITY 2016/2017

Share:

HAYA HAPA MATOKEO YA WANAFUNZI WA ST.JOSEPH WANAOSOMA UDAKTARI MUHULA WA KWANZA 2016

Share:

MPYA:UFAFANUZI KUHUSU SIFA ZA WANAFUNZI WATANO WALIOTAJWA KWENYE HOTUBA YA WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI MHESHIMIWA PROF. JOYCE LAZARO NDALICHAKO (MB.) 26.5.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY



 BONYEZA HAPA KUSOMA TAARIFA KAMILI
Share:

MPYA:ST.JOSEPH UNIVERSITY WAMJIBU WAZIRI WA ELIMU KUHUSU KUTOA SHAHADA YA MIAKA 5 KWA WANAFUNZI WALIOMALIZA FORM 4

Share:

PICHA 20 : Real Madrid walivyowasili jijini Madrid na Kombe lao la 11 la UEFA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Klabu ya Real Madrid ya Hispania usiku wa May 28 2016 ilicheza mchezo wake wa fainali ya Klabu Bingwa barani dhidi ya Atletico Madrid katika jiji la Milan Italia uwanja wa San Siro, hiyo ilikuwa fainali inayohusisha timu kutoka jiji moja la Madrid, hivyo upinzani ulikuwa mkubwa.
34BD6C4C00000578-3614796-image-a-48_1464504236963
Katika mchezo huo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid walifanikiwa kutwaa Kombe lao 11, huku Atletico wakiambulia kushindwa kuweka rekodi ya kutwaa Kombe hilo kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu yao, Real Madrid walifanikiwa kuifunga Atletico kwa mikwaju ya penati 5-3, hiyo ni baada ya dakika 12o kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
34BD66F500000578-3614796-image-a-22_1464503599415
Baada ya Ubingwa Real Madrid waliwasili Hispania katika jiji la Madrid wakiwa na Kombe lao la 11 la UEFA.
34BD6C1E00000578-3614796-image-a-45_1464504191608
34BD773C00000578-3614796-image-a-77_1464506697932
34BD766800000578-3614796-image-a-76_1464506653595
34BD678600000578-3614796-Real_defenders_Pepe_left_and_Sergio_Ramos_take_great_joy_in_show-a-70_1464506190953
34BD756B00000578-3614796-image-a-71_1464506198205
34BD669100000578-3614796-image-a-18_1464503516180
34BD669900000578-3614796-image-a-14_1464503375014
34BD73FA00000578-3614796-image-a-74_1464506237864
34BD66AD00000578-3614796-image-a-15_1464503379819
34BD697F00000578-3614796-image-a-11_1464503333305
34BD72F200000578-3614796-image-a-67_1464506149164
34BD6C4700000578-3614796-image-a-44_1464504148538
34BD672500000578-3614796-image-a-9_1464503301070
34BD673D00000578-3614796-image-a-8_1464503271387
34BD607D00000578-3614796-image-a-5_1464503197718
34BD605100000578-3614796-image-a-4_1464503170204
34BD6C5800000578-3614796-image-a-50_1464504284645
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger